TANZIA Naibu Kamishna Mstaafu wa Polisi (DCP) Michael Kamuhanda Afariki Dunia

TANZIA Naibu Kamishna Mstaafu wa Polisi (DCP) Michael Kamuhanda Afariki Dunia

1746266958932.jpg
 
Pale kinondoni walimchukua Mgombea nafasi Fulani wa chadema mhehe mmoja hivi akiwa katika kujumuika pool table kilichotokea ni maumivu makubwa.
 
TOKA MAKTABA

7 JUNI 2013
(IGP), Said Mwema amefanya mabadiliko ya makamanda wa mikoa
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema amefanya mabadiliko ya makamanda na wakuu wa Upelelezi wa Jinai, huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda akirejeshwa makao makuu ya jeshi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso nafasi ya Kamuhanda, ambaye hivi karibuni alipandishwa cheo na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Ramadhani Mungi ambaye alikuwa Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa Maalumu wa Kinondoni, Charles Kenyela amehamishiwa Makao Makuu na atakuwa kwenye Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Arusha (ACP), Camilius Wambura.

Taarifa hiyo ilieleza zaidi kuwa, DCP Ally Mlege aliyekuwa Makao Makuu ya Polisi amehamishiwa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwa Mkuu wa Utawala na Rasilimaliwatu.
Aidha, taarifa hiyo ilieleza kuwa, ACP Duwan Nyanda, ambaye yuko Makao Makuu ya Upelelezi atakuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Arusha.

Kamuhanda na Mwangosi
Wadau wa sekta ya habari na wanaharakati hawatamsahau Kamuhanda alipokuwa Kamanda wa Mkoa wa Iringa kutokana na tukio la Septemba 2, mwaka jana 2012 wakati polisi mkoani humo walipomuua Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi katika Kijiji cha Nyololo.

Mwandishi huyo alikufa hatua chache alipokuwa Kamuhanda ambaye kabla, alishuhudia polisi wake wakimshambulia kwa kipigo Marehemu Mwangosi.

Mwangosi na waandishi wengine wa habari walikuwa wakifuatilia mvutano wa polisi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho kilikuwa kikitaka kufungua tawi lake katika Kijiji cha Nyololo, wakati polisi walikuwa wakizuia kufanyika kwa uzinduzi huo.


Wakati shughuli za uzinduzi wa tawi la Nyololo ukiendelea, DCP Kamuhanda alifika katika eneo hilo na kuamuru viongozi wa CHADEMA wakamatwe lakini wafuasi wa chama hicho walipinga na yeye aliamuru kupigwa kwa mabomu ya machozi.


DCP Kamuhanda ni kati ya watu wanaotuhumiwa kusababisha kifo cha Mwangosi baada ya kutajwa na Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi na ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Kamanda huyo wa zamani anatuhumiwa kuvunja Sheria ya vyama vya siasa, kifungu cha 11 (a) na (b) na Sheria ya Polisi (Sura ya 322) kwa kuingilia kazi za Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi na kutoa amri ya kuzuia shughuli za Chadema wakati yeye hakuwa na dhamana hiyo katika eneo husika.
Mwananchi
 
Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi na ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Makamanda wa polisi toka muda huo 2012 hadi sasa 2026 pamoja na kupigwa msasa kwa kupelekwa kozi mbalimbali za uongozi chini ya Dr. Lazaro Mambosasa, wameamua kupotezea Kumbukumbu za Kitaasisi Institutional Memory kwa makusudi mbali ya kuwa Tume Ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuonesha mapungufu yao katika utekelezaji wa haki


TOKA MAKTABA:

tober 11, 2012​


RIPOTI YA KAMATI YA NCHIMBI KUHUSU MAUAJI YA MWANGOSI YAUMBULIWA VIBAYA NA TUME YA UTAWALA BORA NA HAKI ZA BINADAMU YA JAJI AMIR MANENTO...​

  • RPC WA IRINGA MICHAEL KAMUHANDA, ​

  • MSAJILI WA VYAMA JOHN TENDWA WABAINIKA KUVUNJA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI KUELEKEA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI WA CHANNEL TEN​

​
Jaji Kiongozi Mstaafu, Amir Manento akionyesha ripoti ya Tume ya Utawala Bora na Haki za Binadamu mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam..
​
Msajili wa Vyama vya siasa, John Tendwa.
​
Michael Kamuhanda, RPC wa Iringa

​
Mwangosi akishambuliwa na rundo la Polisi kabla ya kuuawa kwa bomu.
​
Picha imeondelewa kuhifadhi utu wa mwandishi Mwangosi
​
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kamati ya kuchunguza mauaji ya Mwangosi
 
Naibu Kamishna Mstaafu wa Polisi (DCP) Michael Kamuhanda amefariki Januari 29, 2026 majira ya Asubuhi katika Hospitali ya Bugando Jijini Mwanza alikokuwa anapatiwa Matibabu.

View attachment 3536765

Huyu jamaa alokufa alizaliwa 1954

Huyu mwamba ndiye aliyekuwa mstari wa mbele siku Mwangosi analipuliwa bomu la tumbo na wala mwamba haikumshtua...

Leo hii ardhi imemchukua na yeye pia, sijui kama alifanikiwa kutubu...
 
Back
Top Bottom