Siungi mkono hoja hii. Rais anahamasisha tuchape kazi. Hivyo, yeye, mawaziri, wabunge wawe mfano kwa kuendelea na majukumu yao kama watanzania wengine.All in all,mikusanyiko, ikiwemo ya vikao vya Bunge,ndio huchangia kusambaa kwa maambukizi na hii ndio hoja ya msingi hapa.
Wanaogopa watalii wasijewakaacha kwenda dodomaMaajabu ni kwamba, huyo mbunge wamemgundua kuwa na Corona huko Dodoma siku tano zilizopita lakini mpaka leo hii waziri wa Afya hajatuambia kama Dodoma kuna Corona tayari.
Sijui tunafichwa nini?
Na tutafichwa mpaka lini?
Kwa Tulia yupo kwenye ile list ya wazungumzaji wa corona.Waziri husika yuko wapi atuambie kuhusu na Watanzania wengine amekua kimya sana.
Ni shida kubwa sana. Watu wanatangaza kumuomba Mungu kwa siku tatu alafu wanaishi maisha ya kishetani ya kutowaambia wananchi ukweli. Shetani ni baba wa uongo na Mungu ni Baba wa ukweli.Maajabu ni kwamba, huyo mbunge wamemgundua kuwa na Corona huko Dodoma siku tano zilizopita lakini mpaka leo hii waziri wa Afya hajatuambia kama Dodoma kuna Corona tayari.
Sijui tunafichwa nini?
Na tutafichwa mpaka lini?
Ohhhoooo wameshauleta DodomaJambo la kujiuliza na linalohitaji hatua za kuchukua, mbunge huyu hakuwahi kuingia Bungeni? Kama aliwahi kuingia Bungeni, wabunge wataruhusiwa waendelee kuchangamana na watu wengine au tayari wapo karantini?
Hakika,na usishangae wakaanza kukimbia vikao vya Bunge.Corona inawapenda zaidi
Nakwambia baada ya muda watalazimika kurudi tena kwenye lockdown maana hiyo ndio njia pekee ya kudhibiti huo ugonjwa.Wazungu mnaowategemea lockdown imewashinda sasa wanarudi kazini na maambukizi yakiwa yanaendelea na watu wanakufa bado sembuse Tanzania?
Tiba hakuna, chanjo hakuna halafu unataka lockdown, tutafungiwa mwaka mzima na mwisho wake ni nini?
Kazi ziendelee kama kawaida huku tukichukua tahadhali kwa namna ambavyo wataalamu wa afya wanashauri