Naibu Spika Tulia Ackson athibitisha Mbunge mmoja kupata maambukizi ya COVID-19

Naibu Spika Tulia Ackson athibitisha Mbunge mmoja kupata maambukizi ya COVID-19

Ipo haja ya viongozi wetu kujitathimini kama wanawajibika kutokana na makosa yao
kosa linaweza likagharimu maisha na vizazi vyetu
Kosa linaweza geuka kovu lisilosahaulika
Kosa linaweza weka historia ya vizazi na vizazi
Kosa linaweza chochea hasira miongoni mwetu.
Tuache kuendelea kufanya makosa
 
Papaa Mobimba,
Kilichonishangaza ni kuona huku Tanzania VIP wanafichwa wakati huko Ulaya, Marekani na Asia wanawekwa wazi kwa Umma.
 
Nakumbuka kabla Bunge halijaanza, Zitto alishauri Bunge lisogezwe mbele hadi mwezi May mwaka huu kutegemeana na hali ya ugonjwa ikoje lengo likiwa ni kuwalinda wabunge wasipate ugonjwa huu wa corona.

Kama kawida, wenye mamlaka wazo hili hawakulifanyia kazi na vikao vya Bunge vikaanza kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali ambapo vikao vilianza tarehe 31 mwezi March mwaka huu.

Leo hii ikiwa ni wiki takribani tatu, teyari tumepata mgonjwa wa kwanza wa corona ambae ni Mbunge, na cha kujiuliza hapa ni je, hajaambukiza wabunge wengine?

Tujiulize: Iwapo ushauri wa Zitto ungezingatiwa, haya yangetokea?

Endeleeni tu kujifanya mmeweka pamba masikoni ila mkitafutacho mtakipata.
 
Wabunge Wameruhusiwa kwenda nyumbani badala ya kuwekwa kizuizini hii ni hatari zaidi
Hii kama ni kweli basi hili janga likipita washitakiwa kwa kuwa careless na kutokujali jamii inayowazunguka..., ni mfano gani watakuwa wanaonyesha wajifungie tu wote waendelekee kutumikia wananchi usiku na machana after all Hapa Kazi Tu...
 
Ugonjwa ni siri ya mgonjwa mpaka pale anapoamua kuiweka wazi mwenyewe kwa faida ya wengine.

Je, kwa Kiongozi kuijiweka wazi kwa Manufaa ya Jamii yake ili Kuongeza Umakini Kwao ( Wananchi ) siyo Jambo jema Kimantiki?
 
Ndio wangeweza kuupata sehemu yoyote tofauti na bungeni, wabunge chapeni kazi covid 19 ni vijimafua tu
 
Bia yetu usiseme corona ni ugaonjwa wa kawaida. Huoni ugonjwa huu unafanya watu wanaacha ofisi na kwenda mafichoni? corona si ya mchezo mchezo!
Wapo Wanakunywa chai kwenye mapango ya mawe wanachapa kazi
 
Maajabu ni kwamba, huyo mbunge wamemgundua kuwa na Corona huko Dodoma siku tano zilizopita lakini mpaka leo hii waziri wa Afya hajatuambia kama Dodoma kuna Corona tayari.

Sijui tunafichwa nini?
Na tutafichwa mpaka lini?
 
Salary Slip,
Acha kuleta hoja za kitoto, ameugua waziri mkuu wa Uingereza na shughuli za serikali zinaendelea. Kapata maambukizi mbunge mmoja unataka kutia watu hofu. Na naibu spika anasema anaendelea vizuri. Alitaka lisogezwe mbele ili uchaguzi nao usogezwe mbele?
 
Kwani hao wabunge siyo watanzania? Kama watanzania wanaendelea na kazi kama kawaida hata wabunge waendelee na kazi. Bila kusahau kumkumbusha rais arudi ikulu Dar aendelee kuchapa kazi kama anavyotuhubiria kila siku.
 
Back
Top Bottom