Naibu Waziri Abdallah Sagini: Mto Mara hauna sumu, endeleeni kutumia maji

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mbunge wa Jimbo la Butiama (MB), Jumanne Abdallah Sagini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amewataka wananchi wa jimbo lake la Butiama kuondoa hofu kuhusu Mto Mara uliokuwa unasadikika kuwa na sumu.

Akizungumza na Wananchi wa jimbo lake la Butiama aliwaomba kuamini taarifa iliyotolewa na Kamati Maalumu ya Kitaifa iliyoundwa na Serikali kuchunguza mabadiliko ya maji ndani ya Mto Mara iliyotoa taarifa kwamba chanzo cha mabadiliko katika mto huo ni shuguli za binadamu pamoja na nguvu za asili.

"Jambo hili Serikali imetuondolea hofu tuamini kwamba tuko salama, Nasisitiza hakuna serikali duniani inapanga kuua raia wake, tahadhari zote zilizotolewa ilikuwa ni kujiridhisha na tuhuma hizo. Mto Mara upo salama mnaweza kuendelea kutumia," alisema.

Mbunge Sagini aliyasema hayo wakati wa mikutano na wananchi wa Kijji cha Wegero, Kijiji cha Buswahili, Kijiji cha Kirumi, Kijiji cha Kitasakwa na Kijiji cha Kwisero vilivyopo katika Wilaya ya Butiama baada ya kutembelea sehemu za mto huo Serikali zilizoathiriwa kwenye jimbo lake la Butiama ikiwa ni moja ya ziara yake Mkoani Mara.

Aidha, aliwauliza wananchi hao kama kuna madhara makubwa yaliyotokea kwa mifugo yao baada ya kutumia maji ya mto huo na kuwaeleza kuwa kama mto huo ulikuwa una sumu basi ni lazima mifugo ingedhurika.

Jumanne Abdallah Sagini.jpg
Chanzo: Majira
 
Mto Mara una kinyesi

Mto Mara una sumu

Mto Mara una kemikali hatarishi

Mto Mara una mamba

Mto Mara una majini na machinist

Mto Mara umesingiziwa mambo mengi sana
 
Mbunge wa Jimbo la Butiama (MB), Jumanne Abdallah Sagini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amewataka wananchi wa jimbo lake la Butiama kuondoa hofu kuhusu Mto Mara uliokuwa unasadikika kuwa na sumu.
Arabuni baada ya statement kama hiii tu kutolewa - huyu jamaa anatoswa mtoni afu ananyweshwa maji hayo hayo kwa nguvu.
 
Ushauri wangu wa bure Tafuteni taasisi yeyote ile nje ya nchi , Iangalie hayo maji.

La sivyo mtakufa kama samaki .

Kama sio leo ni keshokutwa, ndio tabia za kemikali zilivyo
 
Back
Top Bottom