Naibu Waziri Adamu Malima aibiwa kila kitu hotelini Morogoro!

Naibu Waziri Adamu Malima aibiwa kila kitu hotelini Morogoro!

Eti Tanzania kisiwa cha amani huku kiunoni amepachika bastola na kwenye begi kuna AK-47.

Hii ni dalili ya wazi kwamba viongozi wetu hawana jambo lolote la maana wanalowatendea wananchi hadi kujihisi hawako salama, na matokeo yake wanaamua kutembea wakiwa wamejihami kijeshi. Nakumbuka waziri Majogo aliwahi kukamatwa nchini India akiwa na AK-47. Huu unaweza kuwa ni uthibitisho kwamba mawaziri na manaibu waziri wote wanatembea wakiwa wamejihami kijeshi!!:whoo:

AK 47? kalashinikov? A Russian machine designed for liberation????? where and why do you need it in Tanzania????
 
huyu ni mtanzania au mtalii $4000 za nini ndani ya nchi tena iringa,morogoro?ndio maana hawajali matatizo yetu
 
Hivi huyu si ndiye yule aliyeripotia na gazeti la MWANAHALISI kuwa alisafiri kwenda Afruka Kusini kwa kutumuia jina bandia.Tafakari huyu mheshimiwa ni mtu wa aina gani
 
Si hoteli ipo Boma rd. Shamba la magereza na Boma rd vipi?

Hotel inaitwa Nashela imejengwa yalipo kuwa mashamba ya magereza, pembeni yake ndo ipo boma road..Hotel hiyo inasemekana ni Waziri Mkuu mstaafu.
 
Akirudi Bungeni apiganie serikali iweke sheria kali ya matumizi au na ugawaji wa dawa za Phychiatric. Imekuwa ni mchezo tu kuzipata hasa Tanzania. Nchi zingine ukikutwa nazo bila idhini ya daktari ni kosa kubwa sana yaani la mauaji. Naona tunashabikia kwa Malima kupewa hiyo. Doctors may help on this, haswa Phychiatrist au anesthetic.
 
Si hoteli ipo Boma rd. Shamba la magereza na Boma rd vipi?

Hotel inaitwa Nashela imejengwa yalipo kuwa mashamba ya magereza, pembeni yake ndo ipo boma road..Hotel hiyo inasemekana ni mmoja ya Waziri Mkuu mstaafu.
 
Ile hoteli ukikaa ndani ukifunga mlango hauwezi mtu kufungua kwa nje. Ila outlet za kutokea nje si kwa reception tu ila zipo zingine kwa pembeni. Siku moja asubuhi nilitoka na bag yangu kwa pembeni nikaingiza kwenye gari. Hakuna aliyeniona wala aliyeniuliza. Kama ningetaka kukimbia kulipa bill ningesepa tu. Nikaenda reception nikakuta mtu yupo ila kwenye chumba cha ndani. Pale ni rahisi tu mtu kutoka na bag hizo bila mtu kuona sembuse kuhonga mlinzi tu. Ila kila floor na corridor kuna security cameras. Labda nao walikua wamelala!
 
Vipi zile pete zake wamechukuwa pia, Malima, wewe unajua kabisa hali ngumu ya Watanzania halafu unalala na mpiganaji huku umejiachia unategemea nini?

Tena shukuru Mungu angekuwekea kete kwenye nyonyo saizi ingekuwa habari ingine, pole sana Mkuu.
 
Kwasisi tulioko Arusha tumeshawazoea hawa wakubwa wakiibiwa na malaya ila sioni kama swala la kuoa kama breaking news. Kwa redio One kuifanya breaking news ni kama kulipiza kisasi maana Malima huwa ana bifu na Mengi na ndiye aliyepeleka malalamiko bungeni kuwa Itv na redio one zinatumia mda mwingi kwenye taarifa ya habari kuhusu Mengi kuliko mkuu wa nchi.
 
Meneja wa hoteli asimame kidete kama mwanzoni kutetea hadhi ya hoteli yake. Ni kweli anatoza 400,000/= kwa siku halafu usiwepo ulinzi hadi mtu anachomoka na mizigo ya kutosha? Ina maana hoteli itakubali kuchafuliwa kwa gharama za hadhi ya Mh Naibu? Nilisema sitachangia thread hii kwa kuogopa kutembelewa, lakini uzalendo umenishinda, kwani hata kule Dar hotel kama Blue Pearl ya pale Ubungo Plaza unaweza ukapata chumba cha bei kama hiyo na nadhani mnajua jinsi ulinzi wa pale ulivyo wa hali ya juu. Sasa mtu akisema ameibiwa mzigo mkubwa katika hoteli yenye kutoza sh. 400,000/= kwa siku, haiingii akilini!
 
Hotel inaitwa Nashela imejengwa yalipo kuwa mashamba ya magereza, pembeni yake ndo ipo boma road..Hotel hiyo inasemekana ni mmoja ya Waziri Mkuu mstaafu.

Samba la Magereza Vs Nashera.
Tanzania kila kitu kinawezekana.
 
Sasa hivi ukimwuliza maana ya CHEO NI DHAMANA - Atakujibu kwa ufasaha sana.
 
Back
Top Bottom