Kwamba alijipumzisha sebuleni akiangalia taarifa ya habari?! Kwamba akaibiwa simu alizoacha chumbani?! Kwamba kwa nafasi yake ni mtu wa kuacha mbali simu zake?! Kwamba tayari alishavua pete?! Kwamba wezi walijua amepitiwa na usingizi sebuleni na hajalala chumbani?! Ooooooopsss.:thinking:
na pete zilivutwa na smaku zikatoka vidoleni
"Kuna Waziri mmoja huko Uingereza alionekana akipitapita mitaani na akina mama, basi habari zikaenea na huyo waziri akaamua kujiuzulu. Alimwandikia Waziri Mkuu barua ya kuomba kujiuzulu, kwa jinsi Waziri Mkuu alivyokasirika hakumjibu alimteua mtu mwingine kuchuakua mafasi yake." Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (1995): Akiongelea uadilifu wa Viongozi wetu.
Sijui Rais atakasirika kiasi gani.
Pia nimemsikiliza Meneja wa Hoteli hiyo ameeleza vizuri na kukiri kwamba kuna udhaifu katika mfumo wao wa ulinzi(ulinzi wa binadamu na ule wa kitaalamu i.e CCTV n.k......) na ameahidi kulirekebisha suala hilo(nadhani ni kwa ajii ya kuwaondoa hofu wateja wao.....
Raha imegeuka kuwa karaha! pole sana mzinzi mwenzangu!
Ningekuwa Adam nikichukua mrembo nahamishia kitanda mlangoni. hakuna mtu kutoka.
Ni pesa za kujikimu sioni kama zina wingi wa kuleta tafrani.
Nyie hamjawahi kuibiwa? Hujasikia wachezaji wa timu ya Brazil wameibiwa Hotelini kwenye World cup pamoja na ulinzi wote?
Ni pesa za kujikimu sioni kama zina wingi wa kuleta tafrani.
Owky so hakuwa na mwanamke................So aishtaki Hotel kwa kutokuwa na ulinzi wa kutosha hasa kwa mtu kama yeye achilia mbali wateja wa kawaida. Akitaka tumuamini kuwa alikuwa clean na kweli vimeibiwa akiwa chumbani, awafungulie kesi ya madai hao wamiliki wa hiyo hotel.
Bila hivyo, Malima ulikuwa na mwanamke, na alokuliza ni mwanamke!
Kweli kabisa mate.....
Hata hivyo inaonekana wengi humu wamechangia na kumhukumu Naibu Waziri kwamba alilala na mwanamke/Changudoa bila kuelewa kiini hasa cha wizi huo....Wengi wameandika kwa kusukumwa na mawazo yao na si kwa facts/hali halisi ilivyokuwa...
Nimeangalia taarifa za habari za ITV na TBC1 inaonekana Mheshimiwa Adam alipitiwa na usingizi na baada ya kushtuka alikuta dirisha lipo wazi na baadae kugundua ameibiwa vitu vingi zikiwemo pesa,mabegi yenye nyaraka, laptop na vitu vingine ambavyo vina thamani ya karibu milioni 20.....
Kwa mujibu wa picha za Video za ITV na TBC1 inaonekana hao jamaa walibetua reli za dirisha hili na kuzama chumbani kupitia dirishani......Polisi wamesema kwamba baadhi ya vitu vilivyoibwa tayari vimepatikana na wanaendelea na msako wa wahusika wa wizi huo....Pia walinzi watatu wa Hoteli hiyo wamekamatwa.....
Pia nimemsikiliza Meneja wa Hoteli hiyo ameeleza vizuri na kukiri kwamba kuna udhaifu katika mfumo wao wa ulinzi(ulinzi wa binadamu na ule wa kitaalamu i.e CCTV n.k......) na ameahidi kulirekebisha suala hilo(nadhani ni kwa ajii ya kuwaondoa hofu wateja wao.....
Kwa ujumla mkasa huu uliompata Adam unaweza kumpata mtu yoyote yule bila hata kuwa na mwanamke/changudoa kama wadau wanavyomtuhumu na kumdhihaki Adam.....Hotel nyingi nchini zina udhaifu mkubwa kaika suala la ulinzi.....Nyingine pamoja na ukubwa wake hazina mfumo wa ulinzi wa CCTV hivyo kuwa ni vigumu kufuatilia mwenendo mzima wa ulinzi katika hoteli hizo na hata kama zina CCTV hakuna ufuatiliaji wa masaa 24 kama inavyotakiwa badala yake wamekuwa wakiziachaa tu na kuzitumia kwa upelelezi/ushahidi mara tukio linapotokea kitu ambacho ni hatari kwani lengo la mfumo wa ulinzi wa CCTV ni kugundua uhalifu na kuzuia usitoke......
Nampa pole sana Adam....Nadhani hili litakuwa ni fundisho kwa waheshimiwa wengine pamoja wamiliki wa Hoteli....
Mkuu niko Hotelini hapa na kuna haka kakipeperushi kananikera kanasema hivi: You are urged to deposit your valuable items such as money, computer, camera, fire arms, etc to the receptionist and a receipt will be issued. The hotel shall not be held responsible for any loss caused by violation of this regulation!!
Sijui kama hiyo hotel nayo ilikuwa na haka katangazo. Kananikera kweli.
.....hoteli za mashenzini taabu tupu, haya sasa, reputation ya hiyo 'guest hse' itabakia na tag pale alipoibiwa mheshimiwa waziri....
I dont buy other cheap stories ati alikuwa na kimada, arrgghh!
Mazingira yale yanaashiria kweli mzee mzima pengine alikua chumba kingine akitenda "dhambi". Na katika uwanja huo shetani ni bingwa wa kuumbua! Haiingii akilini mwa mtu yeyote kibaka aingie, achukue pete, achukue hela mpaka na mabegi yeye kalala!atakuwa alikuwa nakiburudisho cha chap chap hehehe na bado tutagawana sana vya kwenu
Koma kabisa.......
Hii inaweza kumkuta mwanaume malaya tu!!!
Hivi hizi habari za kwamba jamaa aliibiwa hadi nguo zote hawa radio one walizipata wapi? Nimemsikia Malima akielezea kwamba hajaibiwa nguo zote.
Halafu hii forum siyo vijiwe vya umbea umbea, hii habari ya kwamba alikua na mwanamke nayo imetoka wapi? Hivi kweli tuendelee kujiita great thinkers wakati tunakaa hapa jukwaani kujadili umbea unaoletwa na mjinga mmoja?.
Hii ni aibu kwa jukwaa zima.