Naibu Waziri Adamu Malima aibiwa kila kitu hotelini Morogoro!

Naibu Waziri Adamu Malima aibiwa kila kitu hotelini Morogoro!

Bwana ametoa mabinti wametwaaaa jina la adamu lisimuliwe
loh!!!!!!!


Hapa nimetoka kapa.. Bwana ni JK au Malima Sr.?
 
Hilo nalo swali. Yaani waingie watoke na mabegi matatu bila kuwa noticed. Inaweza ikawa ina mcover mheshimiwa lakini ikawa very detremental kwenye business ya hiyo hotel. Kama hotel ya gharama kama hiyo inaweza kuingilika kirahisi hivyo basi hiyo hotel haifai kuwa na gharama hiyo. Hii haitakuwa na tofauti na guest ya uchochoroni!
Maelezo ya meneja wa hoteli mbele ya waandishi wa habari yamepindishwa kujaribu kumuokoa mzinzi yule, lakini yamechelewa! Wenye hoteli hawako tayari kuharibu biashara kumtetea mzinzi! Never on earth!
 
hii ndio moro mji kasoro bahari totoz za hapa zinaufundi wa hali ya juu
dito alipewa dozi yanguvu akashindwa kuimili mauti yakamkuta, sasa huyu dogo
anaona mazoezi yamemsaidia dozi aliyo pata alizimia tu watu wakakomba mzigo.
Tunawasubiri mawaziri wengi waje wapate dozi

naambiwa aliona mabinti wanamekuja na pombe y kienyeji kwenye chupa ya uhai wakaomba aonje
huku amemwaga kwenye glass jack daniel loh ikawa jack malima
teeheeeteeehhhhhh wacha bana muulizeni mama rwakatare ile pombe yetu inaitwaje na heshima gani sio kipata ama kitochi ...ashazoea kuomba kuria mbege kili akajua iko the same loh ..ashukuru awakumshikakunani maana kuna wengine wakiona umelewa unakuta asbh suruali imelowa harufu
loh..ila mlichofanyamadada nyie amtosahaulika na familia ya malima kwa kweli kama si wana ......
 
Wana JF niambieni kuna nini special kuhusu Adam Malima? Maana mada imeanza sa 7.13 na kufika saa hizi ni saa 4 .11 za usiku lakini kuna wchangiaji 481. Yaani posts 50 kwa saa au kwa kila dakika moja na sekunde 15 inayokwenda kuna mtu anapost. Je Adam ni kichwa kiasi hicho au ana maadui wengi? Naomba jibu

Stuxnet, hivi ni kweli huoni what is special kwa huyu waziri, in this case?
 
Nadhani unahisa au unataka tu kumtetea, katika kurasa za awali kabisa mhudumu ameeleza aliingia na mwanamke mweupe akitokea club usiku wa manane. Unataka wasemeje? Aisee jamaa alichemsha Mademu wa Moro wajanja kwa sana. Pole yake anasitahiri kujiuzulu ili kulinda heshima ya nchi na yule kamteua. Hotel haiko na shida maana hakuna kuvunjwa kwa hotel ni problem ya mteja kwenda na changu eti! Kwa nafasi yake alitakiwa kuwa na mtu anayemjua vizuri na si vinginevyo?

Usiongee bila kuwa na data, tutaonekana kama Wazushi. Mimi sikubaliani na uchafu wowote , lakini nina tatizo na ukweli wa hilo tukio.
Polisi wamasema dirisha lilivunjwa na meneja wa Hoteli alikubaliana na maelezo hayo. Wewe ni nani hata upingane na taarifa ya kitaalamu iliyothibitishwa na meneja?
Sina hisa na mtu mkuu, bali sipendi uzushi.
 
Nimeconfirm na kijana mmoja kwenye hiyo hotel ni kweli alilala hapo tangu juzi kwenye chumba cha exctv suite sh 400000 kwa siku tangu jana alirudi usiku kutoka club na dada mweupe mrefu na asbh kaamka kajikuta hana hata chupi katoka na taulo kiunoni!!hawa dada zetu wa club cjui vp amemkomba kila kitu waziri ni aibu Mkuu wa mkoa alienda kuokoa jahazi

kama kulala tu anatumia laki nne kwa siku?,je matumizi mengine inaweza kuwa milioni moja anatumia kwa siku?.na kama ndyo hivyo yeye anaingiza sh ngapi kwa siku?,na kwa hizo pesa kwa mwaka anatumia sh ngapi?,je matumizi yake na mapato yake vinaendana?.kupitia yeye serikali inapata sh ngapi ?au anazalisha sh ngapi? ili awe na uhalali wa kutumia hicho kiwango kwa siku.Je watanzania wanafaidikaje na uwepo wake katika utumishi wa umma?.Au watanzania tunaumia kiasi gani tukiwa na viongozi kama huyu? NISAIDIENI MAJIBU JAMANI
 
Wana JF niambieni kuna nini special kuhusu Adam Malima? Maana mada imeanza sa 7.13 na kufika saa hizi ni saa 4 .11 za usiku lakini kuna wchangiaji 481. Yaani posts 50 kwa saa au kwa kila dakika moja na sekunde 15 inayokwenda kuna mtu anapost. Je Adam ni kichwa kiasi hicho au ana maadui wengi? Naomba jibu

Ishu siyo Malima. Ishu ni kwamba thread imegusa mahala pake! Ukizingatia kwamba mwanamke akipewa nafasi Anaweza!
 
Kutokuwa mwaminifu katika familia siyo sehemu ya maadili ya viongozi wa Taifa la Tanzania? Mbona nchi kama Ujerman au Italy tukio kama hili linampotezea mtu sifa za kuwa kiongozi?
Nchi hii imeendelea sana kiasi utamaduni wa kuwajibika kwa skendo ni ishu iliyopitwa mno na wakati! Ndo maana unaona hata akina Mponda wanapeta!
 
Wana JF niambieni kuna nini special kuhusu Adam Malima? Maana mada imeanza sa 7.13 na kufika saa hizi ni saa 4 .11 za usiku lakini kuna wchangiaji 481... Je Adam ana maadui wengi kiasi hicho? Naomba jibu

Muulize yeye iweje atembee na AK 47 na bastola, kama hana maadui wengi kihivyo! Uliona wapi AK 47 inalinda dola 4,000 $ tu?
 
Alilala hoteli ya laki 4 kwa siku??????
Si ajabu mama watoto hakumwachia hata hela ya "mchicha", kwa kisingizio cha hali ngumu.
Nampongeza huyo dada aliyejihudumia hizo hela zisizo na kazi;
utalalaje hoteli ya laki 4 Moro kwa kutumia kodi za mlala hoi ambaye hajui kesho atakula nini?
Siku tatu tu malazi 1.2m. Afu eti bi kiroboto Makinda anadai hali ngumu wabunge wengi wako mbioni kuacha kazi. Thubutu! Hizo hela za kutanua nazo bila kutolea jasho watazitoa wapi?
 
hakuna siku ambayo magazeti ya udaku yanafurahia hiii thread maana jumatatu ndiyo habari kuu.
 
Kweli kabisa mate.....

Hata hivyo inaonekana wengi humu wamechangia na kumhukumu Naibu Waziri kwamba alilala na mwanamke/Changudoa bila kuelewa kiini hasa cha wizi huo....Wengi wameandika kwa kusukumwa na mawazo yao na si kwa facts/hali halisi ilivyokuwa...

Nimeangalia taarifa za habari za ITV na TBC1 inaonekana Mheshimiwa Adam alipitiwa na usingizi na baada ya kushtuka alikuta dirisha lipo wazi na baadae kugundua ameibiwa vitu vingi zikiwemo pesa,mabegi yenye nyaraka, laptop na vitu vingine ambavyo vina thamani ya karibu milioni 20.....

Kwa mujibu wa picha za Video za ITV na TBC1 inaonekana hao jamaa walibetua reli za dirisha hili na kuzama chumbani kupitia dirishani......Polisi wamesema kwamba baadhi ya vitu vilivyoibwa tayari vimepatikana na wanaendelea na msako wa wahusika wa wizi huo....Pia walinzi watatu wa Hoteli hiyo wamekamatwa.....

Pia nimemsikiliza Meneja wa Hoteli hiyo ameeleza vizuri na kukiri kwamba kuna udhaifu katika mfumo wao wa ulinzi(ulinzi wa binadamu na ule wa kitaalamu i.e CCTV n.k......) na ameahidi kulirekebisha suala hilo(nadhani ni kwa ajii ya kuwaondoa hofu wateja wao.....

Kwa ujumla mkasa huu uliompata Adam unaweza kumpata mtu yoyote yule bila hata kuwa na mwanamke/changudoa kama wadau wanavyomtuhumu na kumdhihaki Adam.....Hotel nyingi nchini zina udhaifu mkubwa kaika suala la ulinzi.....Nyingine pamoja na ukubwa wake hazina mfumo wa ulinzi wa CCTV hivyo kuwa ni vigumu kufuatilia mwenendo mzima wa ulinzi katika hoteli hizo na hata kama zina CCTV hakuna ufuatiliaji wa masaa 24 kama inavyotakiwa badala yake wamekuwa wakiziachaa tu na kuzitumia kwa upelelezi/ushahidi mara tukio linapotokea kitu ambacho ni hatari kwani lengo la mfumo wa ulinzi wa CCTV ni kugundua uhalifu na kuzuia usitoke......

Nampa pole sana Adam....Nadhani hili litakuwa ni fundisho kwa waheshimiwa wengine pamoja wamiliki wa Hoteli....


mkuu si afadhali ameibiwa? angekuwa ameuliwa au kunyeshwa sumu tungesemaje??

mpaka ulinzi anaotembelea Kikwete sisi tuliozoea CSI scenes nyingi unaona kabisa unampata pale, unammaliza hapa

nenda mabenki yetu hakuna ulinzi kabisa

as life getting tougher watch out! usiamini kila kitu mpaka chupi yako mwenyewe!
 
Binafsi huwa nafurahi na kusherehekea wanapoibiwa wakubwa kwani mfumo unaowaibua wezi na majambazi umejengwa na hao hao wakubwa. Hongereni wezi kwa kumwonjesha machungu ya kuibiwa. Ni matumaini yangu kuwa mtaendelea na tabia hiyo kwa wakubwa wengine. Mbarikiwe sana.
 
Webby.
Tatizo kujiaminisha unataja sana vyeo vyako unamuonyesha mtoto picha kwenye Laptop yako upo na kina Pinda, JK.

Mtoto anazubaa tu anakushangaa, wewe unajiona mjanja ukizingatia umeifanya unyama Dar es Saalam, Protea Hotel, Kempiski Hotel

Unaona Morogoro hakuna wajanja, ukija kustuka mtoto kakuacha.

Ritz nasemaje haya mambo ya kawaida kabisa!! tena jamaa ashukuru ni waziri hivyo serikali itagharamia kila kitu pale

kuna story nyingi mno za wenzangu wahandisi wa ujenzi, ,migodi, masurveyor, ma geologist

kuna mahali unabanwa, unaingia na mtoto chumbani unaona kabisa itakuwa short time..mara una extend muda na huku ukilia na

kujuta kwa nini umeoa yule wakati raha ziko huku

kutahamaki huna michoro, simu, laptop na tender documents!!! achilia mbali theodolite na GPS!

kuna wanawake balaa acha kabisa

humu wengi wanasema kwa zile mila za kinafiki za ki-afrika as if they are 100% innocent kumbe ni vice versa kwa sababu ni Malima!

Huyu malima kama alikuwa na kamchezo haka tangu kabla hajawa waziri kuna mechanism gani au nguvu gani ya kuwa ukiwa waziri unaacha haka kamchezo?? kama sio kuwa ukiwa waziri ndio kanaongezeka

kwanza anatabia nzuri kwa dollar 4000? unakuwa na watatu unawachukua sehemu mbali mbali...mbona mshikaji yuko normal tu!! mmoja tu!

pole dume la mbegu
 
  • Thanks
Reactions: ral
Kutokuwa mwaminifu katika familia siyo sehemu ya maadili ya viongozi wa Taifa la Tanzania? Mbona nchi kama Ujerman au Italy tukio kama hili linampotezea mtu sifa za kuwa kiongozi?

sasa huko si ni Ujerumani na Italy??

mbona na sense kama unakataa asili yako??
 
[TABLE="class: tr-caption-container, width: 1"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Adam Kighoma Malima[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adamu Kighoma Malima amekombwa vitu vyake vyote vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 15 katika hoteli ya kitalii ya Nashera ya mjini Morogoro.


Taarifa za kipolisi zilizopatikana kutoka mjini Morogoro zimethibitisha kutokea wizi huo zikisema ulitokea usiku wa kuamkia leo.


Zilimkariri Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro, Hamis Seleman taarifa zilmesema wizi umetokea wakati waziri huyo alipokuwa amejipumzisha kwenye sebule ya chumba chake kwenye hoteli hiyo hadi mida ya 10.45 ndipo alibaini kuibiwa vitu hivyo baada ya kurudi chumbani.


Kwa mujibu wa polisi zimeibwa fedha taslimu Dola 4000 za Marekani na Sh. milioni 1.5, pete mbili za silva zenye thamani ya sh. milioni 2, simu zenye thamani ya sh. milioni 1.3, balaghashia yenye thamani ya sh. 50,000, laptop mbili zenye thamani ya sh. milioni 5.6, taperecorder na headphone vyote vya sh. milioni moja.


Polisi wanasema dirisha la aluminium la chumba cha hoteli alimokuwa Malima limekutwa limevunjwa kwa kitu kigumu.


Habari zinasema nje ya dirisha hilo zimeoneka nyayo nje na ndani ya chumba jambo linaloashiria kuwa ni za mwizi.


Kufuatia wizi huo, walinzi watatu wa hotel hiyo wanashikiliwa na polisi huku taarufa zilizopatikana baadaye tukiandaa kurusha ripoti hii zikisema kwamba baadhi ya vitu vilivyoibwa vimepatikana, ingawa havikutajwa.


Posted by: ByBBashir Nkoromo
 
Hivi kweli Waziri Mzima Safari ya Morogoro unahitaji kuwa na Dola 4,000 mfukoni, ni za nini?

Yaani Mawaziri wa Awamu ya Nne ni Matajiri haswa...
 
Back
Top Bottom