Naibu Waziri Adamu Malima aibiwa kila kitu hotelini Morogoro!

Naibu Waziri Adamu Malima aibiwa kila kitu hotelini Morogoro!

babu unabishi wakati yeye mwenyewe kaongea na waandishi?!!!!!...salimie bibi

Sorry Mkuu,

Siyo kwamba nabisha ila siwezi kuamini,

Hata hivyo nimemskia akiongea kweney TBC1 kwenye taarifa ya habari na inaonekana kuna mengi yamezunguka tukio hilo...Anaonekana kabisa kuwa ana jambo analolificha na wakati huo Meneja anaongea with a smile ...tena karibia aseme kuwa hili jambo ni la kawaida!!

Hivi per diem allowance ya Waziri ni shilling ngapi?

Mie najue the highest rate ya serikali ni 80,000.00. Hizo laki 4 analipiwa na nani?

Babu DC!!:thinking::thinking::crazy::crazy:
 
Nakumbuka wakati vibaka wa kupora saa pale Kinondoni kona ya Namanga walipompora Salim Ahmed Salim saa yake, wakati huo SAS ni waziri wa ulinzi. Baada ya saa moja walitandaa wanajeshi mitaa yote ya Kinondoni na Msasani, mwizi akapatikana within 2 hours, na Rado ya Mzee ikarudishwa salama salmini.
 
Nimemsikai Akisema "Vijipesa" hivi shilingi laki ngapi alizoibiwa
 
TAARIFA YA JESHI LA POLISI NI HII:
NAIBU waziri wa nishati na madini Adamu Kigoma Malima ameibiwa vitu vyake vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 katika hotel ya kitalii ya Nashera ya mjini Morogoro ambapo alikuwa amefikia kwa siku tatu.
Kwa mujibu wa mkuu wa upelelezi na makosa ya jinai mkoani hapa Hamis Seleman alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10.45 alfajiri katika hotel hiyo na kwamab uchunguzi wa awali ulibaini kuwa waziri huyo alikuwa amejipumzisha katika sebule ya chumba hicho na kwamba ndipo alibaini kuibiwa vitu hivyo baada ya kurudi chumbani kwake na kutoa taarifa kwa uongozi wa hotel hiyo.
Vitu vilivyoibiwa kuwa ni pamoja na Dola 4000 za Marekani, fedha taslimu shilingi milioni 1.5, pete za silva 2 zenye thamani ya shilingi milioni 2, simu zenye thamani ya shilingi milioni 1.3, balaghashia yenye thamani ya shilingi 50,000, laptop 2 zenye thamani ya shilingi milioni 5.6, taperecorder na headphone milioni 1.
Mazingira ya wizi huo ni kuwa dirisha la chumba hicho ambalo ni la Alminium limevunjwa na kitu cha chuma na hivyo kusababisha mwizi huyo kuingia ndani na kuiba.Alisema kuwa nje ya dirisha hilo zimeoneka nyayo za mwizi pamoja na ndani ya chumba hicho jambo lililoashiria mwizi huyo kuingia hadi ndani hakuna mtu aliyekamatwa.
Akizungumza na waandishi wa habari hotelini hapo na kuthibitisha kuibiwa vitu hivyo Malima alisema kwamba kinachomuuzunisha ni pete yake ya urithi aliopewa na marehemu baba yake pamoja na moja aliopewa na mkewe.
Alisema alikuwa katika ziara ya siku tatu mkoani Morogoro kwajili ya kukagua miradi ya madini na kwamba baada ya kurudi alikaa katika sebule ya hotel hiyo akiangalia taarifa ya habari na kupitiwa na usingizi na kusinzia ambapo alipostuka 10.45 ndipo aligundua kuibiwa vitu hivyo.
Alisema kuwa bunduki na bastola yake havikuibiwa ingwa vitambulisho, pasipoti pamoja na kadi za benk pamoja na dokumenti zake za ofisi zimeibiwa.

Source: Katunews

Pete zilikuwa kwenye begi? au alivuliwa mikononi?
 
Kina boss wangu mmoja mr Msukuma si jina halisi. Alisa kupewa hela za mradi Kama milioni 4 katoka dar mradi upo moto Mikumi. Jamaa katoka dar kafika Moro aka brake kwa siku nzima, Kama kawa Ana kachangu kake kakialika kakipiga msosi na unywaji Wa hapa na pale.
Kwenda kulala nae si mambo ya majigambo ya kaanza mara afungue briefcase na kuchukua taulo aka oge, LENGO NI KUONYESHA KWAMBA AMEKUJA NJEMA. Demu nae kapanga kivyake kaona hela kaamua ndio wakati Wa KUTOKA. Alikwiba hela zote more than 4m. Boss wangu Ana stuka demu hayupo pesa hakuna. Twaenda kumstua boss tuondoke hataki kumbe kashaibiwa. Kwa ufupi tuli mchukua rafiki ya demu Yule kwa ahadi ya laki. Katupeleka nyumbani twakuta demu ndio Ana gawa Mali za boss wetu. Mashati suruali na pesa na yuko mbioni kusafiri. TILIFANIKIWA KUKOMBOA SH MILLION 3500000 na kukomboa ajira ya boss wetu maana Kama sivyo pingu ilikuwa tayari kwa ajili yake.
USIOMBE YA KUKUTE
 
Hivi pete zinakaa wapi? Kwenye kidole ama begi? Hata kama utasema ulizivua wakati wa kulala bado kuna mashaka maana kwa mujibu wa maelezo ya polisi vitu vimeibiwa saa nne na nusu.
Polisi wetu wetu wanaingizwa mkenge kila siku kuzungumza yasioingia akilini.
.
 
ulinzi hafifu jamani

tuwe wakweli wangapi huwa wanafanya hizi inshu??

mlinzi huwa hatakiwi kumruhusu dada kutoka mpaka aliyeingia naye a-confirm, kwetu busia, iko hivyo
Kweli kabisa mate.....

Hata hivyo inaonekana wengi humu wamechangia na kumhukumu Naibu Waziri kwamba alilala na mwanamke/Changudoa bila kuelewa kiini hasa cha wizi huo....Wengi wameandika kwa kusukumwa na mawazo yao na si kwa facts/hali halisi ilivyokuwa...

Nimeangalia taarifa za habari za ITV na TBC1 inaonekana Mheshimiwa Adam alipitiwa na usingizi na baada ya kushtuka alikuta dirisha lipo wazi na baadae kugundua ameibiwa vitu vingi zikiwemo pesa,mabegi yenye nyaraka, laptop na vitu vingine ambavyo vina thamani ya karibu milioni 20.....

Kwa mujibu wa picha za Video za ITV na TBC1 inaonekana hao jamaa walibetua reli za dirisha hili na kuzama chumbani kupitia dirishani......Polisi wamesema kwamba baadhi ya vitu vilivyoibwa tayari vimepatikana na wanaendelea na msako wa wahusika wa wizi huo....Pia walinzi watatu wa Hoteli hiyo wamekamatwa.....

Pia nimemsikiliza Meneja wa Hoteli hiyo ameeleza vizuri na kukiri kwamba kuna udhaifu katika mfumo wao wa ulinzi(ulinzi wa binadamu na ule wa kitaalamu i.e CCTV n.k......) na ameahidi kulirekebisha suala hilo(nadhani ni kwa ajii ya kuwaondoa hofu wateja wao.....

Kwa ujumla mkasa huu uliompata Adam unaweza kumpata mtu yoyote yule bila hata kuwa na mwanamke/changudoa kama wadau wanavyomtuhumu na kumdhihaki Adam.....Hotel nyingi nchini zina udhaifu mkubwa kaika suala la ulinzi.....Nyingine pamoja na ukubwa wake hazina mfumo wa ulinzi wa CCTV hivyo kuwa ni vigumu kufuatilia mwenendo mzima wa ulinzi katika hoteli hizo na hata kama zina CCTV hakuna ufuatiliaji wa masaa 24 kama inavyotakiwa badala yake wamekuwa wakiziachaa tu na kuzitumia kwa upelelezi/ushahidi mara tukio linapotokea kitu ambacho ni hatari kwani lengo la mfumo wa ulinzi wa CCTV ni kugundua uhalifu na kuzuia usitoke......

Nampa pole sana Adam....Nadhani hili litakuwa ni fundisho kwa waheshimiwa wengine pamoja wamiliki wa Hoteli....
 
ulinzi hafifu jamani

tuwe wakweli wangapi huwa wanafanya hizi inshu??

mlinzi huwa hatakiwi kumruhusu dada kutoka mpaka aliyeingia naye a-confirm, kwetu busia, iko hivyo

Webby.
Tatizo kujiaminisha unataja sana vyeo vyako unamuonyesha mtoto picha kwenye Laptop yako upo na kina Pinda, JK.

Mtoto anazubaa tu anakushangaa, wewe unajiona mjanja ukizingatia umeifanya unyama Dar es Saalam, Protea Hotel, Kempiski Hotel

Unaona Morogoro hakuna wajanja, ukija kustuka mtoto kakuacha.
 
Kajichomea zaidi anaposema watakuwa "vibaka tu..dah vibaka gani wanapenya hoteli kubwa kama ile..
 
dada poa uyo ni soooo............naibu kalamba joka mchezo kwishney
Huyo dada poa hajui kama Allah na Adam Malima ni pete na kidole! Sasa asubiri kushushwa busha la kike kudadadeki
 
Habari zilizopatikana sasa hivi zinasema Naibu Waziri Adamu Malima ameibiwa kila kitu ktk hoteli ya Loshera mjini Morogoro. Hadi sasa bado yuko ndani ya chumba cha hiyo hoteli hajatoka nje. Inasemekana hata nguo alizoavaa amesaidiwa tu na wasamaria wema.

Yaleyale ya mawaziri kuendelea kuumbuka ugenini!

Manjagy bado yanafuatilia issue hii nzima!

Source: Radio One, muda 13:14 pm

HAKA KA
HAKA KA-THREad ni katamu! KUNA KUKESHA HAPA!








KATAMU..NAHISI KUNA KUKESHA HAPA!!!
 
Kama anakanusha hakuwa na mwanamke aifungulie mashtaka hiyo hoteli. Haikuwa na ulinzi wa kutosha tena katika chumba cha Suite chenye gharama ya 400,000 kwa siku!! Wamlipe fidia.

Otherwise Mheshimiwa ongea wa sauti ya chini!!

Mkuu niko Hotelini hapa na kuna haka kakipeperushi kananikera kanasema hivi: You are urged to deposit your valuable items such as money, computer, camera, fire arms, etc to the receptionist and a receipt will be issued. The hotel shall not be held responsible for any loss caused by violation of this regulation!!

Sijui kama hiyo hotel nayo ilikuwa na haka katangazo. Kananikera kweli.
 
muda 13:14 pm ndo nini,yaan umemaliza mpaka chuo kuandika muda ni mgogoro,pepa lako la form 4 akilipata Dr.Ndalichako lazima akufutie matokeo!

Songoro we noma! Yaani umeachana na issue ya n/waziri kuibiwa unaibuka na Dr. Ndalichako! Lol!
 
A pornographic sleep???!!!

Waswahili bwana ina maana hili neno pono walilitohoa toka kwenye lugha ya malkia? Naona kama yanarandana na kushabihia kwa kutamka na yatokayo na ulafi uwe wa samaki pono ama CHANGU utalala tu usingizi wa pono! Ama kweli kiswahili ni tajiri!
 
Nyinyi mnaoongea hovyo, dirisha la chumba cha Adam Malima limevunjwa.

Na yule ni mtu sala 5 hana upuuzi wa kuwa na malaya.
...usichokijua ni sawa na usiku wa giza; ni busara kukaa kimya kuliko kubahatisha, sala tano aliyeenda sauz kwa jina la kikristo kufanyika dili, ovyoo;
 
Jamani watu wanasema eti mdada hawezi kuruhusiwa kupita getini, nani ana ubavu wa kumzuia mtu mwenye mil 15 mkononi kupita getin na walinzi wetu hawa wenye njaa? Hlf uwezekano wa huyo dada kuchukua chumba fulani hapo kabla ili akitoka atoke kama mwenyeji upo? Mimi mwenyewe huwa nikienda huwa msichana ananikuta au namkuta hatuendi pamoja. Kwa hyo walinzi hawawezi kujua uliingia na nani. Yeye awe mkweli tu aliingia na demu, atoe namba ya huyo du waipeleke TCRA kumtafuta maana najua kwa sasa kazima cm.
 
bwana malima amenukuliwa na itv akisema kuwa ameibiwa fedha pamoja na documents mbalimbali za serikali
katika hotel moja huko morogoro, wezi/majambazi hao wakichukua mabegi yenye documents mbali mbali na kuacha bunduki moja na bastola moja.

MAoni yangu:
1. hii inaweza kuwa ni janja tu ya wizara kujifanya kama imeibiwa documents ili zitakapohitajika waseme wameibiwa, au
kuandaa wizi mkubwa sana hapo wizarani, kupewa kwa nafasi kwa taarifa hii kwenye vyombo vya habari kunanitia
mashaka ni harakati za kuwaandaa wananchi, kisaikolojia tu pindi watakapoamua kuficha/kufanya wanalolipanga
wasishtuke sana.

2. Kwa nchi kama hii ya tanzania waziri anatembea na bunduki ikiwa baadhi ya vituo vyetu vya polisi vinakosa
vitendea kazi kama hizo?, kwa nnavyojua bunduki hutumika kama unahitaji kupigana na maadui wengi kwa wakti
mmoja,je waziri anamaadui wengi kiasi hicho?
 
Back
Top Bottom