Naibu Waziri Adamu Malima aibiwa kila kitu hotelini Morogoro!

Naibu Waziri Adamu Malima aibiwa kila kitu hotelini Morogoro!

Hotel inaitwa Nashela imejengwa yalipo kuwa mashamba ya magereza, pembeni yake ndo ipo boma road..Hotel hiyo inasemekana ni mmoja ya Waziri Mkuu mstaafu.

Tena imejengwa ktk shamba la serikali na wala sio kiwanja cha mtu binafsi,hapo ndipo kazi ipo kwa watu wa aridhi Tanzania
yaani sehemu ya wakulima kujifunza kilimo bora,imeuzwa na kujengwa hotel ya mtu binafsi
 
Jamani kuna wadau hapa wanabisha kuwa morogoro hakuna lodge ya laki nne (4)
kwani hiyo hoteli inaitwaje?


quote_icon.png
By ndyoko

Habari zilizopatikana sasa hivi zinasema Naibu Waziri Adamu Malima ameibiwa kila kitu ktk hoteli ya Loshera mjini Morogoro. Hadi sasa bado yuko ndani ya chumba cha hiyo hoteli hajatoka nje. Inasemekana hata nguo alizoavaa amesaidiwa tu na wasamaria wema.

Yaleyale ya mawaziri kuendelea kuumbuka ugenini!

Manjagy bado yanafuatilia issue hii nzima!

Source: Radio One, muda 13:14 pm
 
TATHMINI ZA KITAKWIMU KUHUSU ZIAARA YA MHE MALIMA MKOANI MOROGORO NAAZMA YANGU KUPINGA NDOTO ZA 'URAIS WA NCHI HII KUPEWA VIJITOTO'

1. Hivi sasa ni Naibu tu wa Waziri -


a. Laptops 2
b. Mabegi 3
c. USD 4,000
d. Hela za Madafu Tshs infinity

2. Akija kutwaa U-Ngeleja -


a. Laptops 4
b. Mabegi 6 USD
c. 8,000
d. Muhuri wa Serikali pajani kusaini mikataba ya gesi na Uranium katika kichochoro chochote kile

3. Akija kutwaa U-Dk Bilal -


a. Laptops 8
b. Mabegi 12
c. USD 16,000
d. Kabeba shehena ya Dhahabu ya nchi kuwafuata nao 'Wawekezaji' kokote waliko.

4. Akija kutwaa U-Kikwete -

a. Laptops 16
b. Mabegi 24
c. USD 32,000
d. Na kuuza eneo zima la Kisarawe, Mbuga zetu, na meneo yote ya Madini na Uranium.


NB: Hadi hapa waheshimiwa sana Zitto Kabwe, Januari Makamba na Rais Kikwete, nasema SITAKI URAIS WA VIJITOTO kwa mtaji wa hii aibu ya mwaka ilitokea Morogoro.

Watu tucheke kidogo halafu turuhusu pia COMMON SENSE kufanya kazi kidogo. Kwa kuwa huyu Mheshimiwa anajulikana hana kiwanda Morogoro, machimbo wala biashaara yoyote ya kumuingizia kiasi kikubwa ajabu hivi ya fedha za kigeni wala yeye kuhitajika kuingizia fedha kwa sarafu hiyo, fedh hizi zote zilikua ni za malengo gani na kutoka mikono gni???

Je, ni kweli kwamba MheMalima alizilipwa hizi USD 4,000 pale Moro na 'Mtu' anyetaka gesi yetu, uranium, u-Dowans aau ni kweli Dr Kashillila siku hizi anawalipa kwa sarfu ya nci za nje????????
 
TAARIFA YA JESHI LA POLISI NI HII:
NAIBU waziri wa nishati na madini Adamu Kigoma Malima ameibiwa vitu vyake vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 katika hotel ya kitalii ya Nashera ya mjini Morogoro ambapo alikuwa amefikia kwa siku tatu.
Kwa mujibu wa mkuu wa upelelezi na makosa ya jinai mkoani hapa Hamis Seleman alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10.45 alfajiri katika hotel hiyo na kwamab uchunguzi wa awali ulibaini kuwa waziri huyo alikuwa amejipumzisha katika sebule ya chumba hicho na kwamba ndipo alibaini kuibiwa vitu hivyo baada ya kurudi chumbani kwake na kutoa taarifa kwa uongozi wa hotel hiyo.
Vitu vilivyoibiwa kuwa ni pamoja na Dola 4000 za Marekani, fedha taslimu shilingi milioni 1.5, pete za silva 2 zenye thamani ya shilingi milioni 2, simu zenye thamani ya shilingi milioni 1.3, balaghashia yenye thamani ya shilingi 50,000, laptop 2 zenye thamani ya shilingi milioni 5.6, taperecorder na headphone milioni 1.
Mazingira ya wizi huo ni kuwa dirisha la chumba hicho ambalo ni la Alminium limevunjwa na kitu cha chuma na hivyo kusababisha mwizi huyo kuingia ndani na kuiba.Alisema kuwa nje ya dirisha hilo zimeoneka nyayo za mwizi pamoja na ndani ya chumba hicho jambo lililoashiria mwizi huyo kuingia hadi ndani hakuna mtu aliyekamatwa.
Akizungumza na waandishi wa habari hotelini hapo na kuthibitisha kuibiwa vitu hivyo Malima alisema kwamba kinachomuuzunisha ni pete yake ya urithi aliopewa na marehemu baba yake pamoja na moja aliopewa na mkewe.
Alisema alikuwa katika ziara ya siku tatu mkoani Morogoro kwajili ya kukagua miradi ya madini na kwamba baada ya kurudi alikaa katika sebule ya hotel hiyo akiangalia taarifa ya habari na kupitiwa na usingizi na kusinzia ambapo alipostuka 10.45 ndipo aligundua kuibiwa vitu hivyo.
Alisema kuwa bunduki na bastola yake havikuibiwa ingwa vitambulisho, pasipoti pamoja na kadi za benk pamoja na dokumenti zake za ofisi zimeibiwa.

Source: Katunews
 
dada poa uyo ni soooo............naibu kalamba joka mchezo kwishney

avatar73087_1.gif


Hivi! wachache sana wataokoka na tamaa!
Kwa hali hii simlaumu Malima hata kidogo!
 
dah mkuu kalambwa kiukweli?mda huu ashatengeneza story kwamba kaibiwa na vibaka wamevunja dirisha,sasa ye alikua wapi?sasa kuna haja gani ya kutembea na mabunduki kibao wakati unapiga usingizi wa pono,mi naona wangemla kiboga ndio wangeua bendi kabisa,na angesema kweli kaibiwa vp
 
ulinzi hafifu jamani

tuwe wakweli wangapi huwa wanafanya hizi inshu??

mlinzi huwa hatakiwi kumruhusu dada kutoka mpaka aliyeingia naye a-confirm, kwetu busia, iko hivyo
Wadada wengine huwa wanapanga kabisa na kuwa wenyeji wakati huo wakiwa mawindoni. Hupata windo na kuondoka asubuhi na mizigo na kwa kuwa alikuwepo pale basi huonekana tu kama mteja anayeondoka asubuhi kuwahi usafiri. Mara nyingi hawa huwa wako very strategic siyo wa Club. Ili kumfanya mwibiwa asishtuke mapema, humpa dozi kubwa ya dawa ya usingizi na kulala hadi muda wa kusafisha vyumba. Hii hutokea mara nyingi. Ila kwa hili la Malima huenda ni issue tofauti na wala si kimada kama alivyokanusha mwenyewe.
 
Kama anakanusha hakuwa na mwanamke aifungulie mashtaka hiyo hoteli. Haikuwa na ulinzi wa kutosha tena katika chumba cha Suite chenye gharama ya 400,000 kwa siku!! Wamlipe fidia.

Otherwise Mheshimiwa ongea wa sauti ya chini!!
 
.....daaahhh! .....e bana mapaparazi noma, eeek!!!!
 
kibaraghashia cha 50,000/- nacho kimekwenda na maji...safi sana wamemuchia magobole yake tu...!
 
A pornographic sleep???!!!

samaki aina pono. Ukitafuna minofu ya samaki huyu,sisi huku pwani tunaamini utalala liusingizi lizito mpaka asbhi. Sio porno kwa kuwa Malima ali...
 
ha ha haa anasikitika zaidi kuibiwa mipete yake
sheikh yahya oyeee!
 
Nasikia Baada ya Kula Lugage akataka Kumdhulumu huyo Binti Ujira wake
 
Kama anakanusha hakuwa na mwanamke aifungulie mashtaka hiyo hoteli. Haikuwa na ulinzi wa kutosha tena katika chumba cha Suite chenye gharama ya 400,000 kwa siku!! Wamlipe fidia.

Otherwise Mheshimiwa ongea wa sauti ya chini!!

.....duhhh, .....jamani mwizi ni mwizi tu, na kuibiwa haina uheshimiwa....

Ajali kazini, alipewa madawa ya kulevya?
Ustaadh hanywi pombe, hii skendeli ya "kupikwa" bana..
 
Wizi wa Morogoro wataipata hachukuwi zaidi ya saa 24, alikisia tu, hakujuwa kuwa alipopindukia ni wrong number.
 
Hiyo Hotel aliyokaa Waziri si ya kufikia. Kama hata waziri anaweza kuibiwa 'vijipesa' vyake kiasi cha dollar 4,000 ina maana hata haina safe za kutunzia vitu vya thamani.
 
TAARIFA YA JESHI LA POLISI NI HII:
NAIBU waziri wa nishati na madini Adamu Kigoma Malima ameibiwa vitu vyake vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 katika hotel ya kitalii ya Nashera ya mjini Morogoro ambapo alikuwa amefikia kwa siku tatu.
Kwa mujibu wa mkuu wa upelelezi na makosa ya jinai mkoani hapa Hamis Seleman alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10.45 alfajiri katika hotel hiyo na kwamab uchunguzi wa awali ulibaini kuwa waziri huyo alikuwa amejipumzisha katika sebule ya chumba hicho na kwamba ndipo alibaini kuibiwa vitu hivyo baada ya kurudi chumbani kwake na kutoa taarifa kwa uongozi wa hotel hiyo.
Vitu vilivyoibiwa kuwa ni pamoja na Dola 4000 za Marekani, fedha taslimu shilingi milioni 1.5, pete za silva 2 zenye thamani ya shilingi milioni 2, simu zenye thamani ya shilingi milioni 1.3, balaghashia yenye thamani ya shilingi 50,000, laptop 2 zenye thamani ya shilingi milioni 5.6, taperecorder na headphone milioni 1.
Mazingira ya wizi huo ni kuwa dirisha la chumba hicho ambalo ni la Alminium limevunjwa na kitu cha chuma na hivyo kusababisha mwizi huyo kuingia ndani na kuiba.Alisema kuwa nje ya dirisha hilo zimeoneka nyayo za mwizi pamoja na ndani ya chumba hicho jambo lililoashiria mwizi huyo kuingia hadi ndani hakuna mtu aliyekamatwa.
Akizungumza na waandishi wa habari hotelini hapo na kuthibitisha kuibiwa vitu hivyo Malima alisema kwamba kinachomuuzunisha ni pete yake ya urithi aliopewa na marehemu baba yake pamoja na moja aliopewa na mkewe.
Alisema alikuwa katika ziara ya siku tatu mkoani Morogoro kwajili ya kukagua miradi ya madini na kwamba baada ya kurudi alikaa katika sebule ya hotel hiyo akiangalia taarifa ya habari na kupitiwa na usingizi na kusinzia ambapo alipostuka 10.45 ndipo aligundua kuibiwa vitu hivyo.
Alisema kuwa bunduki na bastola yake havikuibiwa ingwa vitambulisho, pasipoti pamoja na kadi za benk pamoja na dokumenti zake za ofisi zimeibiwa.

Source: Katunews

alijipunzisha na taulo sebuleni? acheni kutuzuga bana, after all Katunews never be reliable source!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom