Naibu Waziri Adamu Malima aibiwa kila kitu hotelini Morogoro!

Kwanza nampa pole Malima . Lakini baada ya hiyo pole tunauiza
  • Hivi kwenye hiyo hoteli akifika kama waziri(Kiofisi) au Kama Malima...........
  • Kama alikuwa na issue binafsi je kikazi alikuwa Likizo au aitoroka ?
  • Ni usafiri gani na dereva gani alikuwa naye (Wake binafsi au wa sirikali)
 
Petty Cash ya Naibu Waziri wa KiTanzania akiwa ziara za kikazi ndani ya Tanzania:- -Dola za Marekani 4000. -Madafu shs. milioni 1.5.Vitendea kazi:- -Laptop tatu aina ya Dell orijino! -Vinasa sauti viwili aina ya digitali na headphones zake. -Simu tatu kali kabisa aina ya Nokia C6, E200 na Blackberry.Virutubisho:- -Pete mbili za almasi -Kadi mbili za benki. -Mabegi matatu ya nguo. -Barghashia mbili.Acheni WABUNGE wasio mawaziri wajinyonge tu au waachie ngazi kama alivyosema Spika wao.
 
Wamiliki wa hiyo hotel nasikia ni vigogo wawili na wake zao, rafikiangu alitoka huku ulaya december akalala hapo anasema mmoja ni yule Mama wa Mewata MKONDYA na mume wake alafu kuna kajamaa kamoja nasikia kalikuwaga NSSF na kanatabia ya kukameruniwa ni kapare jina linafanana na la Mzee mmoja alikuwaga TDFL kwa sasa yuko kwenye kampuni za migodi linaanza na S.inasemekana katabia kajamaa kakukameruniwa ndio kameunganishwa kwenye Ubiya na mkewe kuficha ufisadi wa vigogo
 


Come again...You mean Hellen Mukondya na mmewe Senkoro wa NSSF ndiyo owners wa Nashera?
 
Wamiliki wa hiyo hoteli ni mzee Msekwa akishirikiana na Nimrod Mkono. Naona watu wanatumia nguvu nyingi kupotosha ukweli.
 
Pole muheshimiwa, si unajua tena boys will be boys. Anyway wish to dedicate mbaraka mwinshehe's song 'jogoo la shamba' for your listening pleasure!
 
hah ha ha wanachanganya dola laki nne na dola elfu nne.
 
Leo nimerudi tena humu ndani na kukuta huu mkasa.

Hivi hii KJA 4 (Kikosi cha Jeshi Awamu ya 4) au maaruf kama Serikali ya Awamu ya nne,

kina matatizo gani? Makamanda wetu vipi???

Ebu angalia mlolongo huu:

- Amiri jeshi mkuu anaanguka mbele ya kadamnasi/haraiki

- Ndani ya miaka miwili ya utendaji, Jenerali msaidizi wa Amiri jeshi anapata ajali ya kiutendaji
kwa kuruhusu kampuni ya mfukoni kukwaa zabuni kubwa na nyeti.

- Jenerali mmoja hivi maarufu kama vijisenti anaivaa Bajaj iliyobeba mabinti saa 9 usiku

- Jenerali mwingine nae anabeba mkataba nyeti wa madini na kwenda kutia
saini hotelini huko ngambo.

- Jenerali mwingine nae katika shuguli mmoja, anawasii wakinamama kuwanyima
waumezao naniino

- Jenerali mwingine anawataka raia kuwaua wale wote wanaohusika na biashara
ya viungo vya albino. Alipobanwa akamwaga machozi mbele ya haraiki.

- Luteni mmoja nae katikati ya barabara anatoa silaha ambayo inahitimisha maisha
ya dereva wa daladala mbele ya abiria na wapitanjia.

- Jenerali mwingine anafumwa akiwa anasinzia ndani ya jumba kuu la maamuzi.

- N.k

Nivi tatizo ni nini?

Makamanda wanakosa ukakamavu na nidhamu.

Kwa haya machache tu je uwezo wa kuwa na kikosi mahiri upooo??????????

Nawakilisha
 
Ni lazima mtu awe mjinga kukubali hii hadithi, baada ya masaa matano ndio waandishi wanaitwa eneo la tukio. Watu wengi hapa wanacheka hapa, ila hili jambo linahuzunisha sana. Huyu Malima na Ngeleja ndio watakaoamua mstakabali wa masuala ya Gesi na mafuta katika nchi yetu. Huyu mtu anayeibiwa kila kitu akiwa amelala, ataweza kweli kusoma fine prints za mikataba? Huyu mtu ambaye haijali afya yake kiasi hicho, anachukua machangudoa (allegedly) ataweza kweli kulijali taifa lake?
 

Yeye Malima anasema kuwa hivyo ni vijisenti.
 
Uchunguzi wa kina ufanyike - na ikigundulika alikua na CD, - JK amfute kazi, full stop!
 
Na mimi nimejiuliza maswali haya



du hii kali muheshimiwa alikuwa sebuleni vi2 vilikuwa chumbani.jambazi alijuaje sasa yuko sebleni ili avunje dirisha akaibe?....

kuna lililojificha hapa, wangekuwa vibaka (wengi) ilikuwa rahisi kuwasikia na kama ni mtu mmoja (?) alibebaje vitu vyote hivyo?
 
Uchunguzi wa kina ufanyike - na ikigundulika alikua na CD, - JK amfute kazi, full stop!

Mbona gazeti la NIPASHE linaandika kwamba dirisha ilibomolewa? Fedha zote hizo alikuwa kahamia hotelini hapo?
Ama kweli nchi ina mafisadi!
 

Mwenzio mjanja sana, umemsikia wakati anahojiwa:

Mwandishi: kwa nini Mhe. unatembea na bunduki mbili?
AM: Maisha yangu yana thamani sana. Lazima yalindwe kwa gharama yeyote!

Viongozi wa nchi hii wana mambo kweli.
 
Wakuu,

Kama wiki moja iliyopita Malima alikuwa mkoani Mbeya, specifically, Saza Gold Mine kule Chunya. Sitoshangaa kukutwa na hizo dola 4,000 or 400,000!!!!!
 

Next victim atakuwa Nchimbi,anapenda kungonoka huyo ni balaa.
 
Huyu na bosi wake Ngeleja walikuwa na tuhuma nyingi ambazo walipaswa hata kabla ya suala la Jairo wawe wamejiuzulu.
Kwa hiyo baada ya suala la Jairo ni lazima wajiuzulu au raisi awafukuze kazi na mpaka hiyo jana kila Mtanzania alikuwa akisubiria hilo!

Sasa kwa 'nyongeza'n ya kosa (tuhuma/kashfa) hii sidhani kama huyu bwana ana tena hadhi ya kuhodi ofisi ya umma, anaweza kuendelea na shughuli zingine za binafsi.

Labda kwa vile ni Jumamosi leo ngoja tusubiria mpaka Jumatatu tuone kama atatangaza kuondoka.

Tusingependa kuona wanaharakati wakishishughulikia suala hili, Mh. Adam usiwapotezee muda, waache washughulikie suala la Mama Nkya na Mh. Mponda.
 
yaani nchii hii inasikitisha, inawezekana kabisa pesa alizoibiwa ni makusanyo aliyoyafanya kwenye migodo mbalimbali ktk ziara yake. Maana nasikia ni practice wakitembelea wawekezaji, lazima waondoke na bahasha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…