Sakata la Mh. Adam Malima maswali mengi bila majibu.
Hivi katika hali ya kawaida, mtu anawezaje kumiliki silaha zote hizo, yaani bastola(pistol) na bunduki kwa ajili ya kujihami na maadui na bado anashindwa kugundua kua tayari hapo alipo ameshazingirwa na maadui(ama ni vibaka ama majambazi) na wanafanikiwa kumuibia mali zake pasipo yeye mwenyewe kushtuka mpaka shughuli nzima ina kamilika pamoja na masilaha yote aliyokua nayo.
Binafsi huu ni udhaifu wa hali ya juu, kua huyu kiongozi anashindwa kumiliki silaha lakini pia anashindwa kujilinda yeye binafsi na hivyo kuhatarisha maisha yake pamoja na maisha ya watu wengine.
Kwa msingi huo napendekeza mara baada ya uchunguzi kukamilika juu ya mazingira ya uvamizi huo na kuthibitika kua kulikua na uzembe kwake yeye binafsi huyu kiongozi anyang'anywe silaha, na aajiri walinzi binafsi na hii ni kwa faida yake mwenyewe sababu hawa wavamizi pia wangeweza kuchagua ama kumuibia hizo silaha ama kumdhuru yeye mwenyewe binafsi ama vyote kwa pamoja.
Lakini pia si vibaya tukajiuliza swali hili, Kwa hoteli ya hadhi ya namna hiyo inawezekana vp kufanyika wizi wa namna hiyo pasipo walinzi wa hoteli hiyo kushtuka mpaka kunakucha pasipo kuacha alama isiyo na mashaka kua hapa kweli wizi ama uvamizi ulifanyika?
Mi nadhani kuna taarifa ambazo bado tumenyimwa juu ya mazingira ya uvamizi huo.
Hatahivyo ni swala la muda tu kabla ya ukweli wote kujulikana.
Pole Mh. Adam Malima kwa hayo yaliyo kukuta