PreGE2025 Naibu Waziri Deus Sangu: Mimi ni mafia, nitawashughulikia wanaotaka kugombea jimbo la Kwela

PreGE2025 Naibu Waziri Deus Sangu: Mimi ni mafia, nitawashughulikia wanaotaka kugombea jimbo la Kwela

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Link hii hapa isikie:-

View: https://www.instagram.com/reel/DJtB-IgC6FZ/?igsh=MXhxMHFobm1lMjduaQ==

Anasema ukienda gombea jimboni kwake anakuua , kukupoteza sababu yeye ni USALAMA WA TAIFA

Mpaka jimba amezuia TUME ya Uchaguzi kuligawa.

Anajibasibu kabisa hakuna mtu kugombea pale labda awe amekufa. Akija mtu Mjinga Mjinga anafyeka asubuhi mapema

nchi ikiendeshwa kihuni na wajinga kupewa kipaumbele kwenye uongozi na uwakilishi, haya ndio matokeo yake. Idiots call the day.

Siku hizi usalama wa taifa imekuwa kazi na sifa ya idiots. Unfortunately the ones calling the shots in Today's Tanzania. Imekuwa kazi ya aibu (embarassment). Nimeshangaa kukuta ndugu zangu wengi wa kila aina (numbheads, sycophants, plain idiots) wakitambulishwa kama usalama wa Taifa! Watu wamekaa kizembe kizembe na kuropoka ropoka ovyo tu.

Gone are the days of Mzena when TISS used to be a prestigious institution of high calibre guys and dolls. Smart and dedicated to the service. Hardly known or recognizable in their special assignments.
 
Enzi medani ni medani kweli, huwezi kusikia upuuzi kama huu. JK aliiharibu sana "medani", 2005-2010, waliingiza vilaza wengi sana kwenye medani kwa kulegeza vetting za mtu kuwa mwanamedani.
Kuna vilaza wengi sana jumba jeupe, zao la 2005 kuja juu huku ni weupe kichwani sio kidogo.

Gone are the days.
 
Hayuko…. Anabwabwaja tu sifa za siasa
Kwa namna Fulani Sheria hupindishwa ukiwa CCM. Unaweza piga jinai safi tu kama Ndugai halafu usishtakiwe! Au ditopile kesi ya murder inabadilishwa jina....mifano IPO mingi akine Gegul etc.
 
Kama kweli Deus Sangu ni TISS operative basi TISS haina right people!! Huwezi kuwa operative wa intelligence agency halafu ukaji UNMASK so foolishly!!
Tiss wakanushe alafu mambo ya Usalama kufanya kazi kwa siri Kuba baadhi ya kazi sio za kufanya kwa siri kwa mfano kukanusha suala kama hili ni muhimu sana kwamba sio mtu wao
 

Mbunge wa Jimbo la Kwela, Deus Sangu, ametangaza hadharani kuwa yuko tayari kutumia mbinu kali kushughulikia watakaothubutu kugombea ubunge katika jimbo hilo. Aidha, ametishia kuwashambulia na kuwaumiza watu wanaochapisha taarifa kumhusu kwenye mitandao ya kijamii.

Katika kauli zake, Sangu amedai kuwa yeye ni jasusi aliyefunzwa na serikali kupitia Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), akisisitiza kuwa mafunzo hayo anayatumia kuwazuia watu asiowataka kuingia au kushindana naye kisiasa ndani ya jimbo la Kwela.

Amedai kuwa kwa kutumia mbinu hizo, amefanikisha kulizuia jimbo hilo kugawanywa kinyume na mipango ya serikali na chama tawala (CCM), akisisitiza kuwa yeye pekee ana uwezo wa kulilinda jimbo hilo kubaki chini ya ushawishi wake kwa njia yoyote itakayohitajika.

Kauli hizo zimeibua taharuki miongoni mwa wananchi na wadau wa demokrasia, huku baadhi wakidai kuwa ni hatari kwa usalama na uhuru wa kisiasa katika eneo hilo.
Labda kuna nati imefyatuka kichwani.
 
Hilo jimbo la kwela lina historia hiyo...maana hizo tabia alikuwa nazo mzidakaya dhidi ya wapinzani wake...
 
Si huwa nasikia TISS ukisema sema vitu kudhalikisha Idara unafichwa au unawekwa safe house, au hii ina baraka zao? Mbona kama ni jasusi ni mweupe sana kwa kichwa yaani hana nywele kabisa
 
Kwa muda wa miaka 5 tu atakuwa ametengeneza zaidi ya bilioni 10, lakini kuna mtumishi wa umma amefanya kazi miaka 40 hajatengeneza hata milioni 200. Ni ujinga ujinga tu

Mshahara pamoja na ma sitting allowance na travelling allowance kwa mwezi ni milioni 18. Tuseme 20.
20M X 12 X 5 years = 1.2 billion TSH

Kiiunua mgongo milion 200

Jumla 1.4 bilion kwa miaka 5

Zinafikaje bilioni 10 ?
 
jamaa amesisitiza balaa ni msomi, ila ukichambua anayo ongea ni upumbavu mtupu

anacho jivunia ni nguvu ya dolla wala hana kitu kichwani.

waziri aliye ambiwa asigawe jimbo na akaridhia nae bwege kama aliye mshauri

huyu ukimpinga atasema umetumwa kumbe ni vile hana akili
 
Back
Top Bottom