Naibu Waziri Mkuu: Magari ya Serikali yafungwe mfumo wa gesi asilia

Naibu Waziri Mkuu: Magari ya Serikali yafungwe mfumo wa gesi asilia

safi sana mpango mzuri sanaa...si hawa chadema wanataka kuleta badili ya ubeligiji badala ya kuja na mipango ya maneleo kama hii wanakalia katibakatiba ushuzi mtupu
Kuna watu wa hovyo sana ona huyu sasa hawa Chawa shida kweli
 
Watu wata lala nae mbele si madereva si wafanyabiashara
 
Hivi hiki cheo kina Ofisi yake kweli? Yaan kuna katibu mkuu wake, wizara, wakurugenzi, etc? Nilidhan ni yeye tu ndio yuko pale hata gari ukute anatumia lile lile la Wizara ya Nishati.
nadhani inafanywa namna, kwasasa bila shaka kunaweza kua na kaimu katibu mkuu ofisi ya Naibu waziri mkuu ili kuepusha contradictions baina ya kazi na majukumu za wizara ya Nishati na ofisi ya Naibu waziri mkuu.

aina ya security na msafara wake vinajieleza kua ni ofisi iliyokamilika na inajitegemea.
 
Umeelewa swali langu?
Labda nikupe kwanini nimeuliza swali hilo.

1. Diesel
Hii huwa inapokandamizwa na piston, inafikia sehemu, mkandamizo huo husababisha diesel kulipuka yenyewe na kuisukuma piston katika combustion chamber kuelekea chini na mwisho kupata rotation kwenye crank shaft. Diesel haihitaji spark plug kupata mlipuko huo.

2. Petrol
Petrol inapokandamizwa na piston, inahitaji cheche ili ilipuke na mwisho itengeneze rotation kwenye crank shaft kama inavyotokea kwenye diesel. Kwa hiyo mpaka hapo, tofauti kubwa kati ya mashine inayotumia petrol na diesel ni uwepo wa spark plugs kwenye petrol engine wakati diesel engine haina.

Unapoongeza mfumo wa gesi, maana yake unatumia combustion chamber zile zile zilizopo kwenye gari. Sasa gesi nayo ikikandamizwa, hailipuki kama ilivyo diesel, ni mpaka msaada wa cheche toka kwenye spark plug kama ilivyo mashine ya petrol.

Sasa swali langu msingi wake ni kuwa gesi inahitaji spark plug, lakini diesel haihitaji, utakapoweka system ya gesi kwenye diesel engine, nini kinafanyika kuhusu ulipukaji wa gesi na diesel? Wanahusiasha spark plugs wakati wa gesi na kuziacha wakati wa diesel?
Ondoa nadharia zako hapa kila mtu anajua iliyoandika siyo wewe tum Mbona kuna magari yanatumia gesi na nchi zingine kama India hata Bajaj zinatumia gesi.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko ameelekeza utaratibu wa kubadili mifumo ya magari kutumia gesi asilia uanze na magari ya serikali na kuwa vituo zaidi vijengwe ili kupunguza matumizi ya mafuta.

View attachment 2749046
Amefanyia utafiti athari na faida za matumizi ya gesi asilia katika nchi yetu? Tuna infrastructure ya kuhudumia hayo magari? Nani atabadilisha mifumo hiyo katika magari ya serikali? Temesa ambao ndio wenye jukumu la kuhudumia magari na vyombo vingine vya serikali wana mawazo gani? Na je wana uwezo? Kubadilisha mfumo katika mavieiti ( maana haya ndio yanatumia sana mafuta) uta affect vipi performance yake? Na kadhalika, na kadhalika. Alipaswa kwanza kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kutoa tamko hadharani.

Amandla...
 
Ondoa nadharia zako hapa kila mtu anajua iliyoandika siyo wewe tum Mbona kuna magari yanatumia gesi na nchi zingine kama India hata Bajaj zinatumia gesi.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
Ni kweli ukisemacho, lakini hizo gari au bajaj zinazotumia gesi leo, zilibadilishwa toka kwenye kutumia mafuta kuja gesi au zilitengenezwa kutumia gas toka day one?
 
Ni kweli ukisemacho, lakini hizo gari zinazotumia gesi leo, zilibadilishwa toka kwenye kutumia mafuta kuja gesi au zilitengenezwa kutumia gas toka day one?
Zinaongezewa mfumo wa gesi na ikitokea gesi ikaisha akiwa mahali ambapo hakuna gesi anarudi kwenye mfumo wa mafuta.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Sawa ndugu naibu waziri mkuu. Lkn lengo lako ndugu naibu ni nn hasa?

**Kwamba tutumie gesi yetu? (Siyo yetu tena, Kikwete alimuuhzia machina).
**Ni nafuu kuliko petrol na diesel? (Kwa uhaba huu wa dola tulionao Sasa hivi bei ya gesi itakuwa sawa na ya petrol na diesel).
Sawa bavicha wazee wa kupinga kila kitu bila kutoa suluhisho
 
Zinaongezewa mfumo wa gesi na ikitokea gesi ikaisha akiwa mahali ambapo hakuna gesi anarudi kwenye mfumo wa mafuta.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
Sawa uyasemayo, lakini, ni kwa gari zote za petrol na diesel, au petrol pekee..!!?? Wewe binafsi umeshaona gari ya diesel iliyoongezewa mfumo wa gesi? Binafsi najua gari za diesel huwezi weka gesi (kama nakosea ndo nielimishwe).

Magari ya serikali mengi sana ni ya diesel. Naibu waziri mkuu, aliposema gari za serikali zitumie gesi, alimaanisha watanunua gari mpya za kutumia gesi au wataongeza mfumo wa gesi kwenye gari zilizopo zote zikiwemo za diesel? Au hili la diesel wame-overlook?
 
Back
Top Bottom