Naibu Waziri Mkuu: Magari ya Serikali yafungwe mfumo wa gesi asilia

Naibu Waziri Mkuu: Magari ya Serikali yafungwe mfumo wa gesi asilia

Hayo magari yatakuwa yanatembea Dar peke yake ? Maana vituo vya Gass kwa magari sidhani kama vipo Kila mahali
 
The Boss Hii kauli angesema January Makamba kama naona ambavyo raia wangesema anataka kupiga hela kupitia gesi ya "Rostam" hahahaha.
Kama ni lengo la kudhibiti matumizi ya serikali basi ni kwenye maeneo kama hayo mafuta ambayo huwa yamwagwa tu watu wajijazia tu mafuta kwenye hayo maV8 na hakuna stakabadhi au zipo za kughushi.

Atakiwa afanya iwe ni "pilot program" kwa kuanza mkoa mmoja tu na ikifanikiwa aendeleze mikoani.
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko ameelekeza utaratibu wa kubadili mifumo ya magari kutumia gesi asilia uanze na magari ya serikali na kuwa vituo zaidi vijengwe ili kupunguza matumizi ya mafuta.

View attachment 2749046
Watoe tozo ya mitambo inayotumia gas ktk magari waache maneno,mafuta miradi ya watu
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko ameelekeza utaratibu wa kubadili mifumo ya magari kutumia gesi asilia uanze na magari ya serikali na kuwa vituo zaidi vijengwe ili kupunguza matumizi ya mafut
View attachment 2749046
 
Wanaanzaga hivi hivi ila subiri ripoti ya CAG hutoamini macho yako. Utasikia mfumo wa gari moja umebadilishwa kwa million 10
Hiyo 10M watasema ni ndogo chukua:

Kifaa chenyewe gharama yake.

Labour charge

Disposal ya mfumo wa zamani maana si kwenda kutpa tu kutaharibu mazingira.

Na VAT
 
Na wakuu wa idara wanaopewa mafuta itakuaje....jamaa anataka kuwanyoosha
 
safi sana mpango mzuri sanaa...si hawa chadema wanataka kuleta badili ya ubeligiji badala ya kuja na mipango ya maneleo kama hii wanakalia katibakatiba ushuzi mtupu
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko ameelekeza utaratibu wa kubadili mifumo ya magari kutumia gesi asilia uanze na magari ya serikali na kuwa vituo zaidi vijengwe ili kupunguza matumizi ya mafuta.

View attachment 2749046

Kama wakifanya hivo bhc watapunguza gharama kubwa xnaa kwa serikali
Nashangaa na hili pia mnapinga sijui mnataka nn nyie
 
Naomba kuuliza kwa yeyote mwenye uelewa..!! Hivi kubadili system ya gari kutoka ya mafuta na kuja ya gesi, ni kwa magari yote ya mafuta ya petroli na diesel au petroli pekee..!!??

Je huwezi ukawa na mifumo yote miwili
 
Kutamka ni jambo moja, kutenda au kutekeleza ni jingine.
Kwa nyakati hizi za teknolojia ya habari na mawasiliano, tukiamua kubadilisha magari kutumia gesi, vyuo vyote vya VETA vinaweza kufanya ndani ya ya miezi sita, kwa kununua vifaa kutoka kwa watengenezaji wanaojulikana.
Changamoto kubwa ni viongozi na wenye madaraka kukosa uelewa wa hali halisi hivyo kukuza jambo dogo kulipeleka vyuo vya juu au nje ya nchi (huo siyo utafiti, ni kufunga vifaa kwenye mitambo, vinavyojulikana vinavyofanya kazi).
Wageni hutumia ujinga wa viongozi kutupiga serikalini.
Hiyo kauli pekee imeshapigiwa hesabu kubwa na makampuni mengi ya kigeni na lobbying tayari imeshaanza.
Kitu muhimu ni kujenga uwezo wa ndani.
Changamoto nyingine ni bei za CNG stations na trailer za kusambaza nchi nzima.
Kwa kuanzia, kipaumbele kiwe mikoa ya kusini hadi Dare es salaam ambapo kuna bomba la gesi.tayari.
Mikoa mingine itakayotumia usafiri wa barabara (trailers) ifuate kulingana na mahitaji ya sekta binafsi.
 
Back
Top Bottom