Naibu Waziri Mkuu: Magari ya Serikali yafungwe mfumo wa gesi asilia

Naibu Waziri Mkuu: Magari ya Serikali yafungwe mfumo wa gesi asilia

Gari lafungwa mfumo wa pili wa kutumia gesi badala ya mafuta. Hivyo baadae ule mfumo wa mafuta waweza kuondolewa au kuachwa umefungwa usitumike moja kwa moja. Zipo kampuni kadhaa zenye utanzu na kampuni za nje zinofanya mambo haya na huenda ndo ziko nyuma ya wazo la Naibu Waziri Mkuu.

Uuzaji mafuta waweza kuendelea kwani ipo mitambo na mashine nyingi ambazo zahitaji mafuta.

Mzee wa MSG ataridhia tu kwani yeye ana ufahamu na masuala ya maglobalists ambao ndo wataka magari yatumie mawe ya lithium.

Tanzania tunayo gesi ya kutosha hivyo tayari fursa imepatikana.
Umeelewa swali langu?
Labda nikupe kwanini nimeuliza swali hilo.

1. Diesel
Hii huwa inapokandamizwa na piston, inafikia sehemu, mkandamizo huo husababisha diesel kulipuka yenyewe na kuisukuma piston katika combustion chamber kuelekea chini na mwisho kupata rotation kwenye crank shaft. Diesel haihitaji spark plug kupata mlipuko huo.

2. Petrol
Petrol inapokandamizwa na piston, inahitaji cheche ili ilipuke na mwisho itengeneze rotation kwenye crank shaft kama inavyotokea kwenye diesel. Kwa hiyo mpaka hapo, tofauti kubwa kati ya mashine inayotumia petrol na diesel ni uwepo wa spark plugs kwenye petrol engine wakati diesel engine haina.

Unapoongeza mfumo wa gesi, maana yake unatumia combustion chamber zile zile zilizopo kwenye gari. Sasa gesi nayo ikikandamizwa, hailipuki kama ilivyo diesel, ni mpaka msaada wa cheche toka kwenye spark plug kama ilivyo mashine ya petrol.

Sasa swali langu msingi wake ni kuwa gesi inahitaji spark plug, lakini diesel haihitaji, utakapoweka system ya gesi kwenye diesel engine, nini kinafanyika kuhusu ulipukaji wa gesi na diesel? Wanahusiasha spark plugs wakati wa gesi na kuziacha wakati wa diesel?
 
... mfano tu; yale malori ya Dangote (50 tons) yaliyotapakaa nchi nzima yanatumia CNG. Africa's #1 billionaire ana-prefer CNG; serikali inayolia kila siku "kasungura kadogo" inaendekeza sio tu highly luxurious cars ila pia expensive running costs.
Yamekuwa deisigned hivyo toka kiwandani yalikotengenezwa au yalibadilishwa toka diesel au petrol kwenda gesi?
 
akianzia palepale ofisi ya Naibu waziri mkuu atakua ametisha zaidi
Hivi hiki cheo kina Ofisi yake kweli? Yaan kuna katibu mkuu wake, wizara, wakurugenzi, etc? Nilidhan ni yeye tu ndio yuko pale hata gari ukute anatumia lile lile la Wizara ya Nishati.
 
Kwa kuwa mola ametujalia gas yetu, na kwa bahati nzuri inaweza kutumika, basi tujiwekee mkazo zaidi katika kutumia nishati yetu katika mifumo mbalimbali ili tupunguze ununuzi wa nishati ya mafuta japo kwa 25% tutaokoa pia dollar zetu.
 
Mm nashauli... Waweke oda maalum huko yanakotengenezwa yaje yakiwa yameshafungwa mfumo huo wa ges..ila kukalabati haya , jinsi wanavyo weka mitungi ndani ya gari kuna mashaka sana kiusalama.
Ila yakija kutoka kiwandani tayar yana huo mfumo..naamini wanaweza kujenga mfumo mzuri wa mitungi. Maana kwenye kiwanda wanaweza kujenga mitungi ya bar cube, au pipe ambazo pia ikatengenezwa kwa uimala zaidi kutokana na shughli za kiserkali na umaalum wa hiyo mitungi.
 
Mm nashauli... Waweke oda maalum huko yanakotengenezwa yaje yakiwa yameshafungwa mfumo huo wa ges..ila kukalabati haya , jinsi wanavyo weka mitungi ndani ya gari kuna mashaka sana kiusalama.
Ila yakija kutoka kiwandani tayar yana huo mfumo..naamini wanaweza kujenga mfumo mzuri wa mitungi. Maana kwenye kiwanda wanaweza kujenga mitungi ya bar cube, au pipe ambazo pia ikatengenezwa kwa uimala zaidi kutokana na shughli za kiserkali na umaalum wa hiyo mitungi.
Gari nyingi kwa sasa tayari zina mfumo wa gas, nimeona baadhi ya daladala ambazo tayari zinamfumo huo.
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko ameelekeza utaratibu wa kubadili mifumo ya magari kutumia gesi asilia uanze na magari ya serikali na kuwa vituo zaidi vijengwe ili kupunguza matumizi ya mafuta.

View attachment 2749046
Hapa madereva watamwendea kwa karumanzila kwakutaka kuondoa ulaji wao mkubwa
 
Back
Top Bottom