Naibu Waziri wa Afya, Dkt Godwin Mollel, kuzungumza na vyombo vya habari leo 11 Februari 2021

Naibu Waziri wa Afya, Dkt Godwin Mollel, kuzungumza na vyombo vya habari leo 11 Februari 2021

nyumbamungu

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2017
Posts
1,033
Reaction score
895
Leo Februari 11 Mwaka huu kuanzia mchana Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Watoto, Daktari Godwin Mollel atazungumza na vyombo habari na matangazo hayo kurushwa mubashara na TBC Taifa kuzungumzia hali ya Afya hapa Nchini kwa ujumla wake.

Mfahamishe ambaye hana taarifa.
 
Leo Februari 11 Mwaka huu kuanzia mchana Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Watoto, Daktari Godwin Mollel atazungumza na taifa kupitia vyombo habari na matangazo hayo kurushwa mubashara na TBC Taifa kuzungumzia hali ya Afya hapa Nchini kwa ujumla wake, mfahamishe ambaye hana taarifa.
Taja muda wewe mtu.
 
Leo Februari 11 Mwaka huu kuanzia mchana Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Watoto, Daktari Godwin Mollel atazungumza na taifa kupitia vyombo habari na matangazo hayo kurushwa mubashara na TBC Taifa kuzungumzia hali ya Afya hapa Nchini kwa ujumla wake, mfahamishe ambaye hana taarifa.
This is duplication of efforts. Jana Mganga Mkuu wa Serikali kazungumza, leo tena tunaambiwa Naibu Waziri wa Afya ataongea!!!!......that's well, cha msingi wasije wakapishana and then wakawachanganya wananchi.

Kwa nchi za wenzetu, msemaji wa mambo ya Afya anakuwa ni mmoja tu ili;

1. Wananchi waheshimu hayo matamko

2. Kuondoa kudharauliana kwa watoa matamko

3. Wananchi wawe na uelewa ulio thabiti kuhusu jambo hisika

4. Kupata msimamo thabiti wa serikali

5. To avoid duplication of efforts

Kwahiyo, ni mategemeo yetu kuwa Naibu Waziri wa Afya ndugu Mollel hataukosoa au kupingana na msimamo wa Mganga Mkuu wa Serikali ndugu Makubi, asante!!!!!
 
Mbona tayari sijamwelewa wakati bado hajaongea!!? Kichwa changu hiki kwakwelii[emoji21]
Ni kweli kabisa, siku zote ndugu Mollel ambae ndie Naibu Waziri wa Afya haelewekagi anavyoongea.

Jana nilivyokuwa nasikiliza taarifa ya habari ya saa 5 usiku kupitia kituo cha Azam TV, mtangazaji Ms. Ivona Kamuntu alijaribu kumuuliza vipi msimamo wa Serikali kuhusu COVID 19.

Badala ya kujibu hoja akaanza kuongea vitu visivyoeleweka na ku-dwell sana kumuongelea Tundu Lissu kuwa alivyokuwa anakuja kutoka ugaibuni alivaa barakoa lakini bada ya kutua tu Tanzania akaachana na kuvaa barakoa, eti hata kwenye kampeni zake hakuwa anavaa barakoa.

Huyu Mollel ni mzigo sana, badala ya kuelezea kama alivyoulizwa na mtangazaji yeye anamuongelea mtu.......this is rubbish and shame on him!!!!!
 
"Wataalam wa WHO waliokuwa wanachunguza kama chanzo cha covid-19 ni kwenye Jimbo la Wuhan (China) wamethibitisha kuwa sio kweli kirusi hicho hakikuanzia kwenye maabara ya jimbo hilo ... "

"Watafiti wamegundua kuvaa barakoa mbili kwa mpigo kunapunguza uwezekano wa kupata covid kwa asilimia 95..."
nimeiona Fox News leo asubuhi! nimejikuta nawaza hivi:

Binadamu bila kujali ni kutoka Magharibi au Congo, msomi au hajasoma, wota tuna tabia moja TUNAPENDA KUTAFUTA FARAJA hata pasipo, naona hata hapa JF wengi wanatafuta FARAJA....chanjo ni FARAJA, barakoa ni FARAJA, kujitenga ni FARAJA, naibu Waziri wa Afya ataongea FARAJA.

Nje ya faraja ni PAIN (ukweli ni PAIN) Tukiambiwa ukweli kuwa wazungu na teknolojia zao hawajajua korona ni nini tunakataa kwakuwa ukweli ni PAIN.....naishia hapa kwa kuwa watakaoelewa hawafiki 10.
 
"Wataalam wa WHO waliokuwa wanachunguza kama chanzo cha covid-19 ni kwenye Jimbo la Wuhan (China) wamethibitisha kuwa sio kweli kirusi hicho hakikuanzia hapo... "

"Watafiti wamegundua kuvaa barakoa mbili kwa mpigo kunapunguza uwezekano wa kupata covid kwa asilimia 95..."
nimeiona Fox News leo asubuhi! nimejikuta nawaza hivi:
Binadamu bila kujali ni kutoka Magharibi au Congo, msomi au hajasoma, wota tuna tabia moja TUNAPENDA KUTAFUTA FARAJA hata pasipo, naona hata hapa JF wengi wanatafuta FARAJA....chanjo ni FARAJA, barakoa ni FARAJA, kujitenga ni FARAJA, naibu Waziri wa Afya ataongea FARAJA....
Nje ya faraja ni PAIN (ukweli ni PAIN) Tukiambiwa ukweli kuwa wazungu na teknolojia zao hawajajua korona ni nini tunakataa kwakuwa ukweli ni PAIN.....naishia hapa kwa kuwa watakaoelewa hawafiki 10....
Watu hutawalia kisaikolojia kwanza huko kunakofuata ni mteremko tu.!
 
Back
Top Bottom