Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile atenguliwa, Godwin Mollel achukua nafasi

Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile atenguliwa, Godwin Mollel achukua nafasi

kwa taarifa tu Dr ndungulile ndio alikuwa kichwa kweny wizara si muongeaji ni mtendaji by professional ni daktari haswaa sio wa kuokota PhD kama humjui kaa kimya
Hii ni korona au mengineyo ndo yamekuvuruga? Naona unahara wakati hujaombwa choo😎
 
Kina Ndugulile na wenziye walipaswa kutambua kwamba kusema kweli katika siasa ni dhambi iliyo kuu.

Siasa ni kete tabiri na wanasiasa wote huiishi.Ajabu kina Ndugulile walitaka kuleta Mambo ya ukweli ndaniye ilhali haikutakiwa.

Dhana ya mwanasiasa usimwamini ndiyo inaleta maana ktk hilo.

Huwezi kuwa mkweli na ukadumu katika siasa,never!
 
.
20200517_090251.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli: Tujaribu kutumia njia nyingine za asili kama kujifukiza. Kujifukiza ni scientific kwa kuwa mvuke wa maji, maji yanakuwa vapour yakiwa 100 degree centigrade ambazo zinaweza kumyeyusha coronavirus.
==================

Kujifukiza sio njia sahihi wala tiba ya kuua virusi vya corona. Unapojifukiza unaweza kuleta athari ya kuunguza njia ya hewa, njia ya hewa haijatengenezwa ili kuingiza moto mwilini mwako. Nitoe rai hii sio njia sahihi. # Naibu Waziri was Afya, Dr. Faustine Ndugulile.
IMG_20200517_075037.jpg
 
Anayetoa majukumu ndio anajua kwamba unastahili kuondoka au kuendelea kuwepo kwa sababu ana uwezo wa kukufanyia tathmini, jipe muda wa kujua nini kilijiri mpaka akaondolewa.

Binafsi, naamini Ndungulile alijisahau na kujiona ndio msemaji wa wizara kwa kuchukua majukumu ya waziri wake, kwa kuwa tu ana taaluma ya udaktari. Mara nyingi nilikuwa namuona hivyo.
 
Ngoja niliweke sawa hapa kuhusu Ndugulile.

Kauli zote mbili (kupinga kujifukiza na kutumia barakoa za kitambaa) alizowahi kuzitoa Dr.Ndugulile kuhusu Corona ambazo zimepingana na kauli za mheshimiwa Rais, Dr.Ndugulile alizitoa kabla ya mheshimiwa Rais kutoa kauli zake.

Hakuna namna yoyote ile Dr. Ndugulile angeweza kwenda sambamba na kauli za mheshimiwa Rais wakati alikuwa hajui Rais atakuja kusema nini.

Hii inatupa picha moja kubwa sana katika serikali ya awamu hii kuwa hakuna kitu kinaitwa serikali kwa sasa bali tuna kitu kinaitwa Magufuli na wengine wote serikalini ni wapiga makofi au wagonga meza wa Magufuli.
 
Na hii ndo inaleta maana halisi ya huyu jamaa yetu, hataki watu wasema ukweli, wachambuzi wa mambo kitaaluma, hao kwake hawana nafasi na ndo anatuma ujumbe kwa wengine woote waliopo kwenye kungoja teuzi.

Watu wake ni wale wapaka mafuta wa mambo, waongo waongo.

Wanatumbua macho mbele ya kamera kama wanaongea point kumbe pumba tupu, watu wazima hovyo.

Maprofesa wa matumbo ndo jamaa zake hasa.
 
Anayetoa majukumu ndio anajua kwamba unastahili kuondoka au kuendelea kuwepo kwa sababu ana uwezo wa kukufanyia tathmini, jipe muda wa kujua nini kilijiri mpaka akaondolewa.

Binafsi, naamini Ndungulile alijisahau na kujiona ndio msemaji wa wizara kwa kuchukua majukumu ya waziri wake, kwa kuwa tu ana taaluma ya udaktari. Mara nyingi nilikuwa namuona hivyo.
Obviously alikuwa anaeleweka Kwanza ni mwenzetu. Yule mwingine tunaangalia mkia na vitambaa lkn anachokisema hatukisikilizi maana sio chetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wengi ni malofa.

Ndugulile aliongea ishu ya kujifukiza na barakoa za N95 kabla ya Magufuli...hivyo hakwenda kinyume na boss wake.

Pili ni kama unasema siasa nguzo yake kuu ni uongo...sasa hii siasa ipo kwa faida ya nani?

Serikali zijazo ziweke Sayansi ya siasa kama somo la lazima kuanzia primary mpaka form six.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyethibitisha hiyo miti ina impact ya ku compromise viral activity ni nani na kama inafanya kazi iwe extracted zipatikane vaccine....na hili swala la nyungu walitakiwa watumie watu gani yani mtu tayari ni victim ana dyspnoea afu ajifukize wakati tayari ana respiratory depression....medicine ni ngumu sana ila basi tuheshimu tu maamuzi ya mzee wetu.. Nimefikiria kwa sauti kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
ku compomise viral activity? Iwe extracted zipatikane Vaccines? Wakati tayari ana respiratory depression? Medicine ni ngumu sana?
Kazi ipo!
 
Ummy yeye anawasilisha anachoambiwa aongee tu na kwahili kafanikiwa. Ndugu yangu Ndugulile kwenye hii awamu ukweli haujawahi kumueka yeyote huru.
 
Back
Top Bottom