Naibu Waziri wa Habari aagiza washindi wa Shaaban Robert watunge wimbo kumsifu Magufuli kwa gharama za Serikali

Huyu jamaa ana 4 years to go, kwanini wanamwogopa hivi? Wanajua nini ambacho hatujui? Mbona Mkapa na Kikwete hatukuona haya mambo?
Huyu tofauti sana, haheshimu sheria, katiba wala hataki kuonekana mstaarabu. Na unaweza kutumbuliwa kwa kuonekana huimbi pambio vizuri tu.

Watu wanapalilia kula yao.
 
Usijifanye wewe hapa duniani humtgemei binadamu, yaani uko kivyako Kama nyumbu.

Biblia imesema alaaniwe amtegemeaye mwanadamu HUKU AMEMSAHAU MUNGU.

Usikatishe vifungu vya biblia ili upate maana ya kishetani utalaaniwa.
Hakuna andiko kama hilo.Usichanganye siasa na biblia,ni elimu mbili tofauti.
 
Hawa mawaziri hawajui bado wapo probation badala ya kufikiria nje ya Box ni jinsi gani hao vijana wanaweza kuzalisha contents ambazo zitawaingizia pesa na ajira hivyo serikali kupata kodi yeye anaongeza expenditures kwa serikali ambazo hazina kichwa wala miguu maana ni very personal na hata kama ameota Raisi anataka Glory na yeye kaamua kujipendekeza basi azitoe hizo gharama mfukoni kwake.
 
Wapi waziri au mleta mada kasema kumtukuza Magufuli?
Kasema kumsifu na kusifiwa binadamu akifanya vizuri ni kawaida hajasaema kumtukuza kuwa mwelewa usilete geuzageuza yenu ya maneno.

Kama kufanya vizuri kunahitaji sifa ni sawa, ila watu waamue wenyewe sio kuagizwa.
 
Hizi tabia ndio zinamfanya mh Rais aonekane ana tabia za kidikteta
 
Wapi waziri au mleta mada kasema kumtukuza Magufuli?
Kasema kumsifu na kusifiwa binadamu akifanya vizuri ni kawaida hajasaema kumtukuza kuwa mwelewa usilete geuzageuza yenu ya maneno.
Ningekuwa JPM ningekemea kimyakimya ujinga huu wa baadhi ya viongozi kuwageuza wananchi mazezeta ya kusifusifu na kupongeza ovyo ovyo kwa maslahi yao binafsi.

Rais JPM huko ulipo Nakuomba kemea tabia hii ya Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Viongozi wa dini ya kutumia wananchi kwa maslahi yao. Wanakupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Watanzania wengi wanatambua utendaji wako ktk nchi, lakini hakuna sababu ya hii brainwashing!

Rais Magufuli tafadhali andaa Taifa la wenye akili na uwezo wa kufikiri badala ya Taifa la watu wanaosifusifu wengine. Kila moja wetu atimize wajibu wake ktk nchi hii siyo kusifusifu.
 
Ni jambo jema.

Huyu Ulega mwanae anaitwa Tulia Ackson Ulega kwa sababu alizaliwa siku aliyoapishwa Naibu Spika wa bunge!
 
Jina la Mheshimiwa mtukufu Naibu Waziri tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…