Naibu Waziri wa Maji atoa wiki 2 kwa mkurugenzi, Rais Samia apigilia msumari ''hi kero nisiikute''

Naibu Waziri wa Maji atoa wiki 2 kwa mkurugenzi, Rais Samia apigilia msumari ''hi kero nisiikute''

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
ENG. MARYPRISCA MAHUNDI - NAIBU WAZIRI WA MAJI ATOA WIKI 2 KWA MKURUGENZI, RAIS SAMIA APIGILIA MSUMARI ''HI KERO NISIIKUTE''

Mhe. Eng. Mahundi akiwa Usa River Ausha amesema kuwa Wizara ya Maji imepeleka neema ya miradi ya Maji ili kutimiza dhamira njema ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kumtua ndoo mwanamke kichwani.

"Kwenye jimbo la Arumeru tumeshaleta fedha nyingi na miradi mingi ya maji na utekelezaji wake unaendelea. Tuna mradi mkubwa wa Kibao uliozinduliwa na Mwenge wa Uhuru, zaidi ya Milioni 650 ilitumika. Tayari wananchi wanafurahia huduma ya maji safi na salama ya bomba" - Mhe. Eng. Mahundi, NW Maji

"Bilioni moja na milioni 200 Usa River inakwenda kubaki salama kwa kupata Maji safi bombani. Mradi utakamilia kufikia mwaka ujao wa fedha. Kwa kipindi hiki tunaleta mradi utakaondosha changamoto, maumivu na machozi ya wana Usa River" - Mhe. Eng. Mahundi, NW Maji

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi awahakikishia huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza Arumeru.

Mhe. Eng. Mahundi alishiriki kwenye msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alizungumza na Wananchi wa Usa River, Arumeru Mkoani Arusha wakati akielekea KIA baada ya Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali, tarehe 05 Machi, 2023.

#KAZIIENDELEE
#MAJINIUHAI

WhatsApp Image 2023-03-06 at 14.29.42.jpeg
FqdL50zXgAICM48.jpg
 
Kwanza nashangaa suala la maji eti mtu mpaka ukajaze fomu sijui bla bla kibao, inatakiwa wazunguke mitaa yote hakuna maji wafunge mita hela zao zitarudi kwenye malipo, lakini sio kwa nchi hii.
 
Back
Top Bottom