Wanabodi,
Kichwa cha habari cha bandiko hili kinajieleza wazi, hili likiwa ni bandiko la swali, kuwa Siku Zote Huwa Nailaumu Chadema Kuwa Hawajitambui na Hawajui Wanataka Nini!. Sasa Kesho Chadema Wanafanya Uchaguzi wa Mwenyekiti, Swali ni Jee Sasa Chadema Wanajitambua?, Jee Wanajua Wanataka Nini?...
Katika Uchaguzi wa Kesho wa Mwenyekiti wa Chadema, Kama Chadema Wanajitambua, Watachagua Kuishi, Lakini Kama Bado Hawajitambui Kama Kawaida Yao, Watachagua Kifo!.
Swali ni Jee Chadema Kuchagua Kifo au Kuishi?. Tusubiri Hiyo Kesho Tuone...
Naanza Bandiko Hili na Declaration, Kisha Naleta Justification
Naomba kuanza kwa declaration of interest, mimi Paskali wa Jeiefu, sio mshabiki, mfuasi, au mwanachama wa chama chochote cha siasa, lengo la declaration hii ni kwa ajili ya manazi wa Chadema waliotamalaki humu JF, ambao ukichangia jambo lolote ambalo hawalipendi, watakushukia kwa kukubeza, kwa vile wewe sio Chadema, mambo ya Chadema, yanakuhusu nini?!, hivyo maneno kama "pilipili usioila inakuwashia nini?" hayawezi kukosekana. Naamini kuna Watanzania wengi kama mimi ambao sio wanachama wa chama chochote cha siasa, na kuna wanachama wa vyama vya siasa ambao wako very objective kwa maslahi ya taifa wakiwemo wana CCM ambao wangependa kuona, nchi yetu inapata credible opposition, kwa huku Bara, Chadema ndicho chama pekee kilichoonyesha angalau kinaweza, ila baada ya kutokea huyu game changer aliyabadili the political game, Chadema imeporomoka na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kama Chadema hawatafanya the right thing now, they are going to be reduced to nothing. Chadema ikifa, sio hasara kwa Chadema na wanachama wa Chadema tuu, ni hasara kwa Taifa na Watanzania kwa ujumla kwa nchi kurejea chini ya mfumo wa chama kimoja which is not good at all kwa majaaliwa ya mustakabali wa taifa letu.
Justification
Kuna justification kubwa moja kwa mtu ambaye sio Chadema kujadili mambo ya Chadema. Chadema kwa vile ni chama cha siasa na kina wanachama, kuna watu wanadhani Chadema ni private party, interms of usajili na kujiunga hivyo ni mali ya wanachama na viongozi wao pekee, no!, Chadema is a public party, nichama cha umma wa Watanzania, na kinaendeshwa kwa kugharimiwa na tax payers money, hivyo ni public party, kwenye kitu kinachoitwa "private property no right to trespass", hii maana yaye ni mali ya mtu binafsi ina kinga ya kisheria ya kutoingiliwa, na hata katika mienendo na maisha binafsi ya watu wakiwemo viongozi, kuna kinga ya kifaragha, "the right to privacy" ambayo haipaswi kuingiliwa, lakini mtu yoyote, au taasisi yoyote inayolipwa with tax payers money, inapoteza hizo kinga zote mbili za private propery na the right to privacy, the tax payers have all the rights to know the public as well as the private conduct of such entity maana nikodi zao!. Kwa vile Chadema kinaendeshwa kwa ruzuku, hiyo ruzuku ni fedha yako, fedha yangu na fedha yetu as public, hivyo we have all the rights, kujua kila kitu kuhusu Chadema na kutoa maoni yoyote kuhusu Chadema, na ndio maana hesabu za Chadema, zinakaguliwa na CAG.
Hoja za Bandiko hili
Japo Chadema wenyewe hawajikubali na kuukubali ukweli kuwa Chadema hapa kilipofika kama chama kikuu cha upinzani kiko stagnant na graph yake imeanza kushuka kwa kasi ambapo viongozi na wanachama wake wanaojitambua, they are doing the right thing, wengine wanasubiri tuu Bunge livunjwe nao waamue, hivyo wana Chadema kindakindaki wenye misimamo thabiti, walioamua kuifia Chadema, itawabidi wajitambue "Kama Chadema Sasa Wanajitambua, na Wanajua Wanataka Nini, Watamchagua Mwambe, Lakini Kwa Vile Siku Zote Chadema Huwa Hawajitambui, Sijui Sasa Kama Wanajitambua, Hebu na Tusubiri Tuone!".
Hitimisho
Kwanini Mwambe na Sio Mhowe?.
Nanalizia kwa kusisitiza, Mhe. Mbowe hana tatizo lolote bali amefikia point of his optimum, mwisho wa uwezo wake, he can not do anything more than what he can or what he did due to over staying na kuwa over saturated to the point of saturated solution that can take no more that it can.
Politics is science, inafuata principles of political science, Mbowe alipokea Chadema kikiwa ni chama cha kiharakati, alipaswa aki transform kugeuka chama tawala in waiting. Serikali Kivuli ni government in waiting, ilipaswa kila Waziri akifanya jambo fulani, waziri kivuli ana counters kwa kueleza how wrong the government is wangekuwa Chadema wangefanya nini tofauti but serikali kivuli ya Chadema utaisikia tuu Bungeni but its like it doesn't exist nje ya Bunge.
Namfahamu vizuri Mwambe, huyu sio mwanaharakati ni strategist, baada ya Chadema kumpoteza Prof. Kitila Mkumbo, na ZZK, kiukweli kabisa Chadema is totally empty in terms of strategists, hivyo Mwambe ata i transform Chadema kutoka chama cha kiharakati kukigeuza chama tawala in waiting. Japo umaarufu wa Chadema ni ule uanaharakati wake, chama cha kiharakati kazi yake ni harakati tuu, hakiwezi kwenda Ikulu unless na sisi tufanyie majaribio ikulu yetu!.
You can just imagine kama Chadema hii tunayoiona sasa ndio ingepewa nchi ile 2015, hali ingekuwaje?!, si ingekuwa disastrous, thanks God angalizo hili, limesaidia
Wanabodi, Preamble: Chadema ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo jina tuu, ila uendeshaji wake ni wa kidikteta wa hali ya juu!. Katiba yake inavipengele vya kidikteta vinavyokwenda kinyume cha katiba ya nchi!, hii thread ni ya swali tuu, Hivi Chadema ilivyo, bado haijakabidhiwa nchi, inatoa...
Namalizia Kwa Lile Lile Swali la Msingi, Kama Chadema Sasa Wanajitambua, na Wanajua Wanataka Nini, Watamchagua Mwambe, Lakini Kwa Vile Siku Zote Chadema Huwa Hawajitambui!...Then Watamchagua Tena Mhe. Mbowe. Swali Jee Chadema Sasa Wanajitambua na Kujua Wanataka Nini?Au Bado Hawajimbui?,
Tusubiri Tuone!.
Nawatakia Wana Chadema, Uchaguzi Mwema wa Kuchagua Ama Kuendelea Kuishi Ama Kifo!.
Paskali