Nailaumu CHADEMA kuwa hawajui wanataka nini

Tundu Lisu ana ujuzi,uthubutu,na ujasiri,ila amepungukiwa na kitu kimoja kikubwa sana- Hana hekma!

Anafaa kuwa chini ya mtu au kupewa madaraka akiwa mzee wa miaka 60
Pascal Mayalla ni kweli chadema inahitaji fresh blood ila sio Mwambe,CHADEMA inahitaji fresh blood kama Tundu Lisu ila walichokifanya sio kibaya ni maandalizi ya Tundu lisu kuongoza jahazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu usipoteze muda wako na huyo Pascal bali kumbuka maneno ya Mbowe kuwa uchaguzi huu Rushwa imekuwa tatizo sana na moja wa hao waliokula anaweza kuwa yeye Pascal au huyo anayepigiwa debe Mr Mwambe...binafsi Mwambe ni very Jr kubeba mikoba ya Mwenyekiti Taifa kama sio kuua chama, huyo bwana hata alikotokea wanachama wengi hawamjui ila pesa ya kununua wanachama anayo kapata wapi pesa hiyo kama hajapewa na aliyemlipa Pascal? huyu Mayalla anadai eti Mbowe kakaa sana kwenye uongozi bila kuleta maendeleo na sasa basi panahitajika badiliko lakini mtu huyohuyo anashindwa kusema kuwa CCM imekaa sana kwenye uongozi mpaka sasa inashindwa kumlipa hata mkulima wa Korosho, kumbe kweli mchawi hana usiku wala mchana
 
Mkuu Mayala umegusa ninapo pataka naki kwenye mtizamo kuna Jambo nataka kuweka.

Lolote kati ya mawili haya litakiimarisha chama; mosi iwapo wajumbe kwa utashi wao tu pasi kushawishiwa wakamwambia iwa sauti ya kimya kimya Mfalme muda wa kupumzika umefika.

Na pili iwapo Mbowe, aliamua kufuata taratibu zote za kujaza na kurudisha fomu, ili ionekane namna demokrasia ilivyo tamalaki ndani ya chama na ndio maana wajumbe wakamchagua Mwambe na ulimwengu ukawaelewa hivyo itakua ni milage kubwa sana kwa chama.

CHAMA KITAIMARIKAJE?
Kwanza watakua wamefanikiwa kufanya demage control kwa yale aliyoyasema Prof. Safari na Mh. Waziri Mkuu mstaafu Tuluway Sumaye.

Pili chama rasmi kitaifikirisha upya jamii juu ya community pendwa ya wachagga, Jamii itafuta ule unadharia wa Kuuwawa kwa Chacha Wangwe na kutimuliwa mbali wale mapacha watatu ZITTO, SAMSON NA PROF. MKUMBO.

Muda ni rafiki adhimu hasa katika siasa za nchi hii.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal watu wazima hawadanganyani mimi nakujua na wewe unanijua ila sema tu sivizuri kuanza kutambulishana, wewe umeamua kuwa verified user sawa ila tukikutana tunafahamiana vizuri tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal watu wazima hawadanganyani mimi nakujua na wewe unanijua ila sema tu sivizuri kuanza kutambulishana, wewe umeamua kuwa verified user sawa ila tukikutana tunafahamiana vizuri tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Mmawia kwanza nakubaliana na wewe kuwa kuna wana jf tunajuana in real names na tunajuana kuwa wote ni wana jf lakini hatujuani nani anatumia pen name gani, mimi mwenyewe my two kids are jf members and I don't know the names they use, hivyo inawezekana kabisa mimi na wewe tunajuana in reality, hivyo ningekuomba kuwa mkweli na muwazi kuhusu mimi, jee unavyo nijua in reality mimi nina chama chochote?.
P
 
Tundu Lisu ana ujuzi,uthubutu,na ujasiri,ila amepungukiwa na kitu kimoja kikubwa sana- Hana hekma!

Anafaa kuwa chini ya mtu au kupewa madaraka akiwa mzee wa miaka 60

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Kibaravumbi, naunga mkono hoja, kuna kitu kumhusu Lissu nami nilikisema hapa
P
 
Nimecheka sana mkuu Pascal
Sent using Jamii Forums mobile app
 
ulipoanza kumsiktikia kitla mkumbo kuondoka huu uzi nimeupunguza uzito, hivi pandikizi litafanya kazi kwa bidii?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Ndumbayeye, binadamu tunatofautiana uwezo na uwezo, mwingine ni mzuri katika kupanga mikakati, mwingine ni mzuri kwa kusema sana, mwingine kwa kuhutubia, mwingine kwa ushawishi etc, na ili kufanikiwa lazima hawa watu wenye uwezo tofauti to work as a team. Chadema ilikuwa na team nzuri, mfano Zitto ana very big convincing power, JJ.Mnyika ni researcher mzuri kujimba data, Lissu ni very powerful speaker, Prof. Kitila Mkumbo ni good strategist, team ya Chadema ilikuwa ikikiwasha kinawaka kama ile list ya mafisadi ya Mwembe Yanga au Moto wa Buzwagi Bungeni. Baada ya kumtimua Zitto, JJ.Mnyika now is nothing, baada ya kumtimua Prof. Kitila Mkumbo, kwa upande wa strategies Chadema is zero kwasababu hamna mtu kama Zitto wala Kitila na Zitto kule kwake pia he is nothing kwasababu kuna viungo hana.

Usidharau mtu, mimi kwangu hadi mfagizi ni muhimu na home hadi beki tatu ni muhimu, tena ma beki tatu wanaokoaga majahazi usipime ila watu hawapendi tuu kufunguka kama ambayo jf tunavyo isaidia sana serikali hii ya Magufuli lakini hatutajwi na badala yake ni serikali kutufungulia mlolongo wa makesi, na sisi individual members tunaojulikana ni wana jf, cha moto tunakipata kwa vibano kwenye shughuli zetu
P
 
@PascalMayalla Rudi kusoma hii comment ya jamaa ina ukweli mtupu

Kabla ya kuandika hili bandiko lako ungefanyia assessment haya aliosema huyu jamaa hapo Juu[emoji115]

Ungekuja na Uzi wa solution kuhusu aliyosema jamaa huyo then ndo ungeleta bandiko hilo the justification ingekuwa real

Otherwise unaowaonea chadema kwa muktadha wa Sasa wa kisiasa just call them political survivors .

Acheni wafanye wanachoona wao ni sahihi kwa wakati huu .

Pascal Mayalla the prophet of doom .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Decling stage inaelekezwa kwa mbowe tu mbona haielekezwi kwa ccm 58 yrs in abject poverty? Acheni unafiki
 
Mwambe, kwenye siasa za nchi hii zinazoendelea ni vigumu kupata nafasi ya juu kiasi hicho - angejaribu kwenye kanda lkn taifa ni kuongeza cv tu

Kwetu sisi CCM Mbowe ni bora kuliko akina lisu
 
Wakati huo hukuwa na price tag
 
Pasco, ninakuiheshimu sana na wewe ni moja ya role model wangu, ila sasa umeanza kuwa mnafiki na muongo mkubwa. Kwanini?

CHADEMA kitakufa sio sababu ya uongozi mbovu ni kwa sababu hakuna FAIR GROUND.

CHADEMA ikifa ni hasara kubwa kwa Taifa sio Mbowe wala Lisu. Kumbuka wakati wa kudai katiba mpya kuna wana CCM walipinga ila sasa wanaugulia maumivu makali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Do or die

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu Paskali,
Baada ya kusoma bandiko lako hili, ndio umedhihirisha zaidi tuhuma dhidi yako kwamba kuna kitu unatafuta kutoka utawala wa awamu ya tano. niseme ukweli tu kwamba bandiko lako HALINA VIWANGO.
Aina ya hoja uliyojenga, kuwaambia CHADEMA wamchague fulani na fulani wamuache, ni hoja ya hatari ambayo inatakiwa mtu akanyage kwa tahadhari kubwa. kwa kawaida watu waungwana huwa hawatoi kabisa ushauri wa aina hiyo. hata kama wanataka kusema mchagueni fulani, hawatasema hivyo moja kwa moja, bali watajenga hoja zenye nguvu na madhubuti, ili kuwashawishi wapiga kura, kwa hoja. na hata mtu anaposoma hoja kama hizo, huweza kucheka hapa na pale, lakini hasa ataheshimu mchango wako.

Sasa basi, kwa kuwa umeamua kuandika hivyo ulivyoandika, kuna njia ambazo ungeweza kutumia angalau watu wakakuelewa. unasema Mbowe amefikia kikomo katika utendaji wake. kwa hoja zipi? unasema chama kinakufa, je ni kweli kinakufa au ni mazingira ya kisiasa ya sasa hivi yalivyo?

Ukiangalia kihistoria, CCM na serikali yake huwa wana-target chama kikuu cha upinzani. Ilikuwa hivyo kwa NCCR, ambayo baada ya Lyatonga Mrema kujiunga nacho, kiliibuka kuwa chama kikubwa sana cha upinzani, na kutoa wabunge machachari, kama akina Masumbuko Lamwai. NCCR ilipigwa vita hadi ikawa dhaifu kama ilivyo leo. ikaibuka CUF. Hii nayo ilitamba bara na visiwani, hapo zaidi visiwani. nayo ikawa targeted. utasikia oohh, chama cha waislamu, nk. hatimaye kwa kumtumia Lipumba, CUF imeondoka rasmi katika orodha ya vyama vikuu vya upinzani, na bila shaka uchaguzi wa 2020 utahitimisha rasmi safari yao. ikaja CHADEMA. kule mwanzo serikali za CCM wala hazikuwa na shida na CHADEMA, ambao kwa mwaka 1995 na 2000 hawakusimamisha mgombea wa urais, bali walikuwa wanaunga mkono wagombea wa NCCR. CHADEMA walianza kusimamisha wagombea urais mwaka 2005 kwa kumsimamisha Mbowe mwenyewe. ilikuwa hapo CHADEMA ndiyo ikaanza kupaa. kila uchaguzi CHADEMA kimejiongozea idadi ya wabunge, madiwani nk. na hatimaye kuibuka kuwa chama kikuu cha upinzani. hapo ndipo serikali ya CCM imei-target CHADEMA. sasa hivi kelele zote zinaelelekezwa CHADEMA.

Mara kadhaa viongozi mbalimbali wametangaza kifo cha CHADEMA. walikuwepo akina Steven Wasira, na hatimaye Rais Magufuli mwenyewe ambaye aliahidi kuua vyama vyote vya upinzani kufikia 2020. Na katika wote hao, Magufuli ametumia mamlaka yake kwa kiasi kikubwa ili kuvikandamiza vyama vya upinzani. Kwa hiyo kwa kuweza kuhakikisha CHADEMA iko hai na inaweza kufanya chaguzi zake, na hata akina Cecil Mwambe wakagombea katika mazingira kama haya, ni jambo kubwa.

Unasema unamfahamu Mwambe. unamfahamu vipi? yaani tukuamini tu wewe kwamba madhali unamfahamu kwamba ni strategist mzuri, basi? kafanya nini mpaka hivi sasa? Mbowe tunamfahamu, mazuri yake na madhaifu yake. Mwambe je? Ulitakiwa uorodheshe yapi kayafanya, ili kuwashawishi wajumbe wa CHADEMA.

Hivyo kwa kutamka tu ulivyotamka, hujajitendea haki wewe mwenyewe kama mwanahabari mkongwe.

Lakini kuna hili la UANAHARAKATI. Hizi ni Propaganda za CCM. wanachora ramani chama cha siasa kinatakiwa kiwe vipi. Ebo! Hivi kwanza CCM ni chama cha siasa? kilishakufa siku nyingi mbona? ni kikundi tu fulani kinachotumia dola kutawala. hata wanaCCM wenyewe washajichokea. na ndio maana CCM inaweza kuendesha vioja kama huo unaoitwa uchaguzi wa serikali za mitaa. Na mwenyekiti wao anajipongeza kabisa akiwaambia HONGERENI KWA USHINDI!!!

Chama cha upinzani kinatakiwa kupambana muda wote. lakini tukumbuke pia kwamba nguvu za vyama vya upinzani zinatokana na utayari wa watanzania kuvitetea vyama hivi na kuvilinda. wakiwaachia viongozi tu siyo haki. CHADEMA hawana dola ya kuegemea, kama wanavyofanya CCM. wao wana support ya wananchi tu basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…