Wakuu
Binafsi huwa na Bet sana na bahati nzuri nimemuotea muhindi kama M 40
Na sasa nataka kubet kwenye kilimo
Mwaka huu naingia shambani kweli kweli sio utani, naingia FRONT na sio simu
Nakwenda kulima ekari 50 za alizeti MBUGANI kisha nikitoa naweka dengu
Eneo SINGIDA kwetu kabisa
Matumizi (makadirio ya juu kabisa) kwa ekari 50
[emoji117]Kukodi shamba m 2.5
[emoji117]Kulima shamba m 2.5
[emoji117]Kupanda m 1
[emoji117]Kupalilia shamba m 2.5
[emoji117]Mbegu lk 7
[emoji117]Uvunaji/upakiaji m 2
[emoji117]Mengineyo m 2
Jumla milion 13.2
Jumlisha hidden cost jumla iwe milioni 15
MAVUNO (makadirio ya chini)
Eka moja gunia 7 badala ya 15 za wataalamu
Ekari50 x Gunia 7
Jumla inakua gunia 350
Wastani gunia moja hutoa mafuta dumu 2 bei makadirio ya chini sh elf 50 kwa dumu( dumu linakwenda hadi laki+)
350 x 2 inakua dumu 700
Dumu700 x elf50 unapata Sh M35
Hapo nime assume mashudu yamelipia gharama ya ukanuaji
JUMUISHO
M35 -M15 = M20 Faida
DENGU
Ukitoa tu alizeti unavizia nvua za mwishoni kabisa unalima dengu shamba hilo hilo hulipi gharama za kukodi tena
[emoji117]Kulima m 2.5
[emoji117]Mbegu m 2
[emoji117]Kupanda lk 5
[emoji117]Madawa (emergency) m2
[emoji117]Kuvuna/kupakia 2m
[emoji117]Mengineyo m 1
Jumla m 10
Hidden cost m 2
Jumla m 12
MAUZO
Wastani gunia 4 kwa eka badala ya gunia 8 hadi 10 kwa eka za wataalamu
Ekari50 x Gunia 4 unapata gunia 200
Gunia la dengu lina wastani wa sh Laki 1
Laki 1 x gunia 200 unapata M 20
JUMUISHO
M20 - M12 = M8 Faida
FAIDA KUU (alizeti na dengu)
M20 +M8 = M28
NB
Nimeweka makadirio ya juu sana kwenye matumizi
Na nikaweka makadirio ya chini sana kwenye mavuno na bei
Dua zenu jamani
Ntaleta MREJESHO iwe nime Lost au nime Win