Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

Mkuu pambana ukishamaliza kamua kabisa unipe mafuta nikusadie kuyauza
 
Mleta mada kama uko serious njoo pm nna shamba Simanjiro ekari 15,000 nina ma trekta mawili. Mwaka jana nilianza Na ekari 100 za maharage tu. Mwaka huu nataka kuongeza mahindi, alizeti Na katarm. Njoo tuunganishe nguvu.
Hizo zote hazina visiki? Naweza ongezea trekta moja hapo. Au umemlenga mleta maada tu
 
Hizi kwa mawakala inauzwa 28000 hadi 30000. Kwa baadhi ya maeneo serikali imetoa kwa 7000 kwa vikundi vya vijana waliosajiliwa.

Kama unajitegemea, nenda kwa mawakala japo aina hii kdg n adimu ila ukiipata n bei hio kwa juu
Tupe kidogo kuhusu performance yake?
 
Ni kweli kabisa.
Binafsi sijawahi kusikia mtu amwvuna alizeti zaidi ya gunia 7 na nadhani hawa watu wa pembejeo wanatudanganya Ili wauze mbegu za za Hybrid.

Mimi nitakomaa tu na mbegu zangu za opv
Hapana Mkuu hawakudanganyi ila inategemea na ardhi unayolima na namna ya upandaji.Alizeti haipandwi Kama mahindi mkuu.
2. Kuna mbegu ukipanda shina moja linatoa matawi 20 na kila tawi Lina zaa hii waweza vuna gunia 15 -17 kwa ekari.
Halafu Kuna mbegu ukipanda shina moja Lina zaa Toto Moja tu! Sasa hiyo huwezi kupata gunia zaidi ya 7 kwa ekari.
 
Big up mkuu.Jiandae kisaikolojia pia, hasa kama utategemea mvua, maana sijaona bajeti ya kisima. au upo karibu na mto mkuu.
 
Hii nzuri, songa mbele na ndoto yako usikatishwe tamaa
 
Tupe kidogo kuhusu performance yake?
Inahimili sana shortage of rainfall so ni nzur sana kwa mikoa inayopata mvua chache kwa mwaka,

Kwa ekari moja yenye rutuba na iliyotunzwa vzr, inatoa gunia 15 hadi 20.
 
Hizo zote hazina visiki? Naweza ongezea trekta moja hapo. Au umemlenga mleta maada tu

Sehemu chache ni za kusafisha ila unakua na guarantee ya kulima miaka mingine bila gharama ya kukodisha
 
Utafanikiwa naona umejipanga na hujaweka makadirio ya juu nenda hapa mchawi bei tu bei zisipobadirika utapata faida tu.
 
Utatoa mlio kijana
 
Bei ya soya ikoje huko sokoni kwa sasa? Sio kutuambia tulime tu.
 
Kila lakheri mkuu. Naamini your to win.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…