Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

... Mkuu all the best ila zingatia taarifa za wataalamu hususan TMA wametabiri hali sio shwari sana msimu huu!
 
Mkuu kwanza umefanyaje ukamuotea muhindi aisee...maana mi ananipiga vibaya aisee. Hebu nisaidie ABC inbox mkuu
 
MREJESHO

Wakuu kwema
So far mkeka wangu wa kilimo cha Alizeti unakwenda vizuri sana baada ya zile ODDS kubwa na ngumu kutick
ODDS ngumu kabisa zilikua ni MVUA na PALIZI

SHAMBA EKARI 20
Mpaka sasa nimelima ekari 20 tu...... hii ni baada ya wadau mbali mbali kushauri ekari 50 is too risk ikiwa huna UZOEFU na ikizingatiwa mamlaka ya hali ya hewa ilitabiri mvua zitakua chache

MBEGU (ASA)
Baada ya mchakato wa kitaalamu nikashauriwa nitumie mbegu za Serikali ASA na nilinunua mfuko wa kilo 2 kwa sh 5,000 tu, nilipata mchongo huu kwakuwa nilinunua kwa wingi

Sijatumia MBOLEA yoyote wala sijatumia viatilifu vyovyote kwasababu nimelima MBUGANI aridhi imeshiba na Alizeti haishambuliwi sana na magonjwa

Leo hii nimemalizana na PALIZI na mimea inakwenda vizuri kwa sehemu kubwa

Mpaka sasa SIJAKUTANA na gharama yoyote ambayo imenishtua kwa maana ya kwamba labda ni gharama ambayo sikuifikiria au gharama kuwa kubwa zaidi ya nilivyo KADIRIA
Zaidi mbegu imenipa UNAFUU mkubwa sana, nilipanga kutumia Hysuan Kg 2 kwa 35,000
Lakini nimetumia ASA Kg 2 kwa sha 5,000 na nilinunua mifuko ya Kg2 mifuko 80, yaani eka moja kwa mifuko 4, hapo nime save karibu 2m...... Naishukuru sana serikali kwa hili 🙏🙏
Ingawaje sijajua ubora wake baada ya mavuno

Ntaleta tena Mrejesho baada ya KUVUNA
 

Attachments

  • 9F200835-D7EC-474C-9DE2-3A40AD983F06.jpeg
    27.1 KB · Views: 109
Hongera Mkuu
Umelimia mbuga ya Mvae au Merya ?
 
Mnaanza lini kuvuna huko,ni sehem gani hio??
 
Makunda sio!? Ile mbuga mwaka huu haijaaa maji?....
 
Hongera Sana Mkulima mwemzangu tuendelee kupambana
 
Mayu tunasubiri mrejeaho wa mavuno Kwa hekati,na wingi wa mafuta Kwa hiyo.mbegu.
Natumaini utakuwa mkweli Ili utufumbue macho!
Kuna Hadithi nyingi saana kwenye kilimo baada ya ujio wa Smartphone😁😁
 
Mayu mzee wa mikeka umetisha sana
hiyo ni shambani kwako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…