Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

Uzoefu binafsi.
Gunia la alizeti linatoa lita 15-20.
Mashudu kilo 35-45.
Eka 1 ni gunia 3 mpaka 7. Inategemea aina ya mbegu, mvua, kufukuza ndege.
Bei ya gunia la alizeti shambani 20000 mpaka 35000
Bei ya gunia la alizeti mjini inategemea na msimu na mashineni na mbegu uliyopanda.
Pia hujapiga gharama ya kuvuna na kusafirisha na stoo. Ndio maana wengi wanauzia shambani kutokana na gharama.

Matajiri wa kulima alizeti wapo Manyara, Singida, Dodoma (kongwa,kibaigwa, mbande), Kiteto na sehemu fulani inaitwa Matui huko ndio wanastoo (gunia 5000+) zao na mafuso na mascania yao. Wanapeleka alizeti viwanda vya Dodoma mjini (pyxus) na Mount Meru Singida.

Hizo hesabu ulizopiga 100% ni feki.

Nenda matui hapo manyara ukafanye utafiti utakuja na majibu. Kuna don mmoja wa alizeti yeye ana mascania ya kusomba alizeti kupeleka viwandani yeye analimaga kuanzia eka 800 mpaka buku. Halafu anauza alizeti yake kiwandani. Akimaliza anakuja anatangaza bei ya alizeti ya kununua. Mwaka huu alinunua gunia kwa 60000 mpaka 65000 kwa mbegu nzuri.
 
Shida sio jembe shida ni elimu ya kile unachokilima ujue kinataka nini na kwa mda gani ujue ni mda upi ni sahihi kulima mda upi hutakiwi kulima.

Lakini hata uwe na dhana za kisasa lakini huna elimu ya kutosha ya kile unachokilima utalia tu mwisho wa siku.
Mfano kilimo cha mahindi ili kiweze kukutoa unatakiwa ulime angalau ekari 100
 
Kila la kheri mkuu [emoji1431] Kama unataka mali utaipata shambani
 
kilimo cha kwenye makaratasi, halafu ukalime kwa kupiga simu muda kama huu mwakani utakuwa unawaza kujiua
Ni kweli. Na huyu jamaa kapiga hesabu 100% feki. Aende mwenyewe kufanya utafiti. Ama sivyo atapata tabu sana.
 
Ni wazo zuri sana maana kama ntapata idadi hiyo ya magunia basi shudu litakua jingi sana
Mkuu details hazipo sawa?

Mbona nimejitahidi sana kupandisha gharama na kushusha mavuno na mauzo kwa karibu nusu nusu?
Umejitahd lkn bado hesab zako haziendan na uhalisia kiviiiile, unless kama umezitoa google
 
Nami nimeelekezwa wanauzia Ofisi za kilimo kule karibu VETA Ila nami natarajia Leo ndo Ni lakini pia Kuna Pixus wapo kizota na chamwino Ikulu wanatoa mbengu free takutumia namba uwacheki
Mkuu mrejesho tafadhali
 
Uzoefu binafsi.
Gunia la alizeti linatoa lita 15-20.
Mashudu kilo 35-45.
Eka 1 ni gunia 3 mpaka 7. Inategemea aina ya mbegu, mvua, kufukuza ndege.
Bei ya gunia la alizeti shambani 20000 mpaka 35000
Bei ya gunia la alizeti mjini inategemea na msimu na mashineni na mbegu uliyopanda.
Pia hujapiga gharama ya kuvuna na kusafirisha na stoo. Ndio maana wengi wanauzia shambani kutokana na gharama.

Matajiri wa kulima alizeti wapo Manyara, Singida, Dodoma (kongwa,kibaigwa, mbande), Kiteto na sehemu fulani inaitwa Matui huko ndio wanastoo (gunia 5000+) zao na mafuso na mascania yao. Wanapeleka alizeti viwanda vya Dodoma mjini (pyxus) na Mount Meru Singida.

Hizo hesabu ulizopiga 100% ni feki.

Nenda matui hapo manyara ukafanye utafiti utakuja na majibu. Kuna don mmoja wa alizeti yeye ana mascania ya kusomba alizeti kupeleka viwandani yeye analimaga kuanzia eka 800 mpaka buku. Halafu anauza alizeti yake kiwandani. Akimaliza anakuja anatangaza bei ya alizeti ya kununua. Mwaka huu alinunua gunia kwa 60000 mpaka 65000 kwa mbegu nzuri.

Mkuu ulitumia mbegu gani inayotoa lita 15 - 20 kwa gunia?
Na ujazo wa gunia ni debe ngapi? 6 au 8?
Hapo maana yake gunia moja ni sawa na dumu moja la lita 20

Najua wingi wa mavuno unatokana pia na ubora wa aridhi, ulilima wapi mkuu?
Mi nalima kwenye mbuga na ipo vizuri sana kama nvua hazitakua nyingi
Gunia 3 - 7 sio wastani mzuri kama aridhi ipo vizuri

Stoo ipo ya kuhifadhi wastani wa gunia 500 ipo mkuu tena free, gharama ya kuvuna kupiga na kupakia hadi stoo nimeiweka hapo

Mchango wako umenifanya nitafiti tena kwa kina wastani wa gunia ngapi kwa ekari
Na wastani wa mafuta kiasi gani kwa gunia
Hapa ndio pakujua kama inalipa au la

Kuuza mbegu ni hasara zaidi bora kukamua mafuta
 
Umejitahd lkn bado hesab zako haziendan na uhalisia kiviiiile, unless kama umezitoa google

Mkuu karibu changia uzoefu wako basi

Wastani wa gunia kwa ekari
Na wastani wa mafuta kwa dumu

Gharama sio tatizo
Tatizo ni kujua hiyo fomula hapo juu ndio tutajua kama inalipa au la
 
kilimo cha kwenye makaratasi, halafu ukalime kwa kupiga simu muda kama huu mwakani utakuwa unawaza kujiua

Kuna kumshauri mtu na kuna kumkatisha tamaa mtu

Huu wako ni ukatishaji tamaa mkuu
Kama unazuri la kuboresha basi changia
 
Mkuu ulitumia mbegu gani inayotoa lita 15 - 20 kwa gunia?
Na ujazo wa gunia ni debe ngapi? 6 au 8?
Hapo maana yake gunia moja ni sawa na dumu moja la lita 20

Najua wingi wa mavuno unatokana pia na ubora wa aridhi, ulilima wapi mkuu?
Mi nalima kwenye mbuga na ipo vizuri sana kama nvua hazitakua nyingi
Gunia 3 - 7 sio wastani mzuri kama aridhi ipo vizuri

Stoo ipo ya kuhifadhi wastani wa gunia 500 ipo mkuu tena free, gharama ya kuvuna kupiga na kupakia hadi stoo nimeiweka hapo

Mchango wako umenifanya nitafiti tena kwa kina wastani wa gunia ngapi kwa ekari
Na wastani wa mafuta kiasi gani kwa gunia
Hapa ndio pakujua kama inalipa au la

Kuuza mbegu ni hasara zaidi bora kukamua mafuta
Rudia utafiti upya. Kaulize wakulima wa alizeti wa maeneo unayolima angalau 10 usikie uzoefu wao. Hizi hesabu za karatasi usiziamini mkuu.

Ishu ya kukamua sio rahisi kama unavyodhani. Lazima ujue gharama, maswali na hesabu zifuatazo
1. Kusafirisha gunia toka stoo mpaka mashineni
2. Gharama za ushushaji na upakiaji
3. Gharama za ushuru wa halmashauri njiani
4. Gharama za kukamua kwenye mashine na kuchuja
5. Gharama za madumu
6. Je mashudu utayachukua mashineni au utayaacha
7. Usafiri wa kuyasafirisha madumu+mashudu kupeleka unapotaka
8. Je hayo mafuta unamuuzia nani? Je utauza mwenyewe au utaweka mtu? Je utauza kwa mbinu ipi?
Kwenye kulima makadirio ya eka gharama
1. Kukodi-
2. Kusafisha shamba-
3. Kulima shamba(mkono/trekta)-
4. Kupanda-
5. Bei ya mbegu kwa eka+
6. Kupalilia(mara moja au mbili)-
7. Kulinda ndege-
8. Kuvuna,kupiga,kupepeta,magunia-
9. Kusafirisha toka shamba mpaka stoo-
10. Kupakia na kushusha toka kwenye roli-
11. Usafiri wako wa mara kwa mara kwenda shambani-
12. Dharura-

Ukifanya utafiti upya, tena wa kina ndio utaelewa uhalisia. Usipige hesabu za makaratasi au mahesabu ya matikiti kwenye kilimo utalia mno. Fanya utafiti ukiwa umetulia bila muhaho.
Au lima kama eka 5 za utafiti kwanza wakati pesa umeziweka benki kwenye fixed deposit ya riba.
Nawasilisha.
 
Ni wazo zuri sana maana kama ntapata idadi hiyo ya magunia basi shudu litakua jingi sana
Mkuu details hazipo sawa?

Mbona nimejitahidi sana kupandisha gharama na kushusha mavuno na mauzo kwa karibu nusu nusu?
Ndugu yangu kupata gunia 7 kwa alizeti sio kitu rahisi.

Pia kumbuka kuna kipindi bei inakuwa chini ya 50k. Na kama utakua,ya mafuta si kila gunia litakupa lita 20.

Kea jinsi alizeti ilivyopanda bei Mwaka huu nahisi msimu ujao watu wengi watailima hivyo kupeleka soko kuanguka.

Ili alizeti ikupe pesa lazima uwe mvumilivu
Yaani uiweke stoo mpaka mwezi wa 11 au 12, utafurahi mwenyewe
 
Nami nimeelekezwa wanauzia Ofisi za kilimo kule karibu VETA Ila nami natarajia Leo ndo Ni lakini pia Kuna Pixus wapo kizota na chamwino Ikulu wanatoa mbengu free takutumia namba uwacheki
Weka namba wote tufaidi mkuu
 
Mkuu ulitumia mbegu gani inayotoa lita 15 - 20 kwa gunia?
Na ujazo wa gunia ni debe ngapi? 6 au 8?
Hapo maana yake gunia moja ni sawa na dumu moja la lita 20

Najua wingi wa mavuno unatokana pia na ubora wa aridhi, ulilima wapi mkuu?
Mi nalima kwenye mbuga na ipo vizuri sana kama nvua hazitakua nyingi
Gunia 3 - 7 sio wastani mzuri kama aridhi ipo vizuri

Stoo ipo ya kuhifadhi wastani wa gunia 500 ipo mkuu tena free, gharama ya kuvuna kupiga na kupakia hadi stoo nimeiweka hapo

Mchango wako umenifanya nitafiti tena kwa kina wastani wa gunia ngapi kwa ekari
Na wastani wa mafuta kiasi gani kwa gunia
Hapa ndio pakujua kama inalipa au la

Kuuza mbegu ni hasara zaidi bora kukamua mafuta
Pigia wastani wa gunia 4 hadi 5 tuseme hapo ndio imekubali.

Mwaka jana nililima alizeti za kienyeji lakini nilivuna Mavuno sawa na walio lima hybrid.

Nilikuwa najaza gunia zenye wastani wa kilo 65-71 ambazo zilikuwa zinatoa lita 19-22
 
Back
Top Bottom