Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

Tatizo lipo kwenye rutuba,aridh inayolimwa mahindi inafaa kulima Mahindi na Alizeti,Ila Kuna aridhi ya kichanga Ile tunalimaga Alizeti tu, mahindi haistawishi.
Japo kitunguu maji nae anakimbiza Sana kwa singida
Mkuu vipi kilimo cha alizeti Kwa mikoa yenye mvuà nyingi kama nyanda za juu kusini ....je inastawi vizuri na mavuno yanakuaje?
 
Uzoefu binafsi.
Gunia la alizeti linatoa lita 15-20.
Mashudu kilo 35-45.
Eka 1 ni gunia 3 mpaka 7. Inategemea aina ya mbegu, mvua, kufukuza ndege.
Bei ya gunia la alizeti shambani 20000 mpaka 35000
Bei ya gunia la alizeti mjini inategemea na msimu na mashineni na mbegu uliyopanda.
Pia hujapiga gharama ya kuvuna na kusafirisha na stoo. Ndio maana wengi wanauzia shambani kutokana na gharama.

Matajiri wa kulima alizeti wapo Manyara, Singida, Dodoma (kongwa,kibaigwa, mbande), Kiteto na sehemu fulani inaitwa Matui huko ndio wanastoo (gunia 5000+) zao na mafuso na mascania yao. Wanapeleka alizeti viwanda vya Dodoma mjini (pyxus) na Mount Meru Singida.

Hizo hesabu ulizopiga 100% ni feki.

Nenda matui hapo manyara ukafanye utafiti utakuja na majibu. Kuna don mmoja wa alizeti yeye ana mascania ya kusomba alizeti kupeleka viwandani yeye analimaga kuanzia eka 800 mpaka buku. Halafu anauza alizeti yake kiwandani. Akimaliza anakuja anatangaza bei ya alizeti ya kununua. Mwaka huu alinunua gunia kwa 60000 mpaka 65000 kwa mbegu nzuri.
Kufukuza ndega huwa ni kwa muda gani kabla ya kuvuna?
 
How comes shambani bei ya gunia moja ni 20k - 35k ila huyo don ananunua kwa 60k - 65k?
 
Ndugu yangu kupata gunia 7 kwa alizeti sio kitu rahisi.

Pia kumbuka kuna kipindi bei inakuwa chini ya 50k. Na kama utakua,ya mafuta si kila gunia litakupa lita 20.

Kea jinsi alizeti ilivyopanda bei Mwaka huu nahisi msimu ujao watu wengi watailima hivyo kupeleka soko kuanguka.

Ili alizeti ikupe pesa lazima uwe mvumilivu
Yaani uiweke stoo mpaka mwezi wa 11 au 12, utafurahi mwenyewe
Hivi utunzaji wa mbegu unahitaji dawa ya kuhifadhi?
 
Soma updates bandiko la kwanza mwishoni
Mkuu Mayu bandiko la kwanza hakuna updates kabisa,
km umeshaanza kuvuna au kusafirisha toka shambani na kupiga alizeti kwenye matubuvai
Member wa kwanza alikuambia hicho Kilimo chako kitakupa hasara bora hiyo pesa ungeiweka ukaja kununua Alizeti hata 65 elfu kwa gunia utapata faida kuliko kuipanda
wa pili akakuambia hicho Kilimo ni cha kwenye Makaratasi sawasawa na kile cha matikiti maji
Tupe mtejesho ili uwe Mwalimu wetu KILIMO CHA ALIZETI KINAKATA NA KUMFILISI MKULIMA
Ushuhuda ni mimi mwenyewe na jamaa yangu kalima eka 30 Kongwa mm eka 5
kwake tumevuna eka 10 gunia 9 juzi tu sasa tunaingia eka 15 labda
kwangu eka 5 hakuna dalili ni hasara tu hawa wenyeji wanaokodisha mashamba ni wabaya wanajua kila kitu na ukicheza nao ndio kuambulia mabua
WEKA MREJESHO UMEVUNA SASA UNAONA UTAPATA GUNIA NGAPI?
 
Mazao haya wewe fanya ununuzi tu, utatoka kama una mtaji nunua unachokiona kuliko kuexpect faida kubwa baadae uje kula mweleka ambao hautokuja kusahau maana huwezi kubet na pesa ukaweza. Na kilimo cha mvua hakiaminiki ukizingatia mwaka huu umeelezwa mvua sio ya kutosha.
MKUU BORA ulivyomueleza anunue mazao ya alizeti wanapovuna kuliko kulima
Hebu muulize kapata gunia ngapi?
 
Mkuu Mayu bandiko la kwanza hakuna updates kabisa,
km umeshaanza kuvuna au kusafirisha toka shambani na kupiga alizeti kwenye matubuvai
Member wa kwanza alikuambia hicho Kilimo chako kitakupa hasara bora hiyo pesa ungeiweka ukaja kununua Alizeti hata 65 elfu kwa gunia utapata faida kuliko kuipanda
wa pili akakuambia hicho Kilimo ni cha kwenye Makaratasi sawasawa na kile cha matikiti maji
Tupe mtejesho ili uwe Mwalimu wetu KILIMO CHA ALIZETI KINAKATA NA KUMFILISI MKULIMA
Ushuhuda ni mimi mwenyewe na jamaa yangu kalima eka 30 Kongwa mm eka 5
kwake tumevuna eka 10 gunia 9 juzi tu sasa tunaingia eka 15 labda
kwangu eka 5 hakuna dalili ni hasara tu hawa wenyeji wanaokodisha mashamba ni wabaya wanajua kila kitu na ukicheza nao ndio kuambulia mabua
WEKA MREJESHO UMEVUNA SASA UNAONA UTAPATA GUNIA NGAPI?
Mkuu UPDATES zipo mbona
Bado sijavuna....... LAZIMA nitaleta mrejesho hapa hapa kwenye uzi huu nikivuna tu

BTW huyo jamaa yake kuoata waatani wa chini ya gunia moja kwa ekari imenishtua sana......HOW?
Alizeti iliota vibaya? Au ilikua kawaida tu?
Maginjwa? Ukame? Au nini?
 
How comes shambani bei ya gunia moja ni 20k - 35k ila huyo don ananunua kwa 60k - 65k?
Inasemekana huyo Don alipata tenda ya kuuza alizeti kwenye viwanda vikubwa tz. Alikuwa ananunua Dodoma, Singida na Manyara, Na ni mtu mwenye pesa nyingi sana. Sababu za kununua kwa bei hiyo anajua yeye mwenyewe. Hiyo hesabu anaijua yeye mwenyewe. Ila mwaka huu alizeti inawezekana bei ikashuka hasa Singida maana wamelima sana. Ila sina uhakika juu ya bei.

Halafu bei inategemea na eneo ulilopo,muda unaouza, upatikanaji wa mafuta ya kula na hali ya mvua mwaka ilivyo. Mfano bei ya alizeti kibaigwa lazima iwe nzuri sana kwa sababu kuna mashine nyingi za kukamua mafuta ya alizeti.
 
Mkuu UPDATES zipo mbona
Bado sijavuna....... LAZIMA nitaleta mrejesho hapa hapa kwenye uzi huu nikivuna tu
BTW huyo jamaa yake kuoata waatani wa chini ya gunia moja kwa ekari imenishtua sana......HOW?
Alizeti iliota vibaya? Au ilikua kawaida tu?
Magonjwa? Ukame? Au nini?
umeishia mbali saha UPDATE zako hujaweka kupalilia ni mara ngapi umefanya.
Wenyeji wanaokodisha mashamba ni wabaya sana, wanakuuzia , wana kusafishia shamba, watalima na kupanda wenyewe, kwa tamaa zao watafanya wenyewe bila vibarua hivyo unatakiwa uwepo.
Ukichelwa kwenda wataomba hela ya palizi ya kwanza hadi ya 2 ukizubaa ya 3 na hawafanyi ukifika wakati watasema mvua nyingi weka palizi ya 3
nimeshtuka shamba lilishachoka kwa kulimwa miaka mingi Alizeti nikamwambia jamaa hawa wnasema utapata gunia 18 mpaka 20 kwa eka ni uongo mwisho ni gunia 7 au 8
Leo wanasema jua kali na ndege
huenda wamemkata nasubiri eka zilizo baki nitaweka mrejesho na hizo UPDATES zako tutapata jumisho km Alizeti ni zao la kumtoa mtu
 
Inasemekana huyo Don alipata tenda ya kuuza alizeti kwenye viwanda vikubwa tz. Alikuwa ananunua Dodoma, Singida na Manyara, Na ni mtu mwenye pesa nyingi sana. Sababu za kununua kwa bei hiyo anajua yeye mwenyewe. Hiyo hesabu anaijua yeye mwenyewe. Ila mwaka huu alizeti inawezekana bei ikashuka hasa Singida maana wamelima sana. Ila sina uhakika juu ya bei.

Halafu bei inategemea na eneo ulilopo,muda unaouza, upatikanaji wa mafuta ya kula na hali ya mvua mwaka ilivyo. Mfano bei ya alizeti kibaigwa lazima iwe nzuri sana kwa sababu kuna mashine nyingi za kukamua mafuta ya alizeti.
Hivi kuhifadhi alzeti unahitaji dawa za kuhifadhia kama mahindi?
 
MREJESHO WA GHARAMA so far

Kukodi Shamba ekari 20
20 x 30,00 = 600,00
Shamba lilikua safii

Kulima
20 x 40,000 = 800,000

Mbegu (ASA)
80 x 5,000 = 400,000

Kupanda
20 x 30,000 = 600,000

Palizi
20 x 50,000 = 1,000,000

Mengineyo
1,000,000

Jumla kuu kama 4,500,000

Mpaka sasa nimelaza 4.5M
Bado kuvuna, kupeta, na hifadhi
Makadirio gharama yote isizidi 6M

Mawazo makuu yanayo vuruga kichwa changu kwa sasa ni JE NITAPATA WASTANI WA GUNIA NGAPI KWA EKARI?
 
umeishia mbali saha UPDATE zako hujaweka kupalilia ni mara ngapi umefanya.
Wenyeji wanaokodisha mashamba ni wabaya sana, wanakuuzia , wana kusafishia shamba, watalima na kupanda wenyewe, kwa tamaa zao watafanya wenyewe bila vibarua hivyo unatakiwa uwepo.
Ukichelwa kwenda wataomba hela ya palizi ya kwanza hadi ya 2 ukizubaa ya 3 na hawafanyi ukifika wakati watasema mvua nyingi weka palizi ya 3
nimeshtuka shamba lilishachoka kwa kulimwa miaka mingi Alizeti nikamwambia jamaa hawa wnasema utapata gunia 18 mpaka 20 kwa eka ni uongo mwisho ni gunia 7 au 8
Leo wanasema jua kali na ndege
huenda wamemkata nasubiri eka zilizo baki nitaweka mrejesho na hizo UPDATES zako tutapata jumisho km Alizeti ni zao la kumtoa mtu
Mkuu nimeona post zako kwenye uzi huu na mwingine wa Alizeti ukilalamika sana kwamba kilimo hiki kina uongo mwingi nk
Kwanza ni kiri kilimo chochote au biashara yoyote ikiisha anza kushadadiwa na Motivation speakers basi huwa wanakua na uongo mwingi sana
Lakini pia baada ya uongo huo ukaenda shambani kwa kilimo cha kupiga simu ndio balaa kabisa

Simshauri mtu aliye ajiriwa na hana nafasi eti aende kijijini akakodishe shamba kisha aanze kuwa anatuma hela afanyiwe kazi..... lazima utaumizwa vibaya

Lakini pia maeneo ambayo ukulima wa kibiashara umechanganya sana kumewafanya wenyeji kuwa matapeli sana, wanachojali wao ni kukushawishi ukodi shamba lao, wapate hela ya kukodi, kusafisha, kulima, palizi, kuvuna, kuchunga ndege, kulinda na kutunza shamba nk nk....na mwisho watakula hela unazotuma na mazao wataiba kabla hujaja kuvuna.. Hawawezi kukupa uhalisia watakudanganya hata kama shamba ni bovu kiasi gani

Kilimo kinataka uende mwenyewe front na uwe na muda wa kutosha
Unakwenda mguu kwa mguu shambani kuona wanalimaje, palizi kuvuna nk nk sio kupiga simu au kwenda mara moja au mbili na kuchungulia na kuondoka

Binafsi nimekwenda kijijini kwetu Iramba nakujua vizuri sana
Nimesimamia kila kitu
Nimepanda kwa mstari sio kumwaga mbegu
Nimewasimamia palizi kisawa sawa hadi wananiona mnoko flani hivi

Kwa maelezo yako ni kama umetumia zaidi simu kulima mkuu lazima upigwe

Yaani huku wamelima wengi alizeti lakini ukifika shamba langu utaona tofauti kubwa sana kati ya shamba langu na mengine
Sio kama najisifu ila nimejaribu kufuata kanuni zote na angalau naona mwanga ingawa sijajua ntapata kiasi gani
 
Mkuu nimeona post zako kwenye uzi huu na mwingine wa Alizeti ukilalamika sana kwamba kilimo hiki kina uongo mwingi nk
Kwanza ni kiri kilimo chochote au biashara yoyote ikiisha anza kushadadiwa na Motivation speakers basi huwa wanakua na uongo mwingi sana
Lakini pia baada ya uongo huo ukaenda shambani kwa kilimo cha kupiga simu ndio balaa kabisa

Simshauri mtu aliye ajiriwa na hana nafasi eti aende kijijini akakodishe shamba kisha aanze kuwa anatuma hela afanyiwe kazi..... lazima utaumizwa vibaya

Lakini pia maeneo ambayo ukulima wa kibiashara umechanganya sana kumewafanya wenyeji kuwa matapeli sana, wanachojali wao ni kukushawishi ukodi shamba lao, wapate hela ya kukodi, kusafisha, kulima, palizi, kuvuna, kuchunga ndege, kulinda na kutunza shamba nk nk...... Hawawezi kukupa uhalisia watakudanganya hata kama shamba ni bovu kiasi gani

Kilimo kinataka uende mwenyewe front na uwe na muda wa kutosha
Unakwenda mguu kwa mguu shambani kuona wanalumaje, palizi kuvuna nk nk sio kupiga simu au kwenda mara moja au mbili na kuchungulia na kuondoka

Binafsi nimekwenda kijijini kwetu Iramba nakujua vizuri sana
Nimesimamia kila kitu
Nimepanda kwa mstari sio kumwaga mbegu
Nimewasimamia palizi kisawa sawa hadi wananiona mnoko flani hivi

Kwa maelezo yako ni kama umetumia zaidi simu kulima mkuu lazima upigwe

Yaani huku wamekima wengi alizeti lakini ukifika shamba langu utaona tofauti kubwa sana kati ya shamba langu na mengine
Sio kama najisifu ila nimejaribu kufuata kanuni zote na angalau naona mwanga ingawa sijajua ntapata kiasi gani
Mvua naona kama zinasuasua mkuu,jua ni kali..vip haliwezi kuathiri Alizet kwa sasa?
 
Kwa walio lima mwishoni alizeti ikiwa bado ndogo inaathirika mkuu
Lakini kama wakati mvua inakata alizeti ilikua imekua itaenda fresh tu athari kidogo sana

Ila mvua ikirudi mapema ikamwaga maji ya kutosha itapona
 
Back
Top Bottom