Naingiza milion 22 kwa mwezi kwa biashara ya kuuza Mapapai shambani

Tumia mbegu za kwetu sio za ulaya unafeli ndio maana hauuzi
Mbegu za asili OPV heirloom papai zinakuwa ndogo na zinaharibika haraka haziuzwi 3000 bei ya jumla. Labda supermarket.
Hazina bei kubwa.
Anayebisha aende hata kesho masoko yoyote makubwa ya matunda Dar.
Hapa hatuharibu biashara yako bali tunaweka taarifa sahihi watu wafanye decision sahihi kibiashara.
 
Utakuwa unaishi yombo au buza
Papai tsh 100
Yombo na Buza wananunua papai soko la Stereo Temeke.
Hakuna papai ya bei ndogo bei ya jumla chini ya 500 na hakuna ya bei kubwa kufikia 3000 mbegu za asili.
Wewe waite watu waje subscribe YouTube channel yako wajifunze kilimo lakini usiweke bei za uongo utaumiza watu kisaikolojia mapato yakiwa kinyume na matarajio.
 

Yeye mwenyewe siyo mkulima.

Angekuwa analima asingekuwa na muda wa kutafuta mia 5 humu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…