Nakuelewa ila unamtafuta mwenyewe kwa jitihada zako,ila kama hakupatikana basi endelea kuishi mpaka pale Mungu atakapo mleta mmiliki halali
Nasema hivyo kwasababu watu wema huwa Mungu ana namna yake ya kuwapa haki zao,kuna kisa kimoja enzi za nabii Mussa,nabii Mussa na bwana mmoja mja wa Mungu anaitwa hidhir,walienda sehemu wakakuta ukuta umeanguka,wakauinua
Kwakuwa bwana hidhir alipewa elimu ya ghaibu au kujua mambo yajayo,akamwambia nabii Mussa huu ukuta tumeusimamisha kwakuwa hapa chini kuna adhina ya watoto yatima wawili,tumeusimamisha ili wakija kuwa wakubwa waje watoe hadhina yao kwani baba yao alikuwa ni mtu mwema,kwahiyo Mungu akiamua hiyo haki irudi kwa wenyewe itarudi tu