Naishi kwenye Nyumba ya kupanga mwenye nyumba alifariki ghafla na ndugu hawaijui hii nyumba

Naishi kwenye Nyumba ya kupanga mwenye nyumba alifariki ghafla na ndugu hawaijui hii nyumba

Hii habar kama ni ya kweli,ningekuwa mimi kwanza ile hela ya kodi ningekuwa naiweka bank kana kwamba namlipa mwenye nyumba,huku nafanya jitihada za kumpata mmliki wa nyumba hiyo

Siku wakipatikana nawaambia nadaiwa miezi kadhaa na hela yenu ipo niliihifadhi,hakika utakuwa umetenda haki mbele ya Mungu wako,na kwa neema ya Mungu huenda hata kodi iliyopita wahusika wakakusamehe kwakuwa ungekuwa na uwezo wa kuwadhulumu lkn hukufanya hivyo

Ila vyovyote itakavyokuwa haki ya mtu huwa haipotei,ipo siku tu kwa namna usiyotarajia unajikuta wenyewe hawa hapa
Daah tatizo mkuu hapa mjini shida kuwatambua ndugu wanaweza kujitokeza matapeli sababu jamaa tulikutana nae bar akasema anajenga akimaliza Mimi nihamie kama mpangaji wake Nikalipia miezi 6 ndio mwezi wa 4 akafariki
 
Ni mabay sana basi watu hawajui tu,baba yetu naye alikuwa na mambo kama hayo,kuna mashamba na viwanja alidhulumiwa kwa kupenda usiri usiri

Binafsi sitakuja kufanya haya mambo,mimi ni nafsi mda wowote nipo safarini kwa mola wangu
Ndio hivyo
 
Wakuu naishi kwenye nyumba ya kupanga na familia yangu yenye vyumba vinne na Kila kitu quality kuanzia aluminum mpaka tiles nyumba ni nzuri sana mwenye nyumba alifariki ghafla mwezi wa 4 mpaka Leo mwezi wa 12 nakaa bure naona kama hii ni bahati kutoka Kwa mungu nyumba ya bure sababu nilisikia fununu ndugu wameshagawana Mali zake ila hii hawaijui hii nyumba alikua anafanya Siri sababu ni mpya imezinduliwa mwaka huu naomba muongozo jinsi ya kupata hati miliki ya hii nyumba wakuu
Unachekesha.. kwa hiyo unaaamini Mungu amekupa nyumba kirahisi hivyo?
 
Daah tatizo mkuu hapa mjini shida kuwatambua ndugu wanaweza kujitokeza matapeli sababu jamaa tukikutana nae bar akasema anajenga akimaliza Mimi nihamie kama mpangaji wake Nikalipia miezi 6 ndio mwezi wa 4 akafariki
Nakuelewa ila unamtafuta mwenyewe kwa jitihada zako,ila kama hakupatikana basi endelea kuishi mpaka pale Mungu atakapo mleta mmiliki halali

Nasema hivyo kwasababu watu wema huwa Mungu ana namna yake ya kuwapa haki zao,kuna kisa kimoja enzi za nabii Mussa,nabii Mussa na bwana mmoja mja wa Mungu anaitwa hidhir,walienda sehemu wakakuta ukuta umeanguka,wakauinua

Kwakuwa bwana hidhir alipewa elimu ya ghaibu au kujua mambo yajayo,akamwambia nabii Mussa huu ukuta tumeusimamisha kwakuwa hapa chini kuna adhina ya watoto yatima wawili,tumeusimamisha ili wakija kuwa wakubwa waje watoe hadhina yao kwani baba yao alikuwa ni mtu mwema,kwahiyo Mungu akiamua hiyo haki irudi kwa wenyewe itarudi tu
 
Endelea kuishi na kuitunza nyumba,suala la kuifanya kuwa mali yako haliko sahihi.
 
Nakuelewa ila unamtafuta mwenyewe kwa jitihada zako,ila kama hakupatikana basi endelea kuishi mpaka pale Mungu atakapo mleta mmiliki halali

Nasema hivyo kwasababu watu wema huwa Mungu ana namna yake ya kuwapa haki zao,kuna kisa kimoja enzi za nabii Mussa,nabii Mussa na bwana mmoja mja wa Mungu anaitwa hidhir,walienda sehemu wakakuta ukuta umeanguka,wakauinua

Kwakuwa bwana hidhir alipewa elimu ya ghaibu au kujua mambo yajayo,akamwambia nabii Mussa huu ukuta tumeusimamisha kwakuwa hapa chini kuna adhina ya watoto yatima wawili,tumeusimamisha ili wakija kuwa wakubwa waje watoe hadhina yao kwani baba yao alikuwa ni mtu mwema,kwahiyo Mungu akiamua hiyo haki irudi kwa wenyewe itarudi tu
Mpangaji ni dhahiri ameshaanza kupata tamaa juu ya kumiliki na si kwa ajili ya kutafuta familia yake, ama kwa hakika atakuja kuaibika vibaya maana kwa vyovyote kuna yule rafiki ambaye alimshirikisha atakuja kumuumbua, hati anajua katunza wapi zitapatikana tu
 
Piga namba ya mwenye nyumba huenda ipo hewa ijulishe familia yake dhuluma mbaya
 
Back
Top Bottom