Naishi na Mwanaume, tatizo nikimgusia suala la ndoa anadai nisubiri hayuko tayari kwa sasa

Naishi na Mwanaume, tatizo nikimgusia suala la ndoa anadai nisubiri hayuko tayari kwa sasa

Mpendwa kuna members wamekupa ushauri mzuri ila ninacho kiona kwako kwamba jamaa kwa kuwa unaishi nae pamoja una imani siku atakuoa na unajipa matumaini hewa ni chaguo lake kwa kuwa mnaishi pamoja hujiuilizi mpaka una mshauri unataka ndoa ya ubani jamaa kagoma endea kuvuta subra uvune MAJUTO

Sio kuvuna majuto pia nikimuacha hivi sasa namuonea huruma dunia watamcheka maana amejitoa sana kwangu zaidi ya sana nikisema ni mangapi mema na mabaya aliyonifanyia mema ni mengi mno

Miaka 3 sio mingi panapouhai nampa huo muda ili hata nikiamua maamuzi mengine nisipate lawama
 
Ujue kuna jambo haliko sawa kwako, au kuna kitabia unacho ambacho kinampa Mashaka kuhalalisha kwa kuogopa mkiingia kwenye ndoa hicho kitabia kitaleta matatizo yeye kukwambia hawezi das why anakusubirisha tu kila mtu anahisi may be you can change later
Hawa huruhusiwa kuoa hata wanne, hata akibadilika jamaa si ana shift equilibrium tu.
 
Hata sasa najuta lkn sasa nitafanyaje? Najuta kuwa nae sababu haoneshi msimamo kuwa anataka tufunge ndoa ye anataka tu ishu hivi hivi tu kesho tutaenda kujibu nn kwa mola wetu? Lakini hanielewi ni kama vile namlazimisha
haujui cha kufanya my dear?pole sana
 
Kwa muda mlioishi tayari ni Mme na Make na haki zote hata ikitokea jamaa akifa sasa wewe shida yako ni nini?

Hiyo ni kidunia imani yetu hairuhusu hicho kitu na tunaelekea kuwa wazazi sasa inabidi tukae kwenye mstari hamna anayejua siku yake ya kufa, ukianza na machache mema basi yanayofata yote huwa ni neema tu
 
Sio kuvuna majuto pia nikimuacha hivi sasa namuonea huruma dunia watamcheka maana amejitoa sana kwangu zaidi ya sana nikisema ni mangapi mema na mabaya aliyonifanyia mema ni mengi mno

Miaka 3 sio mingi panapouhai nampa huo muda ili hata nikiamua maamuzi mengine nisipate lawama
Aisee wewe wazazi wako wanajisikiaje unaishi na Mwanaume pasipo kuwa na ndoa unadhani Dunia haiwacheki kwa hiyo unaogopa lawama umeingia kwenye mahusiano huku unaangalia Walimwengu watasemaje eti unampa miaka mitatu na yeye anakupa miaka 30 ya kukuchunguza.
 
Aisee wewe wazazi wako wanajisikiaje unaishi na Mwanaume pasipo kuwa na ndoa unadhani Dunia haiwacheki kwa hiyo unaogopa lawama umeingia kwenye mahusiano huku unaangalia Walimwengu watasemaje eti unampa miaka mitatu na yeye anakupa miaka 30 ya kukuchunguza.

Sasa unataka nirudi nirudi nyumbani?? Au nisubirie hiyo miaka 30 ya kuchunguzwa? Mm siogopi walimwengu ndio maana nimeona miaka3 jinatosha kuamua nn cha kufanya
 
Habari zenu wanaJF

Waislam wenzangu A’alaykum (eid inanukia[emoji39])

Niko na mtu tuna miaka mitatu hadi sasa tumepitia changamoto nyingi furaha na huzuni, kiukweli ni mtu ambaye hajawahi kuniacha hata hatua moja.

Swala lililonileta kwenu.

Huyu mtu ni muislam mwenzangu hamna changamoto zingine zozote isipokua kwenye swala la sisi kuhalalisha anakua mgumu mno (ndoa) ukimwambia tu basi tuhalalishe ni yuko muwazi yeye kwasasa hataki.

Huduma zote anatoa kuanzia matumizi (pesa) na huduma za chumbani[emoji3059][emoji3059] hajaoa, tunaishi wote. Shida ni hiyo tu hataki tuhalalishe ndugu zangu nifanyaje na kuachana nae siwezi japokua mwenyewe alinambia kama naona ananichelewesha basi anipe space ndani ya muda flani ikiwa bado sijaipata hiyo ndoa turudiane.

Hata funga yangu naona haiswihi kabisa maana tunaishi wote then tunafunga eti. Kwenye kila kitu mnakubaliana ila swala la ndoa hapo hataki anasema nivumilie.

Simuelewi! Au ana miiko[emoji848] Niko hoves nimechoka kuzini

mnaishi nae au kila mtu ana kwake ?

kama mnaishi pamoja hiyo ni ndoa labda kama unataka harusi tu to presitage reason

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama umejiridhisha anafaa kua mumeo jambo lako mkabidhi mungu atakufanyia wepesi haraka sana, hapa wengi watakuvunja moyo bt uhalisia wa hitaji lako unaujua wewe.

Ni kweli

Yani wanaona kuachana ni rahisi tu tena kwa mtu ambaye mambo mengi mnaendana na amekufanyia makubwa

Nimemuachia Mungu hopeful atatufikisha kwenye ndoa ya halali

Nimempa miaka3 tu panapomajaaliwa


Threads nyingi humu watu wanalalamika mara hivi mara vile watu wanachangamoto kibao za mapenzi mara nguvu za kiume sasa huyu kila kitu kiko biyee jamani
 
Back
Top Bottom