Pisi kali
JF-Expert Member
- Dec 31, 2019
- 1,234
- 2,535
- Thread starter
- #41
Mwanaume alazimishiwi kuoa.
Kuna vitu vitatu vinachangia mwanaume aoe na vyote ni MUHIMU sana
1. Hali ya maisha yake
Sasa hapa kipimo anacho mwenyewe kichwani.Yeye ndo anajua kwamba kwa uwezo huu wa kifedha naweza kumudu familia na sio wewe jinsi unavyompimia.
2. Mwanamke sahihi
Unaweza kuwa na mwanaume ht miaka 5 na usiwe sahihi niamini mimi kwa hili. Wanaume hatupimi ubora wa penzi kwa miaka tuliyodumu na mwanamke bali kwa ubora wa penzi hasa kwenye ishu ya ku maintain heshima yako kwake na usaliti.Unaweza kudumu nae ht miaka 8 ila km ulishawahi msaliti au mdharau jua ndoa inaweza isiwepo pamoja na miaka yenu 50 ya mahusiano
3. Umri na Utayari wa kuoa
Km hatupo tyr uwaga hatupo tayari tu.Haijalishi nina mwanamke sahihi na nina uwezo wa kumuhudumia.SIPO tayari kuvamia stress za ndoa.
Swali langu ni moja tu na ujijibu mwenyewe.Mpaka mkafikia kukaa pamoja nani hasa alitaka???Usigekuwa ni mzigo hapo hlf hujijui.Wanaume tuna huruma ni kazi kumfukuza mwanamke aliyehamia ht km hatujapenda kbs.
Mwisho kuanzia leo usizungumzie kuhusu kuolewa yaani leo ndo iwe mwisho. Pili Km huwezi kuacha kuzungumza kuhusu ndoa basi fanya jaribio kuu la kujua km wewe ni wa kuolewa nae au si😵ndoka hapo nyumbani rudi kwenu na sababu iwe ungependa uishi na mwanaume aliyekuoa kwahiyo km hayupo tayari basi unarudi kwenu mpk atakapokuwa tyr ila jiandae kujua ukweli halisi why hataki kuoa na ukweli uwaga mchungu.
Kimaisha yuko vizuri tu na mimi wala sio tegemezi kwake kila mtu anakazi zake (tunasaidiana)
Usahihi (hapo anajua yeye sasa maybe ameona mimi sio sahihi kwake)
Umri ana 35 mimi niko na 25yrs, naona hapo kwenye utayari wa kuoa kwake yeye mwenzangu bado
Kuishi pamoja, alinikuta najitegemea na yeye alikua anajitegemea, mawazo yake akasema tutafute nyumba kubwa tuishi pamoja hatukua na muda mrefu tangu tuanze mahusiano almost a month tu hivj, so kuanzia hapo hadi sasa tunaishi pamoja mkoa x
Kuzungumzia ndoa
Nimeacha
Ila as wapenzi ni kitu ambacho naona kinaniumiza na yeye ukitaka akose raha basi zungumzia kuhusu ndoa siku nzima atashinda hana furaha kwahiyo kauli yangu ya mwisho nilimwambia sitozungumzia tena kuhusu ndoa ye mwenyewe akiona sasa yuko tayari sawa
Ila ndani kwa ndani naumia sana, kuna leo na kesho hatuijui kesho yetu na bado tunazaa binafsi sipendi lakini sasa sina uwezo wa kulizuia hilo[emoji17][emoji17] sitaki hata sherehe nimemwambia tuhalalishe tu hata watoto wae wa ndani ya ndoa na tuwe tumekamilisha angalau nusu ya dini inavyotaka