Naiwaza kesho ya John Mrema, Yericko Nyerere na Kigaila

Naiwaza kesho ya John Mrema, Yericko Nyerere na Kigaila

Wallah Lissu atasamehe wote lakini si Yericko ama Ntobi.
Inavyoelekea labda hatujui dhana iliyobebwa na Neno "msamaha" au "kusamehe"

Kusamehe au Msamaha maana yake ni kumtamngazia kwa kauli dhabiti yule aliyekutenda
jambo baya kwa kumwambia "NIMEKUSAMEHE", sina kinyongo wala chuki na wewe...

Kusamehe haina maana kuwa ni lazima tufanye kazi pamoja tena Mimi na wewe. Tutasameheana lakini pia si ajabu hata kidogo kama kila mmoja wetu ataelekea upande tofauti....

Ndo kusema kuwa, kusamehe wala siyo shida na siyo jambo gumu kivile...

Lakini tukumbuke kuwa kila kosa tunalowatendea wengine Lina gharama yake ya kulipia. Moja ya gharama hiyo ni KUPOTEZA KUAMINIKA NA WATU MUHIMU...

Itakugharimu muda na nguvu nyingi kurejesha na kujenga upya uaminifu wako kwa watu...!

Baada ya kutamka msamaha, hatua ya pili ni kutoyapa nafasi hayo mabaya uliyotendewa na mtu huyo kiasi cha kutawala na kuendelea kuumiza moyo na nafsi yako usiku na mchana..

Ndiyo Kuna ule msemo wa "SAMEHE na SAHAU...."

Msamaha au kusamehe mara nyingi una faida zaidi kwa aliyetendwa kuliko aliyetenda.

Ndo kusema kwamba, Tundu Lissu ameshatamka tayari kuwa, hana kisasi wala chuki na mtu awaye yeyote. Kusema kutukanwa matusi au kusemewa maneno mabaya na mtu asiyejua lolote huwa hakumnyimi usingizi kabisa...

Hizi ni kauli za mtu asiyebeba visasi, chuki na kinyongo dhidi ya wanaomtendea mabaya. Hii ni roho ya Mungu wa mbinguni mwenyewe..
 
Ntobi na yerico ni WAPUMBAVÜ

Yes watasamahewa lakini wasahau kuaminiwa
 
Sorry jinsia yako? Unawaza wanaume kweli.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom