Najihisi kama muuaji ila inabidi nifanye

Maskini unaenda kuua Rais wa awamu ya 20, please don't do that!
 
Dunia haujawahi kua fair. Wenzako wanakesha wakiomba wapate mtoto ww unaomba mtoto auwawe salama. Eeh Mola mlete huyo mtoto nimlee.
 
Yani tukuombeee wakati unaenda kuua😬😬, aiseee.
Damn!
 
Unatuchosha mkuu, mosi wewe ni mtu,ulianzia kama mtu, kwa muktadha huo kiumbe kilichopo ndani ya mama mjamzito ni mtu pia ,


Hata mimi mnanichosha pia kwa kutokunielewa; labda nibadilishe tune na hoja iwe hivi:- je kutoa mimba (zygote) kutoka kwa mama mjamzito ni sawa na kuua MTU aliyekuwa hai???--- hii hasa ndiyo mada.

Tumbo la mama ni sawa na kiwanda cha kutengeneza bidhaa, bidhaa ikishaundwa na kukamilika na kukidhi viwango hapo inapata sifa ya kuwa bidhaa kamili, sasa utasemaje mimba iliyotolewa ambayo sio KAMILI IWE NI MTU, Kwani MTU ni nini???---Tafuta definition ya mtu kwanza ndipo uje useme mimba ni MTU.

Maana ya independence in this regard mfano wake ni huu:- Mama mjamzito kwa bahati mbaya akifa na ujauzito je huo ujauzito nao utabaki kuwa hai???, na anapozikwa je husemwa wamezikwa watu wawili au huwa anapasuliwa halafu mimba inazikwa peke yake na mama peke yake???--- nauliza maswali hayo ili uvute fikra zako kwa ukaribu, halafu tugeuze sarafu upande wa pili; kama mimba itakufa na ikatoka (miss carriage) je hiyo mimba itazikwa kwa taratibu zote za mazishi kama anavyokufa mtu independent??, je mbeba mimba naye anaweza kufa katika hali ya kawaida baada ya misscarriage???

kama ilivyo kumpiga mtu labda risasi ni mauaji hivyo hivyo kutoa mimba ni mauaji pia,sababu wote ni watu wanaouwawa,


Ukimpiga mtu risasi na akafa sio sawa na kuipiga mimba risasi, hiyo itasemwa umempiga mjamzito risasi au mjamzito katolewa mimba yake kwa case hiyo mimba inakuwa ni part ya mwili wa mbeba mimba, na hiyo huwezi kukanusha, huwezi kuitaja mimba bila kumtaja mbebaji na huwezi kutoa mimba hewani ni lazima itolewe kutoka kwa mbebaji.

Nataka andiko kutoka kwenye vitabu vya dini linalosema kutoa mimba ni sawa na kuua mtu, au Mungu alisahau kuleta andiko au hakujua kwamba utoaji wa mimba utakuwepo duniani??



Najua kwamba ili mimba itunge ni lazima sperms zikutane na yai la mama, mimi nilikuwa namjibu mtu mmoja aliyeniuliza kama mimi ningetolewa nikingali mimba ingekuwaje ndipo nikampa mfano wa Sperms za nduguze walioachwa kipindi yeye akiingia ndani ya yai ili aje duniani kama Mtu, hapo tofautisha kati ya Mtu na Zygote.

(Find the difference between man and Zygote.)


Ninaposema independence maana yangu ni independence katika 1---Chakula nje ya womb,2-- Hewa nje ya Womb, 3--- kujitambua nje ya womb, 4--- Hisia nje ya womb nk, hapo sasa huyo ndiye Mtu ambaye ukimuua unayo hatia hata siku ya kiyama atasimama kutoa ushahidi kwanini ulimuua, siku hiyo ya Qiyama naye atakuwa na daraja kama mtu, je siku ya Qiyama mimba zilizotolewa zitakuwa na daraja kama WATU???

hivi na wale wanaozaliwa njiti,yuko nje kwenye uangalizi maalumu je ungewaua watoto wa hivi kw vile wako nje ya mama yao?


Ndicho hicho ninachosema kwamba mimba ikizaliwa tu awe njiti au katika hali yoyote ukiua tu basi wewe unayo hatia ya kuua MTU kwasababu huyo tayari alikuwa na independent life.

Hitimisho:-

Narudia kusema; kutoa mimba bila sababu za msingi ni kosa mbele ya Mungu lakini sio kosa linalolingana na Mauaji ya Mtu.---Haiingii akilini kusema kwamba kutoa mimba ni sawa na kuua mtu anayetembea barabarani.
 
Unatetea kuitoa mimba na Id nyingine kweli umeamua!!.


Umesoma vyema mkuu, mimi sitetei kutoa mimba, mimi napinga kitendo cha kutoa mimba kuitwa ni mauaji ya mtu, eti mimba ikiwa tumboni inaitwa ni mtu.

Nasema tena kwamba kutoa mimba bila sababu za msingi ni Kosa mbele ya Mungu lakini sio sawa na kosa la kuua mtu barabarani.
 
Wema Sepetu aliwahi kupata mimba na kutoa, hadi sasa anatamani kupata maumivu ya Labour bila mafanikio......
 


🀣🀣, yaani mimi ni mtoa mimba???!!, na wewe ni mtia mimba???🀣🀣
 
Mi nazani wewe ndio mwehu,nyie madaktari uchwara mnatoa mimba kwa watoto wa shule akiri zenu zimejikita kwenye masirahi tu,hamthamin uhai wa kiumbe chochote

Kwangu ni haram hata mimba ya wiki moja kuitoa eti kisa tu ww uendelee ku survive kwa jinsi inavyo kupendeza.Mimba hutolewa kwa sababu maalum za kiafya tu,sio kama anavyodai huyo shoga yako hapo juu,tena kwa kujisikia,ana afya njema na hana shida yoyote kiafya,na wewe ulivyo limbukeni unaleta mawazo finyu juu ya uhai wa kiumbe kilichomo tumboni.

Unapiga debe watu watoe mimba! we hujui kila kitu huanza na hatua za awali na baadae hukamilika kuwa kiumbe kamili?
Hujui usipo heshimu kilicho kidogo hata kikubwa hutakiheshimu!

Mtazamo wako wa kibinadamu ndio unao kuharibu,Mapenzi sio sitarehe tu ,ukishajua kufanya mapenzi jiandae na kulea kijacho

Mimba ikishatunga , huo tayari ni mwanzo wa kiumbe kingine,haijalishi kinakula kwako au kwa jirani.Thamini uhai wa mwingine,hicho sio kidole au mguu kama unavyofikiria na elimu yako ya biology.
 
Dah Mungu akusaidie na akupe busara humu utashambuliwa sana ila majority ya wanawake wameshaua kimya kimya aisee. Mungu atusaidie tu kwa kweli
Na ww ulishawahi kunyonga kamoja best?
 



if cap fits--- no cap will fit in such a stupid head of yours.

Mahali gani mimi nimesema kutoa mimba bila sababu za msingi sio dhambi??!!----- usitake kupotosha ili uonekane eti umeongea point!!.

Mimi nimesema na ninarudia kusema hivi:- Kutoa mimba bila sababu ya msingi ni dhambi lakini kutoa mimba sio kosa linalolingana na kuua mtu binafsi, mfano kutoa mimba sio sawa na kuchukua silaha na ukaenda kuua mtu barabarani.

Mimba ya binadamu ni kitu cha thamani na kinastahili kutunzwa hadi mtoto/mtu azaliwe.

Siku ya hukumu, Watu wote ndio watahukumiwa juu ya madhambi yao, ama uwe uliuawa au uliua wote lazima tuhukumiwe kulingana na madhambi yetu, kama mnadai mimba ni mtu aliyeuawa wakati alipotolewa tumboni kwa mama yake je nafasi yake siku ya Qiyama ni ipi???---- leteni ushahidi hata kutoka katika maandiko ya dini juu ya mimba iliyotolewa tumboni kabla ya kuzaliwa nafasi yake siku ya Qiyama ni ipi???--- hizo mimba zitakuwa kama watu watakaosimama siku ya Qiyama??!!

Nimeingia upande wa dini kwani upande wa Biology ni weupe pee.

Je, Madaktari wanaotoa mimba kwasababu za kiafya kwa mjamzito au kwasababu za kifya za zygote tumboni na wao ni WAUAJI??

Kama Zygote ataonekana anazo abnomalities, mfano ulemavu utakaomfanya aishi kwa shida na pia awape wazazi wake shida za kimaisha na changamoto zingine na wakaamua kutoa mimba baada ya ushauri wa madaktari, je kama hiyo mimba ni MTU utashindwaje kuwaita hao madaktari Wauaji??--- maana yangu ni hii; usilete visingizio kwamba mimba ikitolewa kwa sababu za kiafya sio Uuaji lakini ikitolewa kwa sababu zingine ni uuaji--- kama umeamua kudai Kwamba kutoa mimba ni uuaji basi kila sababu itakayopelekea kutoa mimba itakuwa ni haramu kwani kutoa mimba ni uuaji kwa mujibu wenu, msiwe ndumilakuwili katika suala hilo.

Hitimisho; Mimi sio daktari na wala sijui udaktari kabisa ingawa O level nilisoma Biology.
 
Kasikilize wimbo wa Nikki Mbishi, kijusi.
 
Anahitaji msaada wa kisaikolojia huyo nyie hamjamuelewa tu
 
Bado sijakuelewa vizuri. Itabidi nirudie kusoma na kupata uhakika wa jambo hili hasa kwa upande wa kiroho kwa kuwashirikisha watumishi wa Mungu.......... hasa kwenye mimba inayohatarisha maisha ya mama ikitolewa je, ni dhambi au siyo dhambi?
 
Bado sijakuelewa vizuri. Itabidi nirudie kusoma na kupata uhakika wa jambo hili hasa kwa upande wa kiroho kwa kuwashirikisha watumishi wa Mungu.......... hasa kwenye mimba inayohatarisha maisha ya mama ikitolewa je, ni dhambi au siyo dhambi?


Bora wewe mkuu unayetaka kufanya tafiti kuliko wale wanaopinga tu bila hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…