Najipanga kufanya harusi rahisi sana, naomba mawazo yenu

Najipanga kufanya harusi rahisi sana, naomba mawazo yenu

music mimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
485
Reaction score
876
Tofauti na watu wengi mimi siyo muumini wa harusi kubwa zenye mbwembwe nyingi. Hivyo nimepanga harusi yangu iwe rahisi sana na nitagharamia kila kitu mwenyewe.

Sijui mke mtarajiwa atachukuliaje ila nitajitahidi kumuelewesha wazo langu mpaka aelewe. Wazazi nao nitawaelewesha maana wao ni wachangiaji wazuri na wanajitoa sana kwenye harusi za watu wengine najua wanatarajia nguvu sawa kwenye harusi ya kijana wao.

Kwa hiyo wadau naomba mawazo ya harusi rahisi lakini nzuri, kwa bajeti ya kama milioni 5 hivi.
~ Ukumbi
~ Matukio ya kwenye sherehe
~ Misosi na vinywaji
~ Namna ya kualika watu na idadi yao n.k.
 
Hongera mkuu. Angalau umeonyesha ukomavu kwa kuepuka liharusi likuubwa litakalokuacha na madeni kila kona.

Mungu Akuongoze na kukujalia ndoa yenye amani na upendo. Ngoja wajuzi wa hizi shughuli waje kukupa mwongozo ambao naamini utasaidia wengi!
 
Asante kwa kunielewa.
 
Wewe tu n.a. roho yako mwanawane. Kuna mwana alifanya yake ya kibingwa...

Aliangalia kwenye circle yake marafiki 25 wanaokula gambe, 25 wanaokunywa soda....akapata 50.

Akatumia mahesabu ya kijeshi/kijeda/kishule kwamba kilo moja ya nchele wanakula watu 4 na nyama hali kadhalika.

Akaandaa budget ya samaki sato 25 kwa wasokula nyama, matunda nk

Ibada ya arusi ikapigwa saa 4 mpk saa 6 mchana. Wakajisogeza ukumbini saa 7 home kwao.

Watu wakala, wakanywa....ilipofika saa 10 waliotindikiwa gambe wakajichanga wakaenda kuleta zingine kwa fedha yao....

Saa 12 kamili jioni MC katangaza "Bwana na Bibi Arusi wanaenda kujipumzisha"[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Zawadi alipata 2m[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi nilifanikiwa kwa kufanya hivi

Tafuta hoteli best hotels in town kama dar nenda Hayatt regency ukumbi huwa nibure utapata kiukumbi portable alafu chakulana vinywaji utaweka order kwao.

Tafuta mpambaji wa hako kasehemu ka watu 50

tafuta mziki wa kawaida na MC fulani wa kuchangamsha mambo

Hakikisha mwenyekiti wa kamati ni wewe na msaidizi wako

Nakuhakikishia utafurahia shughuli yako mpaka basi waalikwa wataona ni kitu cha kishua sana

Mimi nilitumia Milliono 3.8 vyote
 
Tafuta garden omba wawapangie viti au mtu wa event akusaidie idea. MC asiye na jina, muziki usio na kelele nyingi. Msosi na drinks. Waalikwa wasizidi 100. Mtakula mtakunywa mtaongea then mtacheza muziki kidogo kisha shughuli imeisha. Chenji unaenda Zanzibar au Mauritius na mkeo kwa fungate siku 3 zinatosha.
 
Screenshot_20221016-072426_1.jpg
 
Kuna sunni juzi kaja kuoa mtaani kwetu hakuna hata anayejuwa
yaani kama kikao tu
baada ya hapo akamchukua mke wake hao mdogo mdogo hata boda boda hakuchukua
Hahah maisha ni marahisi ila sisi wenyewe ndo tunayafanya yawe magumu
 
Mimi nilifanikiwa kwa kufanya hivi

Tafuta hoteli best hotels in town kama dar nenda Hayatt regency ukumbi huwa nibure utapata kiukumbi portable alafu chakulana vinywaji utaweka order kwao.

Tafuta mpambaji wa hako kasehemu ka watu 50

tafuta mziki wa kawaida na MC fulani wa kuchangamsha mambo

Hakikisha mwenyekiti wa kamati ni wewe na msaidizi wako

Nakuhakikishia utafurahia shughuli yako mpaka basi waalikwa wataona ni kitu cha kishua sana

Mimi nilitumia Milliono 3.8 vyote
Hongera
 
Kuna sunni juzi kaja kuoa mtaani kwetu hakuna hata anayejuwa
yaani kama kikao tu
baada ya hapo akamchukua mke wake hao mdogo mdogo hata boda boda hakuchukua

[emoji23][emoji23]
 
Tofauti na watu wengi mimi sio muumini wa harusi kubwa zenye mbwembwe nyingi.

Hivyo nimepanga harusi yangu iwe very simple na nitagharamia kila kitu mwenyewe.

Sijui mke mtarajiwa atachukuliaje ila nitajitahidi kumuelewesha wazo langu mpaka aelewe.

Wazazi nao nitawaelewesha maana wao ni wachangiaji wazuri na wanajitoa sana kwenye harusi za watu wengine najua wanatarajia same energy kwenye harusi yangu kijana wao.

Kwa hiyo wadau naomba mawazo ya idea za harusi simple lakini nzuri kwa bajeti ya kama million 5 hivi..

Venue
Matukio ya kwenye party
Misosi na vinywaji
Namna ya kualika watu na idadi yao
Etc
Hichi ninachokueleza hapa, kichukue kwa umakini mkubwa, maana nina uzoefu nacho.

1. Huenda 80% ya vijana waliosema hivyo na kujipanga hivyo mwisho wa siku waliishia kufanya harusi kubwa, gharama kubwa au mbwembwe zile zile za harusi zingine tulizozea. Kwanini? Harusi ni tukio la kujionyesha, kuwaburudisha na kuwafurahisha watu wengine kuliko wewe.

2. Taswira ya harusi utakayoifanya itategemea mambo hayo;
-Aina ya maisha unayoishi.
-Mtazamo wa mwenzi wako.
-Mtazamo wa ndugu zako wa karibu
-Mtazamo wa ndugu wa mwenzi wako
-Mtazamo wa marafiki zako wa karibu.

3. Kama unajipanga kufanya harusi simple au isiyo na gharama kubwa, basi zingatia zaidi haya:
-Kujipange zaidi kutaka kuoa (kufunga ndoa rasmi) pasipo kutaka kufanya harusi kabisa!

-Hakikisha anaishi mkoa au maeneo tofauti (mbali) na ambayo ndugu na jamaa zako wewe au wa mke wako wa karibu wanaishi. (Unaweza kuwa huru kufanya kile unachokitaka bila presha ya watu wengine)

-Hakikisha mwanamke unayetaka kumuoa ana mtazamo na msimamo kama wa kwako kuhusu hayo. (Kwa wanawake wengi, fahari ya kuwa na ndoa ni wao kuolewa kwa harusi, tena harusi kali kali).

4. Mipango na mikakati mingi ya harusi mara nyingi hupimwa kwa namna au mwelekeo wa send off itakavyokuwa. Kama mke wako mtarajiwa anajipanga kwa Send off kali, basi hesabu tu, mipango yako ya harusi ndogo inaweza kukwama!
 
Wewe tu n.a. roho yako mwanawane. Kuna mwana alifanya yake ya kibingwa...

Aliangalia kwenye circle yake marafiki 25 wanaokula gambe, 25 wanaokunywa soda....akapata 50.

Akatumia mahesabu ya kijeshi/kijeda/kishule kwamba kilo moja ya nchele wanakula watu 4 na nyama hali kadhalika.

Akaandaa budget ya samaki sato 25 kwa wasokula nyama, matunda nk

Ibada ya arusi ikapigwa saa 4 mpk saa 6 mchana. Wakajisogeza ukumbini saa 7 home kwao.

Watu wakala, wakanywa....ilipofika saa 10 waliotindikiwa gambe wakajichanga wakaenda kuleta zingine kwa fedha yao....

Saa 12 kamili jioni MC katangaza "Bwana na Bibi Arusi wanaenda kujipumzisha"[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Zawadi alipata 2m[emoji23][emoji23][emoji23]
Mimi kabisa uyo soon
 
Hio inatosha kabisa...
Hapo sio harusi ni kufunga ndoa.

Watu kumi,umemaliza hao chawa wengine achana nao hawafaida kwenye ndoa yako,zaidi ya kula na kunywa na kuanza kuitoa dosari harusi yenu,mara hivi mara vile..

Pia utaepuka madeni ya mc,mziki,wapiga picha,ukumbi kwa jambo la siku moja tu...

Siku moja asubuh nilimwambia ngedere wangu mmoja,twende tukafunge ndoa sasa hivi...

Akuamini....sema hakua na malengo na mimi,nikapita hivi...
Ila angekubali,ni mimi na yeye na wasimamizi wawili tunapiga kitu cha serikali..inaisha kihivyo.
 
Back
Top Bottom