Najipanga kufanya harusi rahisi sana, naomba mawazo yenu

Najipanga kufanya harusi rahisi sana, naomba mawazo yenu

Kuna sunni juzi kaja kuoa mtaani kwetu hakuna hata anayejuwa
yaani kama kikao tu
baada ya hapo akamchukua mke wake hao mdogo mdogo hata boda boda hakuchukua
Ukute sunni halafu mpare😂😂😂
 
Simple...uwe na msister asiependa makuu ila. Simple makeup 50,000. Nywele atengeneze natural look 50,000. Nguo ashone kama wanaija wakifunga civil wedding so kibongo bongo gauni fundi anashona 80000 na vitambaa na accesories 150000, venue kama ni dar ziko kibao free ila chakula ndo unalipia na mwisho sijajua unataka wangapi ila lets assume 50 yan hiyo ndo wote. So unalipia sahani 25000 mara 50 its 1,250,000 , picha mfanye 300,000, na usafiri wenu na wazazi tu 300,000 wazazi wakodiwe uber au bolt kama vipi. Drinks assume kila mtu anakunywa ya 20000 so ni 1,000,000 and keki 150000. Jumla 3,333,000 imeisha iyo. Nimejitolea kufanya kazi ya kamati.
 
Wewe tu n.a. roho yako mwanawane. Kuna mwana alifanya yake ya kibingwa...

Aliangalia kwenye circle yake marafiki 25 wanaokula gambe, 25 wanaokunywa soda....akapata 50.

Akatumia mahesabu ya kijeshi/kijeda/kishule kwamba kilo moja ya nchele wanakula watu 4 na nyama hali kadhalika.

Akaandaa budget ya samaki sato 25 kwa wasokula nyama, matunda nk

Ibada ya arusi ikapigwa saa 4 mpk saa 6 mchana. Wakajisogeza ukumbini saa 7 home kwao.

Watu wakala, wakanywa....ilipofika saa 10 waliotindikiwa gambe wakajichanga wakaenda kuleta zingine kwa fedha yao....


Saa 12 kamili jioni MC katangaza "Bwana na Bibi Arusi wanaenda kujipumzisha"[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]


Zawadi alipata 2m[emoji23][emoji23][emoji23]

Imeisha hiyoo hatutaki mba mba mba [emoji23][emoji23]
 
Kuna sunni juzi kaja kuoa mtaani kwetu hakuna hata anayejuwa
yaani kama kikao tu
baada ya hapo akamchukua mke wake hao mdogo mdogo hata boda boda hakuchukua

Hatutaki mba mba mba hiyoo [emoji23][emoji23]
 
Tofauti na watu wengi mimi siyo muumini wa harusi kubwa zenye mbwembwe nyingi. Hivyo nimepanga harusi yangu iwe rahisi sana na nitagharamia kila kitu mwenyewe.

Sijui mke mtarajiwa atachukuliaje ila nitajitahidi kumuelewesha wazo langu mpaka aelewe. Wazazi nao nitawaelewesha maana wao ni wachangiaji wazuri na wanajitoa sana kwenye harusi za watu wengine najua wanatarajia nguvu sawa kwenye harusi ya kijana wao.

Kwa hiyo wadau naomba mawazo ya harusi rahisi lakini nzuri, kwa bajeti ya kama milioni 5 hivi.
~ Ukumbi
~ Matukio ya kwenye sherehe
~ Misosi na vinywaji
~ Namna ya kualika watu na idadi yao n.k.
Bajeti yako ipo juu sana, weka bajeti ya milioni 2 tu inatosha sana.
 
Ila harusi mkuu lazima uwe na bajeti ya dharura usitegemee michango ya harusi na kamati utayumba ni hayo.
 
Nzuri hi mm sipendi masherehe kbsa hvyo wife ajiandae kwenda kwa mkuu wa wilaya.
 
Sikia yangu ya kipare,

Niliwaza watu wawe 100

Ukumbumbi bure eneo la baa

Chakula nilinunua zaga zoote mwenyewe nikamlipa mpishi 300000

Vinywaji laki 7 bia za buku jelo jelo na juice za Azam na soda na maji

Gari la mshikaji

Mpambaji laki 2

Kuhusu suti nilienda kkoo nikatungua ya laki nikaipitishia dry cleaner moja nzur hapa mjin na gauni ya Bibi harus nlimpta jamaa alimnuliat mkewe nikakod laki nalo nikapitishia dry cleaner

Mziki nililipa laki mc nikampa laki camera na video laki mbili haikufik 3m na kishereh kilikua kitamu balaa
 
Sikia yangu ya kipare,

Niliwaza watu wawe 100

Ukumbumbi bure eneo la baa

Chakula nilinunua zaga zoote mwenyewe nikamlipa mpishi 300000

Vinywaji laki 7 bia za buku jelo jelo na juice za Azam na soda na maji

Gari la mshikaji

Mpambaji laki 2

Kuhusu suti nilienda kkoo nikatungua ya laki nikaipitishia dry cleaner moja nzur hapa mjin na gauni ya Bibi harus nlimpta jamaa alimnuliat mkewe nikakod laki nalo nikapitishia dry cleaner

Mziki nililipa laki mc nikampa laki camera na video laki mbili haikufik 3m na kishereh kilikua kitamu balaa
You paid 3 million for 4-7 hours ceremony?
 
Mie harusi yangu nitaifanya Zanzibar ktk hotel ya kifahari ndugu upande wangu ni 10 upande wa Mke ni 10 jumla watu 22.

Bajet Mil 10.

Siombi mchango kwa mtu, hili jambo clipendi kbs
 
Back
Top Bottom