Tofauti na watu wengi mimi sio muumini wa harusi kubwa zenye mbwembwe nyingi.
Hivyo nimepanga harusi yangu iwe very simple na nitagharamia kila kitu mwenyewe.
Sijui mke mtarajiwa atachukuliaje ila nitajitahidi kumuelewesha wazo langu mpaka aelewe.
Wazazi nao nitawaelewesha maana wao ni wachangiaji wazuri na wanajitoa sana kwenye harusi za watu wengine najua wanatarajia same energy kwenye harusi yangu kijana wao.
Kwa hiyo wadau naomba mawazo ya idea za harusi simple lakini nzuri kwa bajeti ya kama million 5 hivi..
Venue
Matukio ya kwenye party
Misosi na vinywaji
Namna ya kualika watu na idadi yao
Etc
Hichi ninachokueleza hapa, kichukue kwa umakini mkubwa, maana nina uzoefu nacho.
1. Huenda 80% ya vijana waliosema hivyo na kujipanga hivyo mwisho wa siku waliishia kufanya harusi kubwa, gharama kubwa au mbwembwe zile zile za harusi zingine tulizozea. Kwanini? Harusi ni tukio la kujionyesha, kuwaburudisha na kuwafurahisha watu wengine kuliko wewe.
2. Taswira ya harusi utakayoifanya itategemea mambo hayo;
-Aina ya maisha unayoishi.
-Mtazamo wa mwenzi wako.
-Mtazamo wa ndugu zako wa karibu
-Mtazamo wa ndugu wa mwenzi wako
-Mtazamo wa marafiki zako wa karibu.
3. Kama unajipanga kufanya harusi simple au isiyo na gharama kubwa, basi zingatia zaidi haya:
-Kujipange zaidi kutaka kuoa (kufunga ndoa rasmi) pasipo kutaka kufanya harusi kabisa!
-Hakikisha anaishi mkoa au maeneo tofauti (mbali) na ambayo ndugu na jamaa zako wewe au wa mke wako wa karibu wanaishi. (Unaweza kuwa huru kufanya kile unachokitaka bila presha ya watu wengine)
-Hakikisha mwanamke unayetaka kumuoa ana mtazamo na msimamo kama wa kwako kuhusu hayo. (Kwa wanawake wengi, fahari ya kuwa na ndoa ni wao kuolewa kwa harusi, tena harusi kali kali).
4. Mipango na mikakati mingi ya harusi mara nyingi hupimwa kwa namna au mwelekeo wa send off itakavyokuwa. Kama mke wako mtarajiwa anajipanga kwa Send off kali, basi hesabu tu, mipango yako ya harusi ndogo inaweza kukwama!