Najiuliza wakati shetani anaasi mbinguni, alishawishiwa na nani? Maana hakukuwa na shetani muda huo. Binadamu tunashawishiwa na shetani dhambini

Imani za ki dini zinafundisha kwamba Binadamu wanashawishiwa na shetani kufanya maovu.

Muovu ni mfuasi wa shetani.

Je shetani wakati anahasi alishawishiwa na nani enzi hizo ? Na kwa nini Mungu asizuie shetani kuhasi ?
Wanasema hivyo kwa sababu shetani ni muasisi wa uasi ...shetani ni muhasisi wa uasi hivyo kawa taitooo ya yoyote afanyaye uasi SHETANI kawa kama SI UNIT ya UASI(DHAMBI)
 
Hili swali huwa najiuliza sana

Ni nani alimshawishi shetani kumuhasi Mungu?

Na kwa nini Mungu asizuie shetani kuhasi ?
kwa hakika nafsi (ya mwanadamu) inaamrisha sana maovu, isipokuwa ile ambayo Mola wangu Mlezi ameirehemu.

Suratul Yusuf : 53

Nafsi ya mwanadamu yenyewe ni yenye kuamrisha maovu

Ibilisi anaongeza ushawishi tu
 
Mimi naona jibu ni moja tu kwamba malaika walipewa utashi kama binadamu

Na itoshe kusema kwamba waliteswa sana kwasababu utashi hauwezi kumuongoza kiumbe akubali kuwa chini ya mwingine, lazima atafute uhuru

Kwa namna fulani namuona shetani kama shujaa ambaye hakukubali kupelekeshwa

Sasa Yahweh naye alikuza mambo tu, nafasi yake ya muweza wa yote haiwezi kupinduliwa na maandamano ya kiumbe mdogo shetani....

Kwanza alijua kabisa shetani atagoma, si mjuzi wa yote?

Haya mambo yanachanganya....

Nimeandika kama mpita njia tu asiyeshika imani yeyote ya kikristo
 
Hili swali huwa najiuliza sana

Ni nani alimshawishi shetani kumuhasi Mungu?

Na kwa nini Mungu asizuie shetani kuhasi ?
Kwenye Qur'an, imeelezwa sababu ya shetani kuasi...

Kosa lake lilikuwa kutokumsujudia Adam , sijda ya heshima na kutambua utukufu na daraja aliyopewa juu ya viumbe wengine.

Kwanini aliasi..... Ni kwasababu ya husda alokuwa nayo kwa baba yetu Adamu, aliapa kwamba yeye angefanywa Bora angemuangamiza na Adamu akifanywa Bora angemuangamiza pia.

Kwanini aliachwa akaasi..... Binadamu na majini wanauhuru wakuchagua njia wanayotaka kupita, Wana nguvu ndani ya maamuzi ya kuwa wema au waovu, kwahyo njia utakayoichagua itakuwa ni jukumu lako na utapelekwa huko huko unapokutaka.

Shetani tangu alivyoasi mpka Leo Bado anaendeleza kazi yake, lakini pamoja na uwepo wa shetani watu wema wapo na waovu wapo, ingekuwa shetani anaushawishi wa Moja kwa moja kwa watu, wema wasingekuwepo hata mmoja.

Shetani ana nguvu baada ya wewe mwenyewe kuamua kufata njia isiyosahihi na yeye anakushawishi zaidi Uende huko huko ulipokuchagua.

Mfano: Wewe una rafiki yako muhuni, mvuta bangi lakini hajawahi kukwambia hata siku Moja njoo tuvute, mkikutana ni story basi. Siku Moja ukaamua mwenyewe tu hebu nami nijaribu kuvuta, mshkaji akakupa bangi ukavuta, mshkaji akaanza

" nikivutaga hii Huwa najiskia vizuri sanaa, inanipa mzuka".

Kuanzia siku hiyo mshkaji akaanza kukuvuta zaidi kwenye uvutaji , akikuona

" Leo mshkaji wangu Nina Ile ya Arusha kbsaa, ya Leo Leo".

Usinambie katika hali hii rafiki yako ndo kakuingiza kwenye uvutaji, Bali ni wewe mwenyewe ndo umeingia.

Ndomna baada ya shetani kuasi kukaja miongozo, na mitume ili kumuweka mtu katika lengo lake husika na asifate nyayo za shetani aliyeasi. Kwahy ukiiacha hiyo miongozo basi wewe na shetani hamna tofauti wote waasi na shetani atakuwa na nguvu juu Yako kwakua umemfanya rafiki.

Lakini ukiifata miongozo uliyopewa shetani hawezi kuwa na nguvu juu Yako.
 
Yes, swali lake ni zuri sana tu, sababu kumbuka bibilia inasema kwenye mbingu mpya na nchi mpya dhambi haita kuwemo... Sasa je kivipi wakati hata mbinguni hakukuwa na dhambi lakini shetani alipata wazo la dhambi?
Kama binadamu tatukuwa huru kama kipindi hicho na sasa, hawatafikiria uovu kama sasa hata kwa nyakati moja?
je, Mungu atatupa uwezo wa ziada wa kuepuka dhambi ambao hakuwapa watu wa mwanzo?
Dhambi ni uvunjifu wa sheria sasa je inasemaje dhambi haita kuwepo wakati sheria zitakuwepo?
katika mbingu mpya dhambi haitakuwepo kwa sababu tutakuwa na uzoefu wa matokeo na madhara ya kutenda dhambi.Dhiki kuu,ziwa liwakalo moto na mateso ya jehanamu ya moto.Ukiona shetani na malaika zake na wafuasi wake wanavyoteseka hakuna atakayethubutu kutenda dhambi.Lakini tutakuwa na ROHO mtakatifu ROHO wa Mungu ndani yetu atakayetuongoza kutenda dhambi.
TUTAKUWA WASHINDI watakao ingia mbinguni ni watakatifu ambao waliishi maisha ya utakatifu wakiwa duniani tena dunia yenye vishawishi vya dhambi wakafaulu mtihani wakashinda vishawishi tamaa mbaya za mwili za dhambi wakamshinda shetani..hivyo wamechujwa hakuna kinyonge kichafu kitakachoingia mbinguni.Kama uliishinda dhambi duniani kwwnye vishawishi vya dhambi ukaingia mbinguni ukiwa mtakatifu ni unlikekly ukifika mbinguni uishinmaisha ya dhambi wakati duniani uliiishi maisha ya kitakatifu.TIKETI YA KUINGIA MBINGUNI ni UTAKATIFU NA ROHO MTAKATIFU.
 
Kwenye Qur'an, imeelezwa sababu ya shetani kuasi...

Kosa lake lilikuwa kutokumsujudia Adam , sijda ya heshima na kutambua utukufu na daraja aliyopewa juu ya viumbe wengine.

Kwanini aliasi..... Ni kwasababu ya husda alokuwa nayo kwa baba yetu Adamu, aliapa kwamba yeye angefanywa Bora angemuangamiza na Adamu akifanywa Bora angemuangamiza pia.

Kwanini aliachwa akaasi..... Binadamu na majini wanauhuru wakuchagua njia wanayotaka kupita, Wana nguvu ndani ya maamuzi ya kuwa wema au waovu, kwahyo njia utakayoichagua itakuwa ni jukumu lako na utapelekwa huko huko unapokutaka.

Shetani tangu alivyoasi mpka Leo Bado anaendeleza kazi yake, lakini pamoja na uwepo wa shetani watu wema wapo na waovu wapo, ingekuwa shetani anaushawishi wa Moja kwa moja kwa watu, wema wasingekuwepo hata mmoja.

Shetani ana nguvu baada ya wewe mwenyewe kuamua kufata njia isiyosahihi na yeye anakushawishi zaidi Uende huko huko ulipokuchagua.

Mfano: Wewe una rafiki yako muhuni, mvuta bangi lakini hajawahi kukwambia hata siku Moja njoo tuvute, mkikutana ni story basi. Siku Moja ukaamua mwenyewe tu hebu nami nijaribu kuvuta, mshkaji akakupa bangi ukavuta, mshkaji akaanza

" nikivutaga hii Huwa najiskia vizuri sanaa, inanipa mzuka".

Kuanzia siku hiyo mshkaji akaanza kukuvuta zaidi kwenye uvutaji , akikuona

" Leo mshkaji wangu Nina Ile ya Arusha kbsaa, ya Leo Leo".

Usinambie katika hali hii rafiki yako ndo kakuingiza kwenye uvutaji, Bali ni wewe mwenyewe ndo umeingia.

Ndomna baada ya shetani kuasi kukaja miongozo, na mitume ili kumuweka mtu katika lengo lake husika na asifate nyayo za shetani aliyeasi. Kwahy ukiiacha hiyo miongozo basi wewe na shetani hamna tofauti wote waasi na shetani atakuwa na nguvu juu Yako kwakua umemfanya rafiki.

Lakini ukiifata miongozo uliyopewa shetani hawezi kuwa na nguvu juu Yako.
sasa kiumbe kimetoka udongoni kina upeo mfupi halafu wewe mwenye nguvu ya kusambaratisha milima unaambiwa ukisujudie eti kipo juu ya viumbe vyote inaingia akilini kweli?

shetani hakuwa mjinga
 
shida sio shetani kuasi
shida ni muumba wa vyote je hakujua ana muumba malkia/shetani atakaye kuja kuasi
kwa nini hakumzuia asia asi maana ana uwezo huo

kwa nn sisi tumuombe ikiwa shida zote hizi chanzo ni yeye
 
katika mbingu mpya dhambi haitakuwepo kwa sababu tutakuwa na uzoefu wa matokeo na madhara ya kutenda dhambi.Dhiki kuu,ziwa liwakalo moto na mateso ya jehanamu ya moto.Ukiona shetani na malaika zake na wafuasi wake wanavyoteseka hakuna atakayethubutu kutenda dhambi.Lakini tutakuwa na ROHO mtakatifu ROHO wa Mungu ndani yetu atakayetuongoza kutenda dhambi.
TUTAKUWA WASHINDI watakao ingia mbinguni ni watakatifu ambao waliishi maisha ya utakatifu wakiwa duniani tena dunia yenye vishawishi vya dhambi wakafaulu mtihani wakashinda vishawishi tamaa mbaya za mwili za dhambi wakamshinda shetani..hivyo wamechujwa hakuna kinyonge kichafu kitakachoingia mbinguni.Kama uliishinda dhambi duniani kwwnye vishawishi vya dhambi ukaingia mbinguni ukiwa mtakatifu ni unlikekly ukifika mbinguni uishinmaisha ya dhambi wakati duniani uliiishi maisha ya kitakatifu.TIKETI YA KUINGIA MBINGUNI ni UTAKATIFU NA ROHO MTAKATIFU.
Umejibu vyema, sema nawaza je katika muda wowote hapa duniani kuna mtu ambae ni msafi na mtakatifu? Au ndio lisilowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu kinawezekana?
 
Hili swali huwa najiuliza sana

Ni nani alimshawishi shetani kumuasi Mungu?

Na kwa nini Mungu asizuie shetani kuasi ?
Nani kakudanganya unashawishiwa na shetani?

Tamaa (nia/desire) au matamanio yako mwenyewe juu ya kitu au jambo hukudanganya. Inategemea na tabia ulizojikusanyia moyoni mwako. Ibilisi ni roho iliyojikusanya moyoni mwako na kuwa tamaa.

Mfano. Mnaweza kuwa wanaume wawili mkapita mahali kuna wanawake wanajiuza. Wewe ukachagua kumfuata muuzaji na mwenzako akaamua kuondoka kukuacha umparamie (au kinyume chake pia ni sahihi). Hapo shetani anatoka wapi sasa jomba.

22 mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;
Waefeso 4:22

23 na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu;
Waefeso 4:23

24 mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.
Waefeso 4:24

27 wala msimpe Ibilisi nafasi.
Waefeso 4:27
 
Mimi naona jibu ni moja tu kwamba malaika walipewa utashi kama binadamu

Na itoshe kusema kwamba waliteswa sana kwasababu utashi hauwezi kumuongoza kiumbe akubali kuwa chini ya mwingine, lazima atafute uhuru

Kwa namna fulani namuona shetani kama shujaa ambaye hakukubali kupelekeshwa

Sasa Yahweh naye alikuza mambo tu, nafasi yake ya muweza wa yote haiwezi kupinduliwa na maandamano ya kiumbe mdogo shetani....

Kwanza alijua kabisa shetani atagoma, si mjuzi wa yote?

Haya mambo yanachanganya....

Nimeandika kama mpita njia tu asiyeshika imani yeyote ya kikristo
Na tangu enzi hzo mpka Leo shetani Wala yeyote Hana uwezo wa kupindua.

Shetani hakupunguza Chochote katika ufalme wake.
Shetani Hakuwa na uadui na muumba wake Bali alikuwa na uadui na aliyeumbwa ambae ni Adam.

Kwani wewe hujawahi kuona katika familia mtoto akifaulu vizuri baba au mama anamletea zawadi nzuri kwaajili yake!??, Watoto wengine wananuna na kulia!?, Wengine wanaanza kuchukia wazazi wao wakati kosa ni lao hawakusoma walikuwa wakicheza!?.

Hapo mtoto akinuna na kukimbia nyumba akahama , kosa ni lako au lake!?.

Au wale watoto ambao wanavuta bangi mpka wanawaibia wazazi wao, mzazi amekanya mpka akachoka, akikutimua kosa ni lake au lako!?.

Binadamu na majini wamepewa uhuru wa kuchagua njia zao wenyewe.

Huwezi kunidharau halafu Bado nikukumbatie!? Ilihali hujaomba msamaha na imejaa kiburi.

Yaani mwanao akutukane mbele za watu , Bado akirudi nyumbani anakubamizia milango , anakuvimbia na wewe ndo baba kichwa Cha familia, umuache usimuadhibu!?, Hawa wengine wanajifunza nini, kwamba baba bogus hata ukimtukana hakufanyi Chochote.

Ikiwa wewe huwezi Hilo kwanini aliyekuumba akubali dharau hiyo.
 
sasa kiumbe kimetoka udongoni kina upeo mfupi halafu wewe mwenye nguvu ya kusambaratisha milima unaambiwa ukisujudie eti kipo juu ya viumbe vyote inaingia akilini kweli?

shetani hakuwa mjinga
Oohh!! Maamuzi ni yako ila sie wengine ni Bora kuliko shetani, wewe kma umeamua kuwa shetani ni Bora kuliko wewe mtajuana na rafiki yako.
 
sasa kiumbe kimetoka udongoni kina upeo mfupi halafu wewe mwenye nguvu ya kusambaratisha milima unaambiwa ukisujudie eti kipo juu ya viumbe vyote inaingia akilini kweli?

shetani hakuwa mjinga
Ni kweli binadamu, tuna upekee mbele za Mungu ila hakuwahi kuwafanya malaika wamsujudie mwanadamu, ukristo unaamina anaepaswa kusujudiwa ni Mungu pekee... Lakini kiuwezo malaika wana uwezo mkubwa kuliko binadamu, ni kinyume na kanuni za asili kiumbe chenye uwezo mkubwa kuwa chini ya kiumbe chenye uwezo mdogo... Nakubaliana na wewe sio ukweli
 
Hapo mwanzo Lucifer alikuwa ndo malaika aliyependwa sana na Mungu na ndiye mkuu,,, yaan ukiwapanga kwenye Irish’s baada ya Ueya Yesu aliyekuwa anafuata alikuwa shetani saa. Shetani alikuwa hayuko taysri kuongozwa na Yesu hivyo a kaamua kujitenga kwa kuvunja sheria ya Mungu . Hivyo akaasi na kuwashawishi wengine na wakejiunga naye
 
Dhambi ni nini??
Kushindwa kutii maelekezo ya Mungu.

Kosa la shetani katika sakata la Adamu na Hawa ni kusema UONGO. Ndiye muasisi wa uongo.

Adamu kosa lake ni kutokutii maelekezo au maagizo ya Mungu. Adamu alipoasi maagizo ya Mungu dhambi ikazaliwa.
 
Back
Top Bottom