Hili swali huwa najiuliza sana
Ni nani alimshawishi shetani kumuhasi Mungu?
Na kwa nini Mungu asizuie shetani kuhasi ?
Kwenye Qur'an, imeelezwa sababu ya shetani kuasi...
Kosa lake lilikuwa kutokumsujudia Adam , sijda ya heshima na kutambua utukufu na daraja aliyopewa juu ya viumbe wengine.
Kwanini aliasi..... Ni kwasababu ya husda alokuwa nayo kwa baba yetu Adamu, aliapa kwamba yeye angefanywa Bora angemuangamiza na Adamu akifanywa Bora angemuangamiza pia.
Kwanini aliachwa akaasi..... Binadamu na majini wanauhuru wakuchagua njia wanayotaka kupita, Wana nguvu ndani ya maamuzi ya kuwa wema au waovu, kwahyo njia utakayoichagua itakuwa ni jukumu lako na utapelekwa huko huko unapokutaka.
Shetani tangu alivyoasi mpka Leo Bado anaendeleza kazi yake, lakini pamoja na uwepo wa shetani watu wema wapo na waovu wapo, ingekuwa shetani anaushawishi wa Moja kwa moja kwa watu, wema wasingekuwepo hata mmoja.
Shetani ana nguvu baada ya wewe mwenyewe kuamua kufata njia isiyosahihi na yeye anakushawishi zaidi Uende huko huko ulipokuchagua.
Mfano: Wewe una rafiki yako muhuni, mvuta bangi lakini hajawahi kukwambia hata siku Moja njoo tuvute, mkikutana ni story basi. Siku Moja ukaamua mwenyewe tu hebu nami nijaribu kuvuta, mshkaji akakupa bangi ukavuta, mshkaji akaanza
" nikivutaga hii Huwa najiskia vizuri sanaa, inanipa mzuka".
Kuanzia siku hiyo mshkaji akaanza kukuvuta zaidi kwenye uvutaji , akikuona
" Leo mshkaji wangu Nina Ile ya Arusha kbsaa, ya Leo Leo".
Usinambie katika hali hii rafiki yako ndo kakuingiza kwenye uvutaji, Bali ni wewe mwenyewe ndo umeingia.
Ndomna baada ya shetani kuasi kukaja miongozo, na mitume ili kumuweka mtu katika lengo lake husika na asifate nyayo za shetani aliyeasi. Kwahy ukiiacha hiyo miongozo basi wewe na shetani hamna tofauti wote waasi na shetani atakuwa na nguvu juu Yako kwakua umemfanya rafiki.
Lakini ukiifata miongozo uliyopewa shetani hawezi kuwa na nguvu juu Yako.