Najua kwa sasa mmejifungia Kikaoni Hotelini Posta ili Kumfuta Kazi Kocha Mkuu, ila hata nyie hatuwataki tena SSC

Najua kwa sasa mmejifungia Kikaoni Hotelini Posta ili Kumfuta Kazi Kocha Mkuu, ila hata nyie hatuwataki tena SSC

Najua Usiku huu au Kesho na haitofika Jumanne Simba SC itaachana rasmi na Kocha wake Mkuu Roberto Oliviera kupitia Tangazo ( Taarifa kwa Umma )

Timu itakuwa chini ya Makocha Wazawa Wawili ( wenye Vyeti na Sifa zinazotakiwa na CAF ) na Kozi muhimu za TFF ameshiriki huku taratibu ikimtafuta Kocha Mkuu mpya ambaye anaweza kuwa ni Nabi ( Tunisia ) au Ibenge ( Congo DR ) au Ndayiragije ( Burundi )

GENTAMYCINE naomba nyote mliokaa Kikao cha Siri hapo Posta ( Hoteli yenye Hadhi ) mkimaliza Kikao nanyi pia muondoke ndani ya Simba SC kama mnavyomfukuza Kocha Mkuu Mbrazili Roberto / Robertinho.
Mkuu vijana wa Facebook wanakuibia content zako
 
😂😂😂😂
Huwa napenda namna anasimangwa na wana halafu yeye wala hana habari anajibu zake, 'Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King'..!!
Wakizidisha kumsimanga anapambana nao kwa matusi makali makali halafu yeye ndo huwa anaishia kulimwa ban. Mods ni kama vile walishamjulia yaani. Na haters wake huwa hawamuachi ndo maana karibu kila uzi atakaoanzisha ni lazima tu utakuwa na hekaheka kwa sababu ni lazima haters waje kumzodoa. Ni burudani tosha 😁😁😁
 
Haters na Hypocrites utawajua tu. Hivi mwaka Jana Klabu ya Yanga SC chini ya Kocha Nabi ilipofanya vibaya Mechi za Kimataifa mpaka Mashabiki na Wanachama wakataka Ajiuzuru au Aondoke huku Wachambuzi na Waandishi wa Habari wakibashiri kuwa atafungashiwa Virago ( Atafukuzwa ) na kila Mtu aliamini hivyo je, alifukuzwa?

Kilichokuumiza ni kuona GENTAMYCINE kaja na Taarifa ya uhakika na niliyojiamini nayo 100% kutokana na Vyanzo vyangu na hatimaye leo Jumanne ( kama nilivyoitabiri ) kile nilichokileta hapa Kimetimia.

Kwani mkikubali tu kuwa GENTAMYCINE ndiyo Mfalme wa Habari za uhakika za Michezo na Masuala Mtambuka ya Kijamii ( katika Jamii ) mnapu gukiwa na nini? Wivu wenu juu yangu utawapelekeni Motoni.

Na kwa Jeuri, Nyodo na Kujiamini nakuja na Exclusive Info nyingine ya Mpira itokanayo na Derby ya Juzi muda si mrefu hapa hapa Jamiiforums na hakuna Mtu Mwingine yoyote yule anayo au anayoijua zaidi yangu Mimi tu.

Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King!!
Sawa mkuu ngoja tusubiri hizo exclusive zingine.
 
IMG_20231021_072200.jpg
 
Posta gani??
Hoteli gani????
Mtaa gani????
Viongozi gani???
Wakiwa wangapi???
Majina yao akina nani??

Usilete ubashiri kwenye masuala ya soka.

Ilikuwa lazima Robertinho atimuliwe labda ni mtoto tu dio asingeweza kulijua hilo
 
Ukitoa matusi plus majivuno, kiburi na dharau jamaa anapata sana taarifa nyeti kuhusu soka la nchi hii! Inawezeka kuna waandishi wanaiba taarifa zake huku!
Niliwahi kukutana na habari mtandao mwingine yani ni C& P ya huyu jamaa.
 
Back
Top Bottom