Najuta kuchukua mkopo “Pesa X”

Hata akifuta app Yao haisaidii kitu....alipe madeni ya watu alipe...
 
Dooh sawa acha tu nikaze ila nkipata nawapa
 
Lipa kwanza halafu kopa tena.

Hapa lengo la kukopa tena ni Ili wao wakutafute wewe na siyo wewe uwatafute, maana ukirejesha halafu wakawa hawakudai, hawatakutafuta kamwe.

Wakikupigia waeleze kwamba mkopo uliopita walikudhalilisha, kwa hiyo utawapeleka mahakamani kudai fidia ya udhalilishaji maana walitoa siri zako za kifedha.

Waambie unawapa siku moja watume sms kuwa contacts zako zote ya kuomba radhi kuwa wewe siyo tapeli.

Wakishatuma sms za kukusafisha (utapata majibu toka kwa ndugu), basi Kaa kimya na usiwalipe huo mkopo wa pili.

Hapa utakuwa umewaingiza kwenye mfumo wako; kwanza, hawataweza tena kuwaaminisha watu kwamba wanakudai maana wameshajichanganya kwa kuomba radhi, pili, utakuwa umejilipa fidia ya udhalilishaji.

Baada ya hapo, hata wakipiga simu waambie hatudaiani.

Maana kama hawana ustaarabu kwako ni kwanini wewe uwe mnyonge kwao?
 
Ningekuwa na pesa ningewalipa mkuu
 
Kama hauna mshipa wa Aibu haitakuwa na maana. Ila kama unao lazima uwe na aibu na utaumia nafsi.. Wanakutengenezea group ambalo member ni ndugu zako(ulo save namba namba zote) wanaweka na maneno makali sana (kama Tapeli, muogopeni ni mwizi)
Zaidi ya yote hata picha zako za uchi kama zipo, Au meseji za napenzi kama ulikuwa unachiti
 
Wanatuma what's up kutoka kwenye phone book yake sijui wanapata wapi na wanakuchafua kwamba ni tapeli.Nilishatumiwa Tena mtu aliyekopa ni mtu anaeheshimika nilishangaa .Achana na mikopo hiyo
 
Futa application yao kwenye simu yako.
Kitu cha pili futa google account halafu unda google account mpya.
Hapo watakua hawakupati kabisa wataishia kukutafuta wewe tu.
Na ukiona wanasumbua sana lain yako ifungie kwa muda.
 
Ni nusu Kwa nusu,. Mbona ni kama matapeli tuu. Ila Kwa kulinda heshima yake alipe tuu. Maana nasikia wanatuma meseji Kwa contact zako zote kuwafamisha kuwa mkopaji ni tapeli. Na wenye wasap watatumiwa picha pia
Ukifuta application yao unaondoa access ya wao kupata contact za ndugu zako.
Watabakia na contact za wadhamini na zako tu.
Pia hata access ya picha zako wanakosa kwasbabu app yao umeifuta.
Pia ukifuta google account utaanzisha account mpya ndio umewakata maini kabisa.
 
Uzuri huko watakapopiga simu ndio kwanza mtu atajuwa hawa ni wale matapeli wa mtandaoni wa ile pesa tuma kwenye namba hii.

Yani mkopeshane pesa wenyewe halafu unipigie mimi simu? Nakupa full dose utakoma.
 
Hii sio sifa bali ni kuharibia watu wenye uhitaji wa kweli wa hiyo mikopo.

Watanzania tujitambue sasa..!
Umeona wapi hii mikopo ya riba asilimia 80 inamnufaisha mtu!??
Bro riba asilimia 80!?
Kama hakika loan nilikopa 50k na wakataka nirudishe 90k.
Sawa ukope laki tano halafu urudishe laki tisa imekaa sawa??.
 
Achana nao watakatisha pesa hao, hawana uwezo wa kukufanya chochote, kwanza hawatambuliki na BOT kama sheria inavyotaka.
Hii nchi ndio maana watu kama Kiboko ya Wachawi wanatutapeli na kutukashifu juu. Halafu tunalia serekali itutetee.

Haya makampuni ya kitapeli ya kukopesha kuna watu wanayatetea kabisa, Eti ulikopa kwa shida zako walipe. Kibaya hata term's and condition zao za uongo sana, Riba unakutana nayo ukishakopa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…