Najuta kuchukua mkopo “Pesa X”

Sasa itasaidia nini wakishanitengenezea Hilo group la what's app??
Haina maana kwako kama wewe ni muokota makopo na mnywa visungura. Ila kama ni mtu mwenye heshima zake, una familia, una ndugu, una marafiki na watafutaji wenzako mnategemeana kwenye suala la uaminifu ujue hapo unapoteza credibility.

Kwa namna yeyote ile mimi siwezi jihusisha na mtu anakopa mikopo uchwara ya mtandaoni na anashindwa kulipa, anakubali kutangazwa kama mwizi. Kama hana aibu kwa wale jamaa sembuse kwa hela yangu mwenyewe ambaye sitomtangaza wala kumsumbua.

Mimi circle yangu kupelea hela ni suala la kawaida hivyo ni simu moja unaomba hela wala husemi unarudisha lini wala unaenda fanyia nini. Sasa leo hii nitangazwe tapeli wa mikopo umiza si nitaonekana mwendawazimu.
 
Usilipe achana nao zaidi ya kutuma message kwa namba za jamaa zako na vitisho viingi hawana cha zaidi.Nika ma Joka la kibisa.Hao ni matapeli wanafanya biashara haramu.Ndo maana ukiwauliza ofisi iko wapi hawakuonyeshi ! Hapo ndo ujue hao ni magumashi biashara wanayofanya sio ! We waulize ofisi iko ile uende.Wakikuonyesha njoo hapa unitag ! Watakutumia maneno meeengi ya vitisho lakini hakuna lolote !
 
Wanaorudisha ni wengi kuliko wanaotapeli na riba zao kubwa. Sasa hivi hapa Tz hakuna biashara yenye hela kama ukopeshaji. Wanaofikia level za microfinace wanapiga hela sana.
Ooh okay sawa, naona ina utapeli mwingi.....katika biashara ambayo siwezi hata kuithubutu ni hii yani huo mtaji wa kukopesha bora nkale kitimoto na bia, hapana asee.
 
Hii haiwezekani
 
Dah kweli nchi ngumu sana unakopa 50 elfu tu inakutoa kamasi mbichi je ingekuwa milioni moja si utauza nyumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…