sawa lakini asijutieSawa ardhi ni mali lakini malengo yake ya kukwepa kodi ya pango mjini hayajatimia kwa sasa. Kaenda kununua mbali mno haimsaidii. Labda kama angenunua huko kwa malengo ya kufuga lakini si makazi wakati shughuli zake mwenyewe ziko posta mpya. Hivyo mimi namshauri eneo hilo alifanye la mifugo ajipange atafuta karibu apange baadaye anaweza kuja kupauza kwa bei nzuri tu
nilidhani unasema Milioni 13 kumbe milioni 1Kuna viwanja vinauzwa 1.3milion huko kisemvule na vikindu, huwa najiuliza kiwanja cha 1.3milion si kitakuwa mbali sana na mjini..yaani kila siku una drive 70km kwenda na kurud kazini..lakin hongera kwa kuwa na Nyumba
Kuna viwanja vinauzwa 1.3milion huko kisemvule na vikindu, huwa najiuliza kiwanja cha 1.3milion si kitakuwa mbali sana na mjini..yaani kila siku una drive 70km kwenda na kurud kazini..lakin hongera kwa kuwa na Nyumba
Kujenga sio tatizo kinachotakiwa usijenge maadamu umepata kiwanja.Kabla ya kujenga zingatia yafuatayo:Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).
Bado sijaweka ukuta, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.
Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
Iko hivo hata bunju miaka ya nyuma palionekana kijijini lami ilikuwa inaishia nyaishozi kuja huku kidongo chekundu hakuna umeme leo hapashikikiNina ushuhuda: Pale Sinza, miaka ya nyuma kulikuwa ni pori. Chuo kikuu enzi hizo wakachukuwa eneo kubwa na kuwagawia ma-lectrurers wao. Kuna waliokataa wakasema ''huku porini kwenye madimbwi ya maji ni nani atakuja kukaa huku. Leo hii Sinza imegeuka na kuwa eneo tofauti kabisa. Hapo ulipozunguzumzia Sinza makaburini na maeneo yote ya karibu yalikuwa na pori na ndiyo kisa cha kuyafanya yawe sehemu ya kuzikia.
Bei tunazonunulia viwanja dsm ni bora ukaenda mkoani utapata kiwanja karibu kabisa na mjini unajenga nyumba yako safi na ukiipangisha hukosi kodi ya 200k au 150k kwa mwezi. Mfano mkoa kama Tanga ukiwa na million 6 au 7 unaweza kupata kiwanja within 15 kilomita kutoka mjini, ukijenga nyumba nzuri kupata mpangaji ni uhakika. Kodi utakayopata mkoani unaitumia kupanga sinza au magomeni
kasema kerege, sio Perege.... ni bagamoyo baada ya bunju, mapinga then KeregeUnasema perege iko wapi? Sio Mwanga upareni ndaani ndani huko?
Bora uwashauri wenzio wenye mawazo kama yako ili wasikimbilie kujenga maana sisi wenye majumba mjini tunawahitaji kama wapangaji wetu kutuingizia kipato, sasa kila mtu akijenga sisi tutakula wapi? Bora uwashauri wenzio mbaki kuwa wapangaji tu hivyo viwanja tutanunua sie na tutajenga mijengo wengine mbaki tu kuwa wapangaji.Kwa Dar kwa mfanyakazi wa kawaida kutaka ujenge nyumba kiwanja utapata kilomita 40 au zaidi nje ya mji ujenge.
Mbaya zaidi ofisi nyingi ziko posta hivyo itakulazimu uwe unaamka sa 9 ili kufika ofisini sa 2, na kurudi nyumbani ukitoka sa 11 unafika sa 3. Hii sababu ni moja tu ya miundombinu mibovu kwa hapa Dar es salaam, barabara ya kuja na kutoka mjini ni zile zile hakuna njia mbadala na kama zipo ni za hovyo sana.
Mimi Dar siwezi kujenga, ni hasara tupu, ggharama za usafiri kutoka kwako hadi kazini ni zaidi ya 200,000 kwa mwezi, hujaja chakula, uusumbufu mwingine alafu niwe najisifu tu eti kisa nakaa kwangu.
Nenda kinyerezi, mbezi makabe, goba, mabwepande na kwenda huko Mapinga, mbweni, kitopeni, nk watu wametelekeza nyumba nzuri kule kwa sababu ya adha ya usafiri.
Bora upange jirani na mjini uishi kwa raha kuliko kua na kwako huku unaishi kwa shida kisa unaishi kwako. Kuna mshikaji wangu kajenga huko kimara porini imebidi akimbie nyumba, akapange apartment kariakoo.
Mimi nimepanga jirani tu na kazini kwangu, kilomita 8, hata sa 1:30 natoka kwangu na nafika kazini kabla ya ya 2:00 na maisha ni matamu sana.
Maisha ni hesabu, ukifanya miscalculation maisha yako yatakua magumu sana.
Iko hivo hata bunju miaka ya nyuma palionekana kijijini lami ilikuwa inaishia nyaishozi kuja huku kidongo chekundu hakuna umeme leo hapashikiki
Kumbe wapo wengi nina ndugu yangu kajenga huko naye kakimbia amerudi mjiniDadaangu kajenga huko huko mitaa ya baobab sec school, ndani ndani ni anajutraa balaa, nae kapakimbia!
Usalama ni changamoto isiyo na solution ya kuaminika. Kuna jamaa alikuwa maeneo hayo, ana uwezo, ameweka ukuta wenye nyaya za umeme na ving'ora na mbwa ndani lakini bado alikuwa target ya majambazi mara kwa mara. Mara wamtegeshee wakati anaingia kwenye geti au wakati mwingine waje mchana.Vipi kuhusu usalama
Yah..watu wanakusubiri wakati unaingia..wanakufanyia unyama wanamaliza wanapika na msosi wanakula wanasepa..majitani hadi waje kujua inakua too late.Usalama ni changamoto isiyo na solution ya kuaminika. Kuna jamaa alikuwa maeneo hayo, ana uwezo, ameweka ukuta wenye nyaya za umeme na ving'ora na mbwa ndani lakini bado alikuwa target ya majambazi mara kwa mara. Mara wamtegeshee wakati anaingia kwenye geti au wakati mwingine waje mchana.