Najuta kuhamia kwangu Kerege

Najuta kuhamia kwangu Kerege

Labda sikueleweka..ishu hapa sio jirani akiniona nimeshika chuma la eicher atasemaje .ishu ni yale mazoea mzee baba!hapa hakuna cha elimu ya kujitmbua wala nn...!kuna kaulemavu kapo sana ukizoea kutembelea gari!wenyewe wanakajua!
Haka kaulemavu kabaya sana hata ukikaza siku mbili ukapanda daladala lazima urudi kwenye gari yako hata kwa mkopo wa mafuta
 
Mkuu binafsi si kushauri hiyo nyumba uuze hata kidogo ,bora ww umejenga kerege mimi nimejenga kiromo na nimehamia huko na shughuli zangu zinaenda ,fikiria mtu anaekaa mlandizi anapiga mishe town au anayekaa chalize na kila siku asubuhi yuko town na jioni anageuka ,
Usiuze nyumba mkuu ,utakuja juta usawa huu ,
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Bado sijaweka ukuta, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
Kerege pazuri sana na ni karibu kuliko kwa anayeishi Kigogo Fresh au Chanika kuelekea mjini kati.

Nadhani kuna mambo utakuwa hukubaliani nayo kuyaacha na ndiyo yanayokuumiza.

Mfano: Unatumia gari kubwa mno, hutaki kujichanganya na watu na bado hujakuwa na timing na muda foleni inakuwa imepungua.

Pata hii: Mdau wangu anaishi Kisemvule ana gari inaitwa Alphard, kila asubuhi ana vichwa saba kwenda navyo mjini kwa 2,000 na jioni kurudi hali kadhalika.

Anapata shs 14,000 na kurudi 14,000 hapo vipi? Hajarahisisha maisha tuu?

Thus why nakwambia jichanganye na wenyeji utapata mbinu mpya ya kujikwamu lakini kama hakuna mbadala basi nunua gari ndogo achana na magari ya show off. Yanakunyonya damu
 
Mkuu uza hiyo gari tafuta Toyota hiace ya 15milion, Asubuhi unapokuja mjini beba abiria, unaporudi kerege pia beba abiria. weekend aamka asubuhi piga trip kazaa tegeta bagamoyo.. Hapo utakuwa umejiongezea kipato lakini pia utakuwa umepata hela ya mfuta kila siku ya kuendea kazini..
Kuandika ni rahisi kama kilimo cha online
 
Bora uwashauri wenzio wenye mawazo kama yako ili wasikimbilie kujenga maana sisi wenye majumba mjini tunawahitaji kama wapangaji wetu kutuingizia kipato, sasa kila mtu akijenga sisi tutakula wapi? Bora uwashauri wenzio mbaki kuwa wapangaji tu hivyo viwanja tutanunua sie na tutajenga mijengo wengine mbaki tu kuwa wapangaji.
Wakistaafu wanahamia kwenye kodi za 5000 jangwani
 
Kerege pazuri sana na ni karibu kuliko kwa anayeishi Kigogo Fresh au Chanika kuelekea mjini kati.

Nadhani kuna mambo utakuwa hukubaliani nayo kuyaacha na ndiyo yanayokuumiza.

Mfano: Unatumia gari kubwa mno, hutaki kujichanganya na watu na bado hujakuwa na timing na muda foleni inakuwa imepungua.

Pata hii: Mdau wangu anaishi Kisemvule ana gari inaitwa Alphard, kila asubuhi ana vichwa saba kwenda navyo mjini kwa 2,000 na jioni kurudi hali kadhalika.

Anapata shs 14,000 na kurudi 14,000 hapo vipi? Hajarahisisha maisha tuu?

Thus why nakwambia jichanganye na wenyeji utapata mbinu mpya ya kujikwamu lakini kama hakuna mbadala basi nunua gari ndogo achana na magari ya show off. Yanakunyonya damu
Kupakia watu saba kila siku kwenda na kuridi ni kuchosha gari tu for nothing
 
Wakuu enzi za Neema za Mkwere nilijenga maeneo ya Kerege sasa mambo yalipobana kodi ikanishinda Sinza nikahamia kwangu Kerege asee najuta maana hizo gharama za mafuta zinazidi kodi ya nyumba Sinza (400,000/=).

Bado sijaweka ukuta, vibaka kila mara wanavamia nikiwa kazini mjini nimejaribu kuuza nyumba haiuziki wanunuzi wengi wanadai huku uswahilini sana.

Funzo: Vijana msikimbilie kujenga kama hamjajipanga.
Wala si kwamba haiuziki kwakuwa ni uswahilini kaka angu, bali uko nje ya mji kuuza nyumba inachukua muda, mi pia nilihama nikaipangisha nyumba huko, na nimetangaza kuuza muda tu inasumbua,, nilijenga uko kipindi Cha uvumi kwamba pakijengwa bandari patakuwa mjini, bas tulinunua viwanja na wenzangu kwa fujo, sasaivi tunajuta
 
Kwa Dar kwa mfanyakazi wa kawaida kutaka ujenge nyumba kiwanja utapata kilomita 40 au zaidi nje ya mji ujenge.

Mbaya zaidi ofisi nyingi ziko posta hivyo itakulazimu uwe unaamka sa 9 ili kufika ofisini sa 2, na kurudi nyumbani ukitoka sa 11 unafika sa 3. Hii sababu ni moja tu ya miundombinu mibovu kwa hapa Dar es salaam, barabara ya kuja na kutoka mjini ni zile zile hakuna njia mbadala na kama zipo ni za hovyo sana.

Mimi Dar siwezi kujenga, ni hasara tupu, ggharama za usafiri kutoka kwako hadi kazini ni zaidi ya 200,000 kwa mwezi, hujaja chakula, uusumbufu mwingine alafu niwe najisifu tu eti kisa nakaa kwangu.

Nenda kinyerezi, mbezi makabe, goba, mabwepande na kwenda huko Mapinga, mbweni, kitopeni, nk watu wametelekeza nyumba nzuri kule kwa sababu ya adha ya usafiri.

Bora upange jirani na mjini uishi kwa raha kuliko kua na kwako huku unaishi kwa shida kisa unaishi kwako. Kuna mshikaji wangu kajenga huko kimara porini imebidi akimbie nyumba, akapange apartment kariakoo.

Mimi nimepanga jirani tu na kazini kwangu, kilomita 8, hata sa 1:30 natoka kwangu na nafika kazini kabla ya ya 2:00 na maisha ni matamu sana.

Maisha ni hesabu, ukifanya miscalculation maisha yako yatakua magumu sana.

Hapa umenisema kabisa. Nimeacha nyumba kubwa nzuri Msumi nimerudi NHC Ubungo kodi laki mbili . Kule mafuta kwa mwezi laki nne bado foleni, kuchelewa kulala na kuwahi kuamka. Watoto huwaoni hadi weekend. Juu ya yote gharama za maisha bidhaa bei juu sana . Tufikirie sasa vertical building extension.
 
Mkuu soko la nyumba kwa sasa limeshuka sana kwa mfano kinondoni kwa pinda kuna nyumba mpaka za laki sita achilia mbali tabata achilia mbali makumbusho uko kote ni karibu na posta not less than 10 min upo kazini au nyumbani na muda wa kupumzisha akili ifikirie vitu vingine upo.
Kerege nadhani ata kama utakua na mafuta ya kuchoma kila siku bado nadhani hautakua na muda wa kufaid maisha kwa maana ya ya kwamba jioni ukifika homu itakua arrnd saa nne na kutoka hom asubuh ni saa 12 sharp hapo hamna maisha ni utumwa.
Panga hata chumba kimoja kino au sinza then ijumaa unarudi kerege and jumatatu anatokea atleast uifaid nyumba yako kipindi cha wknd
8 km from bagamoyo road ata mpangaji labda kama kuna mradi ndo utapata wapangaji otherwise supply ya nyumba mijini kwa ss ni kubwa mtu hana sababu ya kupanga nje ya mji
 
Mkuu uza hiyo gari tafuta Toyota hiace ya 15milion, Asubuhi unapokuja mjini beba abiria, unaporudi kerege pia beba abiria. weekend aamka asubuhi piga trip kazaa tegeta bagamoyo.. Hapo utakuwa umejiongezea kipato lakini pia utakuwa umepata hela ya mfuta kila siku ya kuendea kazini..

Ushauri mzuri pia...ww ni mtu wa 2/kuongea hv...kuna boda amenishauri hii kitu...kahama to ushirombo🤔!
 
Mkuu soko la nyumba kwa sasa limeshuka sana kwa mfano kinondoni kwa pinda kuna nyumba mpaka za laki sita achilia mbali tabata achilia mbali makumbusho uko kote ni karibu na posta not less than 10 min upo kazini au nyumbani na muda wa kupumzisha akili ifikirie vitu vingine upo.
Kerege nadhani ata kama utakua na mafuta ya kuchoma kila siku bado nadhani hautakua na muda wa kufaid maisha kwa maana ya ya kwamba jioni ukifika homu itakua arrnd saa nne na kutoka hom asubuh ni saa 12 sharp hapo hamna maisha ni utumwa.
Panga hata chumba kimoja kino au sinza then ijumaa unarudi kerege and jumatatu anatokea atleast uifaid nyumba yako kipindi cha wknd
8 km from bagamoyo road ata mpangaji labda kama kuna mradi ndo utapata wapangaji otherwise supply ya nyumba mijini kwa ss ni kubwa mtu hana sababu ya kupanga nje ya mji

Traveller hyo avatar ni wapi huko??mwe nimevutika...!
 
Back
Top Bottom