Najuta kujenga kibanda changu uswahilini. Mswahili ni mtu duni sana

Najuta kujenga kibanda changu uswahilini. Mswahili ni mtu duni sana

Wewe utakuwa umetoka familia maskini sana unamaindi hata vipolo jifunze kujali maskini utapata baraka zaidi
 
Umekua baba mlezi sasa
Mjukuu wa mwenye nyumba. 2 yrs old. Mimi naangalia sana katuni. First time nashangaa dogo huyo, nikamuuliza wewe nani akawa anataja jina ila simuelewi nikamtoa nje babu yake ndiyo akamtaja jina.

Naongea na babu yake yeye kasharudi ndani kwangu.

Sikuona tatizo. Balaa likaja kulilia remote, ukitaka kutoka anakuzuia, babu yake anasema niache funguo kwamba akimaliza kuangalia wafunge wanishikie funguo.

Nimelala nasikia hodi ya kugonga mlango kwa nguvu nafungua ni yeye, kaingia kafikia kujilaza kwenye kochi anasubiri tv. Namuambia mi nalala rudi baadaye ananijibu "Sitaki" hii wiki ya pili sijarudi nyumbani.
 
Ur a nice guy and I am not . A nice guy is after three things one of them is approval.

I don't want approval from any person.

I am an Alpha Male. Google that bro
So Google is your life guide line your book of moral and ethics?
 
Baada ya kujibanabana hatimae nikajenga kibanda changu uswahilini.

Jirani yangu ana mpangaji wake. Huyo mpangaji wake ana mtoto mdogo (4yrs). Mimi nina watoto watatu mmoja la Saba wa kike wawili wakiume (5) and (3).

Sio kwamba Mimi ni mchoyo na mbinafsi, la hasha! Ila hakuna kitu nakichukia katika maisha yangu kama vikwazo. Hii familia ya huyu mtoto mdogo inashindwa kumdhibiti mtoto wao wa kike (4yrs).

Msosi umeiva huyo kaibuka. Tatizo sio chakula. Anakuta watoto wangu wanakula nimewawekea nyama kila mtu na vipande vyake Kwa bajeti yeye huyo mtoto doezi anafika anachukua plate ya chakula anan'gan'gania kisha anaanza kulia eti hataki watoto wangu wale. Hapo mama ake yupo nje.

Siku nyingine anatoka huko kwao anakuja kunywa maji kwangu. Akiwa anakula na wanangu wakitaka kunywa maji analia anataka yeye ndio awe wa kwanza kunywa.

Kero kero zipo nyingi sana. Mimi nilikuwa sina habari hizo cause sishindi home. Last week nimerudi home mapema nakuta madogo ndio wametoka shule halafu eti huyo mtoto analia hataki wao wale chakula walicho andaliwa na dada kazi kwamba kidogo apewe yeye tu.

Na analia kwa nguvu kama kachomwa na mkuki vile. Hapo mama ake yupo nje. Huwa naambiwaga upuuzi huu but sikuwahi kushuhudia. Nikasema hawa wanafanya huu ujinga kwasababu wananiona nimekaa Kikristo sana.

Basi nilimchukua huyo mtoto nikamnyanganya hiyo plate nikamshika nje hadi kwa mama ake nikaanza kumchana mama ake.

"Wewe Mwanamke msiniletee maswala ya ki...nge. Kwangu sio kituo cha kulelea watoto. Mtoto wako anafanya us..nge humkanyi.." Kuanzia leo sitaki kumuona mtoto wako nyumbani kwangu.

It was a surprise for her kwasababu nadhani alikuwa ananiona nimekaa kisomi kisomi na anavyosikiaga naweka ngoma za gospel kwangu basi anajua huyo Mtakatifu Matayo.

Basi kuanzia siku hiyo adabu imekuwepo. Mazoea hakuna tena. On top of that nimeanza kuwa napiga kwa nguvu nyimbo za kigumu.

Ngoma kama Hit 'Em Up na nyimbo nyingine za kigumu gumu ili at least wajue huyu jamaa msela hataki mambo ya kidwanzi.

Majirani kushirikiana kwenye mambo mengine sio kukerana kerana kiasi hicho. Kama una njaa njoo ukope hela umpikie mtoto wako sio kumuacha aje awakere watoto wangu.

Toto lako kula kwangu halafu siku likipata tatizo si ndio mwanzo wa kushikana uchawi huo. Sisi ngozi chafu huwaga sio wastaarabu kabisa

Ngoja nitafute hela nipige Mwanaukome. Ndio maana matajiri wakijenga nyumba zao huwa wanazipiga stop nonsense

#Walayhi nimeona umuhimu wa kuoa. Ukiwa na mke majirani hawawezi kufanya upuuzi kwa sababu wanajua mama mwenye nyumba Hawezi kukubali. Ila wakiwa wanakuona kibachela bachela hivyo wanakuchukulia ki-gentleman sana.
Umewahi kwenda kuwapa msaada wa chakula watoto yatima?
Kuna wengi tunaishi nao mitaani, wanao wazazi lakini wana sifa zote za yatima.
 
ahahahaha sawa mkuu
 
aise mkuu,kati ya vitu sipendi kuona ni watoto wachafu,yani wazazi wengi wa uswahilini wanajisahau sana unakuta mtoto nguo zimetoboka,zina mikojo na matope dah huwa najiskia vibaya sana,najiuliza kwanini walizaa mtoto wakati hawawezi kumtunza.
umasikini sio sababu ya watoto wote kuwa wachafu,wengine ni wachafu kwa sababu ya uchafu wa mama zao

Mara nyingi wanawaacha watoto wakizurula hovyo. Nobody cares. Mara nyingi hawa wamama wengi wa uswazi wanapenda kukaa vijiweni kupiga soda na umbeya. Watoto wamewasahau.
 
Aissseee Roho za Kichoyo, Kichawi ndizo nazo Ziona kwenye Uzi huu,, Ni Hatari mtoto mdogo kula kwako imekuwa Tabu kweli Utanzania Umepotea mbona Misosi Ni issue za Kawaida Sana alafu hayoo Ni Mambo ya Kike.
 
Nope sio uchumi. Mimi sitaki watoto wangu wasumbuliwe. My family is a nuclear family. Nataka nikiwa nakula niwe nimekaa kwenye meza moja Mimi na watoto wangu damu yangu.. sitaki allien nyumbani kwangu.. wanawafundisha watoto wangu tabia mbaya na kuwakwaza.

Imagine toto linakuja linakuta watoto wangu wanakula halafu linashikilia plate linaanza kulia. That's amount to child abuse.
Kwamba utaki Allien kwako, haki nimecheka hatari
 
kikubwa hapa Duniani tunapita tu kesho unaweza ukawa haupo watoto wako watazurura watamkuta baba wa mtoto huyo atawatendea hivyo hivyo
 
Magu legeza ,

Wababa wanakuja kufungua nyuzi kwasababu ya finyango mbili za nyama.
Mkuu, kama hizo kero hazijakupata temea chini na ushukuru Mungu.

Yawezakuwa mazingira ulipoanzia maisha na hadi ulipofikia sasa, haujapambana ama kushuhudia.

Huyu mtoa mada kaandika kwa ku 'highlight' maisha ya kishenzi ya uswahilini hasa.

Leo wewe unaona mwenziyo kama mchoyo flani, kumbe anachotaka ama alichokieleza hapo ni kutetea uhuru wake binafsi na wa familia yake.

Ni hivyo tu, kila mtu anahitaji faragha.
Na kama ni kutoa kitu, iwe chakula ama chochote kile, mtu ni lazima ajipange katika nafsi yake na siyo kuingiliwa, kushinikizwa ama kufosiwa.

Na mazoea ya hovyo kwa jirani ama mpangaji mwenzako, ndiyo kero zenyewe zinazojadiliwa humu.

Kila mtu aishi kwa faragha zake, kusaidiana ni jambo la heri hakukatazwi.

Sijui kama utakuwa umenielewa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja:

Wengi wa sisi tunapenda kuvunga ili tusionekane tuna rohombaya, mimi kama mswahili nimekuelewa sana, unajaribu kulinda uhuru na furaha ya wanao.
Tatizo hapa sio jamaa wala sio mtoto,tatizo ni mzazi wa mtoto ambaye hashughuliki na kumuongoza mwanae.

Enzi 2009 tulikuwa tunaishi uswahilini mbagala na mama na wadogo zangu wawili, ilikuwa ikifika mida ya misosi, kuna dogo wa jirani 3 yrs unakuta kafika, tukawa tunaichukulia kawaida daily.

Kuna siku ilikuwa jumapili bwana nilikuwa dirishani natoatoa vumbi kama mishale ya saa saba kasoro mchana, hili dirisha ndio linaloangalia kwa jirani.

Basi buana huku naendelea na usafi mara bi mkubwa na madogo wakaniita sign ya kuwa msosi tayari, sikuamini pale nilipoona yule jirani anamtoa yule mwanae ndani na kumuelekeza akimbie haraka kuelekea home ili aje afinye.

Hapo tatizo ni mama wa mtoto, na sio kama alikuwa hana uwezo wa kumlisha, maana mumewe alikuwa dereva wa mikoani na akirudi anamletea ma misosi kama yote.

Tatizo uswahilini kuna ubinafsi hatujali kama kitu kinaweza kuwa kero kwa mwingine or no.
 
aise mkuu,kati ya vitu sipendi kuona ni watoto wachafu,yani wazazi wengi wa uswahilini wanajisahau sana unakuta mtoto nguo zimetoboka,zina mikojo na matope dah huwa najiskia vibaya sana,najiuliza kwanini walizaa mtoto wakati hawawezi kumtunza.
umasikini sio sababu ya watoto wote kuwa wachafu,wengine ni wachafu kwa sababu ya uchafu wa mama zao

Aisee, hii ni kero kubwa sana
Kuna kipindi niko zangu na geto mitaa ya temeke, jirani yangu alikuwa na mtoto ndio anatembea, basi dogo anapenda radio unakuta anakuja room mara abonyeze bonyeze,siku kaja kavuta ka HP kangu kakapiga chini kakaharibika screen nikakausha, ukimtoa analia afu maza ake haata hatilii mkazo wa ku take action ya kumzuia

Kero zaidi ni kwamba dogo alikuwa havalishwi hata pampers ,ananuka mikojo au unakuta anakuja room mara kakojoa au anajinyea, unaanza kufuta maana huwezi ruhusu mama ake aje ndani kwako kufuta vinyesi vya mwanae.

Nilipoona kero inazidi nikaanza kukaza sasa, dogo akija namtoa nje nafunga mlango, ataliaa hapo atapigapiga mlango mama ake hana habari, pale ndio naposhangaaga.
 
Back
Top Bottom