Najuta kujenga kibanda changu uswahilini. Mswahili ni mtu duni sana

Najuta kujenga kibanda changu uswahilini. Mswahili ni mtu duni sana

Mjukuu wa mwenye nyumba. 2 yrs old. Mimi naangalia sana katuni. First time nashangaa dogo huyo, nikamuuliza wewe nani akawa anataja jina ila simuelewi nikamtoa nje babu yake ndiyo akamtaja jina.

Naongea na babu yake yeye kasharudi ndani kwangu.

Sikuona tatizo. Balaa likaja kulilia remote, ukitaka kutoka anakuzuia, babu yake anasema niache funguo kwamba akimaliza kuangalia wafunge wanishikie funguo.

Nimelala nasikia hodi ya kugonga mlango kwa nguvu nafungua ni yeye, kaingia kafikia kujilaza kwenye kochi anasubiri tv. Namuambia mi nalala rudi baadaye ananijibu "Sitaki" hii wiki ya pili sijarudi nyumbani.
Mtie vibao na ww
 
Habar za weekend zangu JF .
Kwa jinsi maisha yanavyokwenda kasi zaid ya ile ya mwanga haya ni baadhi ya mambo ambayo hutakiwi kupitia na kama umepitia basi hakikisha hurudii.

1. Matumizi mabaya ya pesa
2. Kusoma ndio maisha
3. Kukata tamaa bila kujaribu
4. Kukubali kila unachosikia/ambiwa
5. Kuwekeza bila utafiti
6. Kutaka/kufanya Mambo mengi kwa wkt mmoja
7.Kutokuchagua mtu sahihi ktk mahusiano yako.

Karibuni kuchangia pamoja tupeane madini kuna watu walisha experience ayo mambo unaweza kuongezea nyama.
Baada ya kujibanabana hatimae nikajenga kibanda changu uswahilini.

Jirani yangu ana mpangaji wake. Huyo mpangaji wake ana mtoto mdogo (4yrs). Mimi nina watoto watatu mmoja la Saba wa kike wawili wakiume (5) and (3).

Sio kwamba Mimi ni mchoyo na mbinafsi, la hasha! Ila hakuna kitu nakichukia katika maisha yangu kama vikwazo.

Hii familia ya huyu mtoto mdogo inashindwa kumdhibiti mtoto wao wa kike (4yrs).

Msosi umeiva huyo kaibuka. Tatizo sio chakula. Anakuta watoto wangu wanakula nimewawekea nyama kila mtu na vipande vyake Kwa bajeti yeye huyo mtoto doezi anafika anachukua plate ya chakula anan'gan'gania kisha anaanza kulia eti hataki watoto wangu wale. Hapo mama ake yupo nje.

Siku nyingine anatoka huko kwao anakuja kunywa maji kwangu

Akiwa anakula na wanangu wakitaka kunywa maji analia anataka yeye ndio awe wa kwanza kunywa.

Kero kero zipo nyingi sana. Mimi nilikuwa sina habari hizo cause sishindi home. Last week nimerudi home mapema nakuta madogo ndio wametoka shule halafu eti huyo mtoto analia hataki wao wale chakula walicho andaliwa na dada kazi kwamba kidogo apewe yeye tu.

Na analia kwa nguvu kama kachomwa na mkuki vile. Hapo mama ake yupo nje.

Huwa naambiwaga upuuzi huu but sikuwahi kushuhudia.

Nikasema hawa wanafanya huu ujinga kwasababu wananiona nimekaa Kikristo sana.

Basi nilimchukua huyo mtoto nikamnyanganya hiyo plate nikamshika nje hadi kwa mama ake nikaanza kumchana mama ake.

"Wewe Mwanamke msiniletee maswala ya ki...nge. Kwangu sio kituo cha kulelea watoto. Mtoto wako anafanya us..nge humkanyi.."

Kuanzia leo sitaki kumuona mtoto wako nyumbani kwangu.

It was a surprise for her kwasababu nadhani alikuwa ananiona nimekaa kisomi kisomi na anavyosikiaga naweka ngoma za gospel kwangu basi anajua huyo Mtakatifu Matayo.

Basi kuanzia siku hiyo adabu imekuwepo. Mazoea hakuna tena.

On top of that nimeanza kuwa napiga kwa nguvu nyimbo za kigumu.

Ngoma kama Hit 'Em Up na nyimbo nyingine za kigumu gumu ili at least wajue huyu jamaa msela hataki mambo ya kidwanzi.

Majirani kushirikiana kwenye mambo mengine sio kukerana kerana kiasi hicho.

Kama una njaa njoo ukope hela umpikie mtoto wako sio kumuacha aje awakere watoto wangu.

Toto lako kula kwangu halafu siku likipata tatizo si ndio mwanzo wa kushikana uchawi huo.

Sisi ngozi chafu huwaga sio wastaarabu kabisa

Ngoja nitafute hela nipige Mwanaukome.

Ndio maana matajiri wakijenga nyumba zao huwa wanazipiga stop nonsense

#Walayhi nimeona umuhimu wa kuoa. Ukiwa na mke majirani hawawezi kufanya upuuzi kwa sababu wanajua mama mwenye nyumba Hawezi kukubali. Ila wakiwa wanakuona kibachela bachela hivyo wanakuchukulia ki-gentleman sana.
Mpende jirani yako kama nafsi yako
 
kuna jirani aliwahi nisumbua mpaka nikahama uswazi, yaani yeye daily kukicha familia yake anaisukumiza kwangu alafu nikirud jion nakuta mahtaj yamepungua akati niliacha pesa yakutosha, wife aliponambia huo ujinga nikamwambia kwa nini usimwambie mama yao eti anaogopa kero na jirani, kilichofuata nilimfuata nikamweleza yule mama...

baada yakumwambia akaanza visa kila siku mapaka dirishani na juu ya nyumba, ikanibidi nifanye mchakato wa kuhama uswaz.
Washenzi sana hawa watu
 
Huu uzi mpaka comments umenichekesha sana, utadhani masihara kumbe the movie is real.

Ila naomba nikuulize mkuu swali moja, una watoto 3 unaishi na house girl mama zao uliachana nao.
Swali.

How possible kila mwanamke unamuoa then unaachana nae??
Kupata watoto NI lazima uoe ?
 
Na ww unaonekana mswahili huna haja ya kupiga vijembe kupitia muziki ili wakuelewe!!
mm kama ningekuwa ww. Na nina hela huyo mtoto wa jirani angekuwa anakuta nimemuwekea mabakuli ya nyama.
Kama unajua kuna mtoto anafwata wanao na yeye muweke kwenye bajeti period! Ila sio sawa kumfukuzia mtu tena mtoto chakula.
Labda me ndio mshamba ila ishu za mamsosi huwaga sinaga shobo nazo kumbania mtu.
Leo umekula nyama kesho kinahotoka hata kukiona hutaki kishakuwa takataka
 
Ungetumia hekima ya watu wa pwa i tu unapamkulia unampelekea kqao kila unapojisikia kufanya hivyo na dsiku usipopeleka "hawawezi"kuja kukugongea.

Maana iko wazi hapo lishe tabu tu na umaskini kwa mtoto haujifichi msaidie jirani baba usiwe na roho ya choyo she is 4yrs old show them love utaweza kum control na atakuwa na adabu tu.

Chuki mbaya kwa watoto ni mbaya mno na ni laana
Hawana umasikini wa kukosa hela ya Kula mama ake anauza chapati na Baba ake anapiga mishe zake town.

Nimpelekee chakula kwao halafu ale afe ionekane nimumewekea sumu Mimi. Mzee vp mbona unanishauri vitu vya kitoto hivyo?
 
Kama unajua kuna mtoto anafwata wanao na yeye muweke kwenye bajeti period! Ila sio sawa kumfukuzia mtu tena mtoto chakula.
Labda me ndio mshamba ila ishu za mamsosi huwaga sinaga shobo nazo kumbania mtu.
Leo umekula nyama kesho kinahotoka hata kukiona hutaki kishakuwa takataka
Halafu mtoto wa watu akipata madhara ionekane wewe ndio umemdhuru? Katika vitu unavyo takiwa kuwa navyo sensitive katika maisha yako basi NI chakula kinachopikwa nyumbani kwako na akina Nani wanao Kula chakula hicho.

It seems like u have a very little understanding about waswahili
 
Malezi ya hovyo sie mbona tukikuwa hatuli kwa watu ovyo ovyo nakumbuka mpaka bibi yetu alikuwa anatuletea chakula nyumban
Ndio maana nashangaa huyu jirani yangu
 
Nikikujibu utasema nikupe authority nikikwambia authority NI kamusi utaniuliza tena kamusi nini.

Naomba nichague kutokukujibu
sawa,,,, japo hili swali sikulielekeza kwako. nilimquote sbd else!
 
Kaka familia yako sio kubwa sana, pangisha nyumba kisha kapange ushuani uishi kwa amani. Uswahilini hakuna anayepaweza daima. Hapo subiri kulogwa
 
Kaka familia yako sio kubwa sana, pangisha nyumba kisha kapange ushuani uishi kwa amani. Uswahilini hakuna anayepaweza daima. Hapo subiri kulogwa
Nimezaliwa uswahilini nimekulia uswahilini. Matter fact nimezaliwa huku huku na hicho kiwanja nilicho jenga ni share ya urithi WA Mshua.

Kuna nyumba nyingine kubwa imejengwa Kiswahili inavyumba na sebule Choo jiko na bafu kama nane hivi niliachiwa na Mshua hiyo nimeipangisha na nimeweka tangazo NI marufuku Kwa watoto WA jirani au MKE WA jirani kuingia ndani ya chumba cha mpangaji mwenzake

Hakuna mchawi anaweza kuniroga mimi
 
Kwanza ni kosa kumlisha mtoto wa mtu kwako bila uwepo wa wazazi wake. Iwe ulaya, au uswahilini, usiwe unapenda kulisha watoto wa watu.

Muda wa msosi ukikaribia kasindikize kwao, na kasikuletee mazoea hapo ya kuwabana watoto wako wasienjoy mema ya baba yao......
Moderator naomba mui ongeze comment hii Chini ya Uzi wangu kama moja Kati ya comments Bora kabisa Chini ya Uzi huu.

Ur the true son of Ur father
 
Sina MKE bro Mimi ni msela. Hawa watoto kila mtu na mama Yao. Sipendi tu watoto wangu kufanyiwa kero. Toto linakuja na mikono yake michafu huko halijaogeshwa linanuka mikojo linakuja kusumbua watoto wangu.

aise mkuu,kati ya vitu sipendi kuona ni watoto wachafu,yani wazazi wengi wa uswahilini wanajisahau sana unakuta mtoto nguo zimetoboka,zina mikojo na matope dah huwa najiskia vibaya sana,najiuliza kwanini walizaa mtoto wakati hawawezi kumtunza.
umasikini sio sababu ya watoto wote kuwa wachafu,wengine ni wachafu kwa sababu ya uchafu wa mama zao
 
aise mkuu,kati ya vitu sipendi kuona ni watoto wachafu,yani wazazi wengi wa uswahilini wanajisahau sana unakuta mtoto nguo zimetoboka,zina mikojo na matope dah huwa najiskia vibaya sana,najiuliza kwanini walizaa mtoto wakati hawawezi kumtunza.
umasikini sio sababu ya watoto wote kuwa wachafu,wengine ni wachafu kwa sababu ya uchafu wa mama zao

Inakera Sana. Na uchafu ndio Alama kuu ya mswahili
 
Back
Top Bottom