Najuta kumpa ndugu yangu PS (playstation), kawa kama Teja

Najuta kumpa ndugu yangu PS (playstation), kawa kama Teja

Kuna madogo hapa nyumbani walinidanganya walisema anko tununulie PS tunaweka CD za masomo and bla bla pia Kuna games za hesabu na nini kumbe Yananipiga kamba Sasa na uzee huu nikazama mfukoni wakaenda kununua aisee kila siku yanalala saa Saba ukipita karibu na chumba Chao unasikia tu Mara Ronaldo with the ball..nampango wa kuichukua kuifungia chumbani

Unamsikia tu Martin Toiler😂😂
 
Kuna madogo hapa nyumbani walinidanganya walisema anko tununulie PS tunaweka CD za masomo and bla bla pia Kuna games za hesabu na nini kumbe Yananipiga kamba Sasa na uzee huu nikazama mfukoni wakaenda kununua aisee kila siku yanalala saa Saba ukipita karibu na chumba Chao unasikia tu Mara Ronaldo with the ball..nampango wa kuichukua kuifungia chumbani
[emoji1787]
 
Mkuu ni freemason na agenda zao za siri. Walianzisha haya magemu kimaksudi tu. Haya ma whatsapp TikTok, fb, tinder l, mastercard, visa, visa electron, fifa, worldcup, epl, dstv, KFC, McDonald's, Netflix, western union etc ni wao. Yani freemason wanavuruga sana akili za madogo. Haya magemu ya ps Smart911 anayajulia sana.
[emoji23]🫙
 
Mimi ilikuwa game boy enzi zile ilikuwa ya mshikaji hivi mwarabu kitaa na alikuwa ananiachia napenda kucheza spider man. Bahati mbaya ps siijui vizuri ila dogo langu ndo yuko fresh noma anashiriki mpaka mashindano ila naona kama miaka mitatu kaacha yuko busy na masomo..
 
Bado wanasoma wapo kidato Cha pili suluhu Ni kuipokonya tu Kama ina huo uraibu nitawafanyia shambulio la kushtukiza wakiwa katikati ya mchezo
Matokeo darasani vp?

Uzuri wa hii ps unaweza kuifanya kama fimbo, wakizingua kitu flan huwachapi wala kuwagombeza, unawafanyia shambulizi za kustukiza wakiwa katikati ya mchezo unaibeba unaifungia ndani hata siku 2, wakirudia unaifungia hata wiki.. Ile raha ya kucheza wanapoikosa inakuwa ni adhabu nzito kwao.
 
Matokeo darasani vp?

Uzuri wa hii ps unaweza kuifanya kama fimbo, wakizingua kitu flan huwachapi wala kuwagombeza, unaxhukua ps unaifungia ndani hata siku 2, wakirudia unaifungia hata wiki.. Ile raha ya kucheza wanapoikosa inakuwa ni adhabu nzito kwao.
Matokeo Ni mazuri tu so far, Sasa in a long run isije ps ikawagharimu au niwe nawapa Jumapili tu ndio waitumie
 
Niliwahi kununua playstation Kwa mwanafunzi flan hivi wa chuoni alikuwa anadaiwa ada na hana pesa, aliniuzia hio mashine Kwa laki 3 na nusu, lengo langu lilikuwa niiuze hata kwa laki 5 maana hii mashine inauzwa takribani laki 8 madukani, kazi zilinitinga nikawa nimeiweka tu sebleni.

Sasa Kuna ndugu yangu huyu kamaliza form 4 mwaka jana anaenda kuanza chuo mwezi huu alikuja kunisalimia mwezi wa 7 hivi, aliiona hio ps na akaanza kuitumia, ilibidi akae siku 4 lakini game lilimnogea alikaa wiki, anavyoondoka aliniomba sana nimpe mashine, nikampa ila nikamwambia aitunze atairudisha akienda chuo.

Mwezi uliopita nimepigiwa simu na mama yake analalamika nimemuharibu mtoto wake, muda mwingi anacheza ps, kulala saa Saba usiku, kapoteza umakini na kawa kama Teja .

Ilibidi mama yake amnyang'anye hio ps kaifungia sehemu anayoijua yeye kaniambia siku nikiihitaji atanisafirishia.

Baada ya kufungiwa hio ps dogo akaanza kwenda kucheza kwa rafiki zake wenye ps, mda ambao marafiki zake hawapo kaanza kwenda kwenye frem za mtaani wanazochezesha ps kwa hela

Sasa huku kwenye frem wanazochezesha ps huwa wanalipia pesa kwahio dogo kaanza kuiba Hela nyumbani Ili aende kucheza, kukiwa hakuna pesa anaweza kuuza vitu vidogo vidogo, baba yake alipogundua alimtembezea kipigo cha haja lakini bado hasikii
Dogo anahitaji tiba ya saikolojia Japan kuna soba houses za waraibu wa social media...
 
Matokeo Ni mazuri tu so far, Sasa in a long run isije ps ikawagharimu au niwe nawapa jumapili tu ndio waitumie
Kama matokeo mazuri waachie tu watoe ushamba.

Hizi ps huwa Kuna kipindi kinafika zinazoeleka.

Kwa Sasa itumie iwe kama kifaa cha adhabu, unaweza kuwapa kazi flani wasipoifanya unaifungia ps, makosa madogo madogo unaifungia hata siku 1 ama 2, makosa mazito dozi inaongezwa
 
Kama matokeo mazuri waachie tu watoe ushamba.

hizi ps huwa Kuna kipindi kinafika zinazoeleka.

Kwa Sasa itumie iwe kama kifaa cha adaabu, unaweza kuwapa kazi flani wasipoifanya unaifungia ps
[emoji106]
 
Back
Top Bottom