Najuta kumsaidia rafiki yangu huyu

Najuta kumsaidia rafiki yangu huyu

Tukuulize wewe,

Hivi unachojutia haswa ni kipi? Kujuta unajua maana yake? Disappointment ni jambo la kawaida.

Kampuni ita-extend muda wa kutafuta mfanyakazi. Wapo wengi sana mtaani.

Jamaa yako hata angetuma CV na makorokocho yote, pengine angeharibu mbeleni. Na lawama pamoja na gharama zikakuangukia wewe.

There is nothing to regret. Vinginevyo ulikuwa na percent yako, imekupita kando.
Sawa mkuu, mi sina percentage yoyote hapo😀.
 
Nimeamua kuandika Uzi huu, ili vijana tukumbushane kutumia Fursa kwa muda muafaka baada ya kufanyiwa uhuni na rafiki yangu mmoja(x).

Ndugu yetu huyu (x) amekuwa na tabia ya kulalamika kuwa Hali ni ngumu, na hivyo tumfanyie mpango wa yeye kupata ajira au kazi yotote itakayo msaidia.

👉Hazikupita siku nyingi, ndugu yangu mmoja katika utafutaji(huyu tumuite y) Ali nipigia simu na kuni julisha juu ya uwepo wa nafasi ya kazi katika kampuni moja ya uuzaji wa rangi.

Nami nikaona sio vibaya, niki mpigia pande rafiki yangu x (kosa kubwa 🙉). Basi nikamjulisha Kaka (y) kuwa kuna rafiki yangu mmoja ana weza akafaa kwa nafasi hiyo.

👉Aka nihoji Kama namfahamu vizuri??, Je ni muaminifu, muadilifu??. Nikajibu ndio na kummwagia sifa Kama zote x.

Kaka (y) aka nipa taratibu zote ambazo zilipaswa kufuatwa, ili Jamaa yetu huyu apate nafasi hiyo ya kazi.
👉 Kijana x, ali paswa aandae wasifu mdogo(mfano wa CV) aki elezea yeye ni Nani?

👉Ana omba kazi kitengo kipi??( Kitu kimoja alicho ambiwa kaka y), nafasi hii ime tolewa kwa ajili ya kijana ambaye ata kuwa Kama ana tumika kufanya baadhi ya deal( so akiwa smart ita mtoa).

👉kijana anaye omba nafasi hiyo, alikuwa na siku 2 za kutuma wasifu huo. Hivyo Ali paswa autume haraka.

Kisha ajiandae na interview, ambayo ange pita bila kipingamizi chochote.
👉kwa maana ya kwamba mtu anae wafanyia interview, alikuwa ana taarifa zake zote. Hivyo ni suala la kukamilisha taratibu tu.

Kijana (x) aka pewa taarifa zote na utaratibu anao paswa kufata, kwa bashasha na kujiamini akasema haita chukua hata nusu saa(30) ata kuwa Kama liza.

👉Cha kushangaza siku nzima ikaisha, pasipo kijana kufata taratibu alizo pewa.

Nikapigiwa simu na Kaka (y) Aki niuliza mbona mpaka Sasa Hakuna kitu kilicho fanyika?

Kaka (y)Aka niomba nimpe namba za simu za kijana (x), ili aweze kuwasiliana nae ajue kakwama wapi?

👉Kijana (x) kupigiwa simu aka Anza kutoa sababu za ajabu na kipuuzi, eti Sina nauli ya kwenda sehemu hiyo ya kazi(🤐).

👉Kaka (y) aka muambia nauli sio tatizo, Kikubwa tuma wasifu wako sehemu husika.

Siku ya 2, ika Isha kijana (x) haja fanya Kama alivyo elekezwa, na kibaya zaidi haku nipigia simu mimi Au kumtafuta Kaka y).

👉Nika amua nichukue jukumu la kumtafuta kijana (x), sababu alizo nipa ni kuwa hakuwa na bundle la internet hivyo Ali shindwa kutuma wasifu(cv).

Mpaka Sasa kijana x, haja mtafuta kaka (y) angalau kuomba msamaha au kujutia kwa kitendo Cha kihuni alicho kifanya.

👉Sasa naji uliza vijana tuta fika kwa mtindo wa kihuni wa Aina hii?

👉Ungekuwa wewe, unge chukua maamuzi yapi??

I mean no to nobody
View attachment 2734711
Nirahisi sana ku jump in conclusion,

Hivi unajua gari la automatic ukiweka D unaendesha, lakini kama hujui kuendesha gari ukiwekewa D huwezi kuliendesha. Mfano huu unakuhusu wewe uliyeamua kumsaidia rafiki yako
 
Kaza tako basi.

Wewe unashindwa nini kumplease jamaa yako ili usipoteze uaminifu wako kwake?

Wewe unataka uombwe radhi, ila hutaki kuomba radhi. Duh!

Huna sababu ya kumlalamikia jamaa.
Mkuu matusi ya nini, au ndo utaratibu wanao utumia hapo kwenu 🤔.
👉Mimi ndo Nisha malizana na Jamaa aliye toa mchongo.
👉 Tatizo like Baki kwa ndugu yetu, na hatu mfikirii Sana.
 
Mkuu matusi ya nini, au ndo utaratibu wanao utumia hapo kwenu 🤔.
👉Mimi ndo Nisha malizana na Jamaa aliye toa mchongo.
👉 Tatizo like Baki kwa ndugu yetu, na hatu mfikirii Sana.
Unamfikiria sana. Mpaka unamuanzishia uzi huku unalalamika inadhihirisha wazi.

Niwie radhi.
 
Jifunze tu,mimi nimeamua kila mtu apambane kivyake simtafutii tena mtu kazi,yaani mtu unamtafutia kazi kwa shida zake alafu badae we ndo unaanza kusota yaani kila lawama kazini inakuja kwako,nimekoma nimekoma kila mtu apambane kivyake,hata sisi tulisota hayakuja ghafla

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Jifunze tu,mimi nimeamua kila mtu apambane kivyake simtafutii tena mtu kazi,yaani mtu unamtafutia kazi kwa shida zake alafu badae we ndo unaanza kusota yaani kila lawama kazini inakuja kwako,nimekoma nimekoma kila mtu apambane kivyake,hata sisi tulisota hayakuja ghafla

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
Nime kuelewa mkuu
 
Back
Top Bottom