Najuta kumtia umasikini Mama yangu

Najuta kumtia umasikini Mama yangu

Hakuna kitu kina replace thamani ya mtoto Kwa mama.... mtoto wako thamani yake anaijua aliyemzaa na wewe...ngoja nikupe swali la kizushi, what if umeshakufa halafu inakuja kujulikana kabisa Kwa vinasaba huyo mtoto kumbe ulipewa tu zawadi kumbe ni wa Denis? 😁😁😁
🤣🤣🤣 nitafufuka nigombanie kombe jokes 🤣🤣🤣 kesi ngumu hiyo mpenzi ila kifo ni kifo...japo nimekuelewa sana​
 
I feel you brother..pambana bila kuchoka. Usimlaumu yeyote.take full responsibility of your life
Shukrani sana ndugu yangu. Japo napambana sana ila ndio hivyo nakuwa kama nimesimama...!
 
Mkuu wewe Si unafanya Kazi Garda na unalipwa 750k ,,,tumia huo mshahara kutoboa ..
 
Una ujuzi wa kuandika articles? Mfano nikikwambia andika kuhusu vituo vya mabas Dar es salaam na route zake? Ruksa kufanya utafiti online, ila ziwe authentic... Unaweza?
Ninaweza...! Nilisoma uandishi full...video editing. Camera operating. Japo sijabezi kabisa kwenye habari za michezo...!
 
Pole sana.
Usipende kujiingiza kwenye mafanikio ya mtu mwingine.
Huna uwezo wa kumfanikisha wala kumsaidia mwingine.
Mwenye uwezo huo ni Mungu.

Kama Mungu hajataka kukutumia kumsaidia au kumfanikisha Mama yako kosa lako liko wapi?

Hakuna yeyote ambaye unaowajibu wa kumsaidia au kumfanikisha zaidi ya mtoto uliyemzaa wewe. Full stop.

Yaliyotokea kabla ya wewe kuwepo hayakuhusu na huna uwezo nayo.

Wewe pambania Maisha yako ukiyaweza ndio ufikirie ya wengine. Vinginevyo utakufa Maskini kama wanavyokufa wengine
 
Labda niseme ukweli ,hakuna kipya hapa.

ulichokiandika ,ndio hali halisi ya vijana wengi wa kitanzania ,amka pambana . pole sana na huruma za jf hazitokusaidia!

kama ni Ke -i feel ure pain
kama ni me - we belong the same pain pambana chief utapata.

tushakula blueticks sana kwa ndugu,jamaa na marafiki.

Ahsante MUNGU kanitoa juani
Ahsante mama Samia kanitoa street
Toto la mama samia, niaje kipande cha huko? Maana bila huyu mama sijui ingekuwaje.
 
Mimi ni kijana Ambae nimezaliwa mwanzoni mwa mwaka 1990. Hapa hapa kwenye jiji la MAKONDA. Japo Baba na Mama yangu Kila mmoja ni mwenyeji wa mkoa wake.

Mama yangu alibahatika kusoma Hadi darasa la 7. Alifanikiwa kusoma typing enzi hizo ilikuwa hot sana kozi hiyo kama ilivyo computer siku hizi. Alisomeshwa hiyo kozi ili atafutiwe kazi ukizingatia kuwa mjomba wake alikuwa na cheo kikubwa TU wizara ya AFYA {R.I.P BABU}

Bahati haikuwa yake kwani katika harakati hizo za kutafutiwa kazi ikagundulika kuwa yeye Mama ni mjamzito. Hapo ndipo maisha yake yalipoanza kuwa ya kawaida nadhani mimba hiyo ilimtoa kabisa kwenye reli😭😭😭

Wenzie aliosoma nao enzi hizo Wana maisha mazuri na majina makubwa mfano Mtendaji mkuu wa NMB. Mh Ruth Zaipuna amesoma na mama yangu darasa Moja.

Nisingekuwa mimi kuja Duniani pengine mama yangu hivi sasa angekuwa mbali sana kimaisha.

Ujio wangu hapa Dunia umefanya mama amekuwa na maisha ya kawaida sana. Amehangaika sana na kwa kiasi Fulani Bado ananihangaikia😭😭😭

Nina huzuni sana licha ya kuwa nimesoma lakini elimu yangu haijanisaidia. Ni kama ubongo wangu umefungwa minyororo nashindwa Cha kufanya😭😭😭

View attachment 2808722

Na umri wangu huu nikiumwa ikahitaji milioni 1 TU haki vile nitakufa huku najiona. Umri wa mama yangu unaenda Kwa Kasi itafikia kipindi ataitaji msaada wangu.

Na Mimi Bado najitafuta japo namuomba sana Mungu anisaidie nijipate haraka. Na Nina muomba sana Mungu asimchukue mama yangu kabla sijajipata. Na ni Bora anichukue Mimi kwanza japo natamani sana siku Mungu atakayonichukua anichukue nikiwa nimemuacha Mama yangu pazuri 😭😭😭

Mwenzenu najuta sana kumpa mama yangu UMASIKINI​
Sasa wewe unajuta kwa lipi, na wakati starehe walifanya wazazi wako! Mbona unataka kuchanganya watu!!
 
Sidhani kama ajutii japo aniambii ila dah. Inatia hudhuni imagine marafiki zangu niliosoma nao 75% wanaajira zinazoeleweka.

Inafikia kipindi mama nikimpigia simu ananiambia mtafute rafiki yako Fulani pengine anaweza kukuunganishia kazi.

Huku huyo rafiki yangu nikiwa Sina mawasiliano nae yoyote SI unajua tena Kila hatua mtu anayo piga anakuwa na marafiki wapya.

Nina miaka 30+ lakini Bado 75% ya maisha yangu IPO mikononi Kwa mama.​
Baba kafa au?
 
Back
Top Bottom