Najuta kumtia umasikini Mama yangu

Najuta kumtia umasikini Mama yangu

Huwezi.jua,ukipata labda utakufa kifuani kwa Malaya,hebu jaribu kuanzisha kitu ukipendacho.
Kwenye umalaya Mimi sipo kwasababu huo umalaya Kwa kiasi Fulani umeibomoa sana familia yetu. Hadi Leo hii nimekuwa mtu wa kulaumu. Ndio maana kwenye andiko langu hili hujaona sehemu nimemtaja BABA. isingekuwa yeye kuendekeza chini Leo hii Mimi pengine ningekuwa kwenye nafasi nzuri TU😭😭😭

Kwa hiyo Mimi Nina uchungu siwezi kuendekeza chini. Japo napapenda ila Kwa mtu mmoja TU🤣🤣🤣​
 
Kuna muda wa kina baba Huwa wanakosea sana. Hivyo kwakuwa nimeamua kujilaumu mwenyewe sijapenda sana kumzungumzia baba kwasababu ingepelekea Mimi kumlaumu.

Itoshe TU kusema kuwa Kuna vitabia vya kiarabu ambayo vimekuja kututia UMASIKINI sana sisi waafrika. Yani hatujaona jambo jema kuliiga Zaidi ya kuoa wake wengi. Mwisho wa siku familia inamshinda😭😭😭

Mkuu Nina mengi ya kuzungumza ila Leo nilitaka kujilaumu mwenyewe ili nisinge mbele.​
Tatizo ni kutomshirikisha baba yako kwenye lawama zako. Nyie watoto mliolishwa maneno ovu na mama zenu siku zote mnawachukulia baba zenu kama hamnazo.

Na mtaishia pabaya siku zote.

Imeandikwa waheshimu Baba na Mama yako upate heri na siku nyingj duniani.
 
Si ndio hapo sasa

Kina baba wako underrated kinyama....sio fair
Na unaweza kukuta huu uchovu alio nao umechangiwa na kiburi alicho nacho cha kumpuuza baba.

Watoto wa mama wana tabu sana. Hata kutongoza anaomba ushauri kwa mama.
 
Mimi ni kijana Ambae nimezaliwa mwanzoni mwa mwaka 1990. Hapa hapa kwenye jiji la MAKONDA. Japo Baba na Mama yangu Kila mmoja ni mwenyeji wa mkoa wake.

Mama yangu alibahatika kusoma Hadi darasa la 7. Alifanikiwa kusoma typing enzi hizo ilikuwa hot sana kozi hiyo kama ilivyo computer siku hizi. Alisomeshwa hiyo kozi ili atafutiwe kazi ukizingatia kuwa mjomba wake alikuwa na cheo kikubwa TU wizara ya AFYA {R.I.P BABU}

Bahati haikuwa yake kwani katika harakati hizo za kutafutiwa kazi ikagundulika kuwa yeye Mama ni mjamzito. Hapo ndipo maisha yake yalipoanza kuwa ya kawaida nadhani mimba hiyo ilimtoa kabisa kwenye reli😭😭😭

Wenzie aliosoma nao enzi hizo Wana maisha mazuri na majina makubwa mfano Mtendaji mkuu wa NMB. Mh Ruth Zaipuna amesoma na mama yangu darasa Moja.

Nisingekuwa mimi kuja Duniani pengine mama yangu hivi sasa angekuwa mbali sana kimaisha.

Ujio wangu hapa Dunia umefanya mama amekuwa na maisha ya kawaida sana. Amehangaika sana na kwa kiasi Fulani Bado ananihangaikia😭😭😭

Nina huzuni sana licha ya kuwa nimesoma lakini elimu yangu haijanisaidia. Ni kama ubongo wangu umefungwa minyororo nashindwa Cha kufanya😭😭😭

View attachment 2808722

Na umri wangu huu nikiumwa ikahitaji milioni 1 TU haki vile nitakufa huku najiona. Umri wa mama yangu unaenda Kwa Kasi itafikia kipindi ataitaji msaada wangu.

Na Mimi Bado najitafuta japo namuomba sana Mungu anisaidie nijipate haraka. Na Nina muomba sana Mungu asimchukue mama yangu kabla sijajipata. Na ni Bora anichukue Mimi kwanza japo natamani sana siku Mungu atakayonichukua anichukue nikiwa nimemuacha Mama yangu pazuri 😭😭😭

Mwenzenu najuta sana kumpa mama yangu UMASIKINI​
Pambana dogo janja acha kulialia na kubweteka na kukumbuka historia za kibwege kama izo
 
Mtoa Mada upo too negative
Usibadilisha mindest itakuchukua Muda mrefu kufikia MAFANIKIO

Acha kuongea maneno negative Kama hayo kwa kufanya hivyo unairuhusu hiyo hali kutawala Maisha yako.

Acha kulalamika
Kuwa mtu kushukuru jjfunze the power of Gratitude

Kila wakati kuwa mtu wa Kulivaa tumaini
 
Sioni uhusiano hapo mimi mama yangu mkubwa hakusoma darasa hata moja hajui hata kuandika ila watoto wake wote wako Sydney -Australia.Mimi mama yangu alisoma soma ila mwanae nipo bado natombanisha mijusi tu.Kaza wewe maisha yako ni jukumu lako hata ulie kuanzia sasa mpaka Jan,2024 hakuna kitakachobadilika zaidi ya kupambana.
 
Shukrani sana. Japo nimebahatika kumletea wajukuu🤣🤣 🤣 hivyo hata nikitangulia wajukuu zake SI wapo watareplace nafasi yangu...​
Hakuna kitu kina replace thamani ya mtoto Kwa mama.... mtoto wako thamani yake anaijua aliyemzaa na wewe...ngoja nikupe swali la kizushi, what if umeshakufa halafu inakuja kujulikana kabisa Kwa vinasaba huyo mtoto kumbe ulipewa tu zawadi kumbe ni wa Denis? 😁😁😁
 
Nikadhani uliiba mali za mama yako, kumbe alibeba mimba yako. Sasa wewe unahusikaje kwenye hilo? Kwani mchakato huo wa mimba Wewe ulihusika?

ndio maana under 30, mnajiua sana siku hizi.
 
Tatizo ni kutomshirikisha baba yako kwenye lawama zako. Nyie watoto mliolishwa maneno ovu na mama zenu siku zote mnawachukulia baba zenu kama hamnazo.

Na mtaishia pabaya siku zote.

Imeandikwa waheshimu Baba na Mama yako upate heri na siku nyingj duniani.
Sawa...
 
Back
Top Bottom