Najuta kumtia umasikini Mama yangu

Najuta kumtia umasikini Mama yangu

Sidhani kama ajutii japo aniambii ila dah. Inatia hudhuni imagine marafiki zangu niliosoma nao 75% wanaajira zinazoeleweka.

Inafikia kipindi mama nikimpigia simu ananiambia mtafute rafiki yako Fulani pengine anaweza kukuunganishia kazi.

Huku huyo rafiki yangu nikiwa Sina mawasiliano nae yoyote SI unajua tena Kila hatua mtu anayo piga anakuwa na marafiki wapya.

Nina miaka 30+ lakini Bado 75% ya maisha yangu IPO mikononi Kwa mama.​
Wakati wa Mungu ni wakati sahihi,itafika siku Yako....halafu acha mawazo ya kutamani kufa kabla ya mama Yako,omba sana neema ya kumzika mama Yako kama Kweli unampenda...mama kuzika mtoto ni uchungu usioelezeka
 
Huyu ndg yetu inaonekana amelelewa na mama peke yake, bahati mbaya zaidi akalelewa kimama (huenda akawa ni mtoto wa pekee) kwahyo amekuja kushtuka akiwa amechelewa kidogo😀

Princes, Kijana wa kiume hutakiwi kulaumu kitu kama hicho, yaani unatamani mama angetoa mimba😳😳

Umasikini haujaanzia kwako wala kwa mama yako, kuna watu ni maskini ukiwaona hitojitambua kama masikini tena ila wao wameridhika na hawana wa kumlaumu..

Pamoja na hayo si kila aleyesoma alipata kazi mwaka 90 sio mbali kihivo.. kwani wangapi ni wasomi wazuri lakini hawana kazi? Huwaoni??

Huenda mama yako hata bila kubeba mimba asingepata kazi na maisha yangeenda tu na hivyo ndivyo ilikuwa, kwani pamoja na kutoajiriwa; aliwezaje kukulea na mpaka sasa umesema unamtegemea kwa kiasi kikubwa na bado wewe unamzidi elimu, anawezaje?
Umeiweka vizuri mkuu! Anatakiwa kufanyia kazi mambo mengi sana.
 
Mimi ni kijana Ambae nimezaliwa mwanzoni mwa mwaka 1990. Hapa hapa kwenye jiji la MAKONDA. Japo Baba na Mama yangu Kila mmoja ni mwenyeji wa mkoa wake.

Mama yangu alibahatika kusoma Hadi darasa la 7. Alifanikiwa kusoma typing enzi hizo ilikuwa hot sana kozi hiyo kama ilivyo computer siku hizi. Alisomeshwa hiyo kozi ili atafutiwe kazi ukizingatia kuwa mjomba wake alikuwa na cheo kikubwa TU wizara ya AFYA {R.I.P BABU}

Bahati haikuwa yake kwani katika harakati hizo za kutafutiwa kazi ikagundulika kuwa yeye Mama ni mjamzito. Hapo ndipo maisha yake yalipoanza kuwa ya kawaida nadhani mimba hiyo ilimtoa kabisa kwenye reli😭😭😭

Wenzie aliosoma nao enzi hizo Wana maisha mazuri na majina makubwa mfano Mtendaji mkuu wa NMB. Mh Ruth Zaipuna amesoma na mama yangu darasa Moja.

Nisingekuwa mimi kuja Duniani pengine mama yangu hivi sasa angekuwa mbali sana kimaisha.

Ujio wangu hapa Dunia umefanya mama amekuwa na maisha ya kawaida sana. Amehangaika sana na kwa kiasi Fulani Bado ananihangaikia😭😭😭

Nina huzuni sana licha ya kuwa nimesoma lakini elimu yangu haijanisaidia. Ni kama ubongo wangu umefungwa minyororo nashindwa Cha kufanya😭😭😭

View attachment 2808722

Na umri wangu huu nikiumwa ikahitaji milioni 1 TU haki vile nitakufa huku najiona. Umri wa mama yangu unaenda Kwa Kasi itafikia kipindi ataitaji msaada wangu.

Na Mimi Bado najitafuta japo namuomba sana Mungu anisaidie nijipate haraka. Na Nina muomba sana Mungu asimchukue mama yangu kabla sijajipata. Na ni Bora anichukue Mimi kwanza japo natamani sana siku Mungu atakayonichukua anichukue nikiwa nimemuacha Mama yangu pazuri 😭😭😭

Mwenzenu najuta sana kumpa mama yangu UMASIKINI​
Huwezi.jua,ukipata labda utakufa kifuani kwa Malaya,hebu jaribu kuanzisha kitu ukipendacho.
 
Kila kitu unachokiona dunia hii ni siri na ukiijua siri itakuweka huru.

Unataka kuendelea kuishi hayo maisha unayoishi sasa, itafute SIRI ya maisha yako.....
 
Wakati wa Mungu ni wakati sahihi,itafika siku Yako....halafu acha mawazo ya kutamani kufa kabla ya mama Yako,omba sana neema ya kumzika mama Yako kama Kweli unampenda...mama kuzika mtoto ni uchungu usioelezeka
Shukrani sana. Japo nimebahatika kumletea wajukuu🤣🤣🤣 hivyo hata nikitangulia wajukuu zake SI wapo watareplace nafasi yangu...​
 
Back
Top Bottom